Umuhimu wa serikali kutumia wazawa kiuchumi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
upo mjadala mkubwa juu ya uzawa na makampuni ya nje katika kutekeleza shughuli za kiuchumi, mimi binafsi taaluma yangu ni mhandisi ila natamani sana ningesoma uchumi maana Tanzania sioni wachumi kabisa, inawezekana wapo lakini walikuwa wanatumia madesa hivyo kazini hawajapata madesa sijui, inawezekana wanasisa na viongozi hawawapi nafasi kutumia taaluma zao sijui sababu kwa nini hawatumikii nchi yetu nadhani wanajua wenyewe na wakipenda watatueleza. swala ninalotaka waeleza watanzania ni kuwa serikali kutumia wanachi wake kutika shughuli za kimaendeleo ndilo chaguo la kwanza kiuchumi. hii inatokana na ukweli kuwa serikali inamiliki fedha zilizo katika mzunguko wake wa ndani kwa maana ya fedha huanzia serikalini zinazunguka kwa wananchi na kurudi serikalini kwa njia tofauti mfano serikali inalipa watumishi mishahara inakata kodi hivyo sehemu ya fedha inarudi serikalini na iliyobaki mtumishi anaipeleka katika mzunguko. mtumishi huyu kila napofanya manunuzi analipa kodi tena hivyo fedha nyingine katika ile iliyobaki inarudi serikalini tena, wale waliopokea ela kutoka kwa mtumishi na wao wanapotaka kuitoa kufanya manunuzi yoyote wanakatwa kodi hivyo sehemu nyingine inarudi serikalini mwisho wa siku unakuta fedha yote inazunguka kwa wananchi ikiwatatulia matatizo yao na kurudi serikalini na serikali huingiza tena kwa wananchi na hivyo ndivyo ninavyoelewa mzunguko wa fedha. Sasa hapa linakuja swala la nchi kuinua uchumi wake ni kwa kuzuia fedha zilizo katika mzunguko wake zisitoke nje ya mipaka ya nchi na kujaribu kuchota fedha katika mizunguko ya nchi nyingine na kuleta katika mzunguko wake. hili kiuchumi huitwa kuongeza mauzo nje na kupunguza manunuzi nje. sasa nchi inapokuwa inatekeleza mradi wa maendeleo kwa mfano ukichukua fedha ukaitenga ukachukua kampuni ya kutoka nje kuja kufanya mradi huo mfano ni ujenzi wa barabara asilimia kubwa ya fedha itapelekwa kampuni hiyo ilikotoka hivyo fedha nyingi itatoka nje ya mipaka na hilo ni swala la kudidimiza uchumi na nchi inalifanya pale tu kwa ndani inapokuwa hakuna uwezekano wa kuufanya mradi kama huo hivyo kwa sababu kutokuwa na barabara ni kudidimiza uchumi zaidi kuliko kuachia bilioni kadhaa zikaenda nje. lakini kama ni mradi huo huo wa barabara unakuwa na kampuni ya nchini mwako ambayo itatumia vifaa kutoka ndani na faida kubaki ndani wanapomaliza kutengeneza barabara serikali inabaki na barabara na fedha inakuwa bado mali yake kwani zimeingia katika mzunguko wake na kuna na inaendelea kuzitumia. KWA SERIKALI YENYE WACHUMI HAIWEZI KUSEMA HATA SIKU MOJA KUWA KAMPUNI YA NJE IMETENDA GHARAMA NDOGO HIVYO INAAMUA KUNAGALIA BAJETI ALIYONAYO MKONONI KUBAKIZA FEDHA KIDOGO NA KURUHUSU MABILIONI KUTOKA NJE. ukienda katika madini, wachimbaji wadogo wanainua uchumi zaidi kama ni wazalendo kuliko makampuni ya nje. ni kwa vipi swala hili linaangaliwa kwa kuangalia mzunguko wa fedha ndani ya nchi yako na si kodi tu. kiasi alichochimba mchimbaji mdogo kwa mwaka ni fedha kiasi gani ya mapato ya madini inaingia katika mzunguko wa fedha wa nchi kwa asilimia ya mapato yote ya mauzo na kwa mchimbaji ambaye ni kampuni kubwa ya nje ni asilimia kiasi gani inabaki katika mzunguko wako wa fedha wa ndani. tatizo kubwa linalotafuna nchi yetu ni Corruption kwani nchi imekwisha jenga uwezo mkubwa kwa wataalamu lakini undugu, kujuana, rushwa vinatafuna nchi yetu. mradi ukija wakisema wapewe wazalendo watu wanapeana kwa kujauna, kwa rushwa bila kujali utaalamu na mwisho wa siku mradi haukamiliki au ubora wake unakuwa wa chini. cha kusikitisha ni pale makampuni ya nje yanapoleta watu hawana uzoefu kabisa wanajifunzia kwetu na tunawaona bora. KUDUMISHA UCHUMI SI LAZIMA UUZE NJE TU BALI HATA KUWEKA SERA YA KUZUIA FEDHA KUTOKA NJE MFANO TANZANIA TUNATUMIA FEDHA KIASI GANI KWA MWAKA KATIKA BAJETI YA SERIKALI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO. JE TUMEWAHI KUJIULIZA NI KIASI GANI CHA FEDHA HIZO KINABAKI KATIKA MZUNGUKO WETU WA NDANI? JE TUMEWEKA SERA GANI YA KUHAKIKISHA ASILIMIA KUBWA YA HIZO FEDHA ZINABAKI KATIKA MZUNGUKO WETU WA NDANI NA KUINUA UCHUMI WETU.
 
Watanzania tuna mikakati gani kutumia gesi yetu kuzuia fedha ya mafuta inayokwenda nje, tuna mikakati gani kuinua wazawa ili tuzuia fedha ya maendleo katika miradi inayokwenda nje, tuna mikakati gani kuzuia uingizaji wa vitu vya electronic feki kama simu. Kwa mikakati bora ya kiuchumi katika nyanja hizi tutapiga hatua kubwa kiuchumi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom