Umuhimu wa mikopo katika utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati na maendeleo ya Wananchi

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Kuna mjadala unaoendelea kuhusu nchi kukopa au kutokukopa. Kama mwananchi wa kawaida nani ningependa kutoa mtazamo wangu kwa faida ya wote.

Kwanza ni muhumu ikafahamika kwamba HAKUNA nchi duniani inayotekeleza miradi ya maendeleo bila kukopa. Hata nchi tajiri ulimwenguni zinakopa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ndio maana unasikia Marekani inauza Treasury Bonds zake na nchi kama China inazinunua za thamani hadi dola za Trilioni 1 huko ndio kukopa kwenyewe ili watekeleze miradi ya maendeleo.

Takwimu za Mkopo wa dunia global debt -2020 zinaonesha nchi tajiri ndio zilizoongoza kukopa.

Marekani peke yake deni lake lilikuwa asilimia 31.8 ya deni la dunia; Japan deni lao lilikuwa asilimia 18.8 ya deni la Dunia; Uingereza share yao ilikuwa ni asilimia 3.7; Ufaransa ailikuwa asilimia 3.8. Nchi 54 za Afrika deni lao kwa pamoja (combined) ni asilimia 2 tu.

Hiyo ndio sababu hadi leo Afrika tunakabiliwa na changamoto za kutokuwa na barabara za kutosha, hatuna reli za kutosha; hatuna maji ya kutosha; hatuna vituo vya afya vya kutosha; hatuna madarasa ya kutosha nk.

Wakati nchi za Afrika hazikopi vya kutosha ili kuweka hiyo miundombinu ya msingi; nchi tajiri zilizoendelea wanakopa ku-upgrade miundombinu ambayo tayari wanayo. Kwa mfano hivi sasa China wanayo reli ambayo treni inasafiri kwa spidi ya km 300 kwa saa; sasa wamekopa kujenga reli yenye spidi ya kilomita 600 kwa saa. Sasa kuna kosa gani sisi kukopa kujenga barabara?

Kama Nchi tajiri zinakopa kuvumbua teknolojia itakayofanya uzalishaji viwandani ufanywe na robot badala ya binadamu- kuna kosa gani sisi kukopa kwa ajili kujenga madarasa yatakayosaidia watoto wetu wasome kwa staha? Kama wenzetu wanakopa kwa ajili ya kwenda Mwezini.

Binafsi sioni ubaya. Hivyo ni muhimu sana kuielewa dhana ya nchi kukopa sio jambo geni na wala sio jambo baya na kila nchi duniani inakopa.

Serikali inavyokopa kutekeleza miradi muhimu ya maendeleo inapaswa kuungwa mkono na sio kubezwa.Jambo la msingi ni lile alilosema Rais kwamba tunapokopa miradi itekelezwe kwa ufanisi nakuzingatia thamani ya fedha inayotumika kutelekeza mradi "value for money"
 
Kinachosikitisha sana ni pale nchi inapokopa kwa ajili ya miradi ambayo serikali yenyewe haina wataalam wa kuisimamia kisayansi. Badala yake wanaenda kuajiri wataalam kutoka huko huko ilikotoka hiyo mikopo.
 
Back
Top Bottom