SoC02 Umuhimu wa Mikataba na faida za kusimamia mikataba katika utendaji nchini

Stories of Change - 2022 Competition

Theb

JF-Expert Member
Jan 25, 2019
3,929
7,268
Andiko langu litakuwa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza itakuwa ni utangulizi hapa nitaelezea maana ya mikataba na faida ya mikataba, sehemu ya pili nitaelezea mikataba iliyoleta migogoro au sintofahamu katika mambo mbali mbali nchini. Sehemu ya tatu itakuwa ya mwisho hapo nitatoa ushauri pamoja na maoni yangu.

MKATABA
Mkataba, kwa ufafanuzi rahisi zaidi, ahadi inayotekelezeka kwa sheria. Ahadi inaweza kuwa kufanya jambo fulani au kutofanya jambo fulani. Uundaji wa mkataba unahitaji idhini ya pande zote ya watu wawili au zaidi, mmoja wao kwa kawaida akitoa ofa na mwingine akikubali. Iwapo mmoja wa wahusika atashindwa kutimiza ahadi, mwingine ana haki ya kusuluhishwa kisheria.

Sheria ya mikataba inazingatia maswali kama vile mkataba upo, nini maana yake, kama mkataba umevunjwa, na ni fidia gani inastahili kulipwa mhusika, (Maana kutoka Britannica).

Mikataba ina faida kama, kuonyesha makubaliano ya watu wawili au zaidi pamoja na mashahidi. Husaidia kupunguza migogoro sheria ikisimamiwa vizuri na Husaidia vyombo vya kisheria katika kufanya maamuzi iwapo kutatokea sintofahamu katika mkataba husika, pia huhakikisha ulinzi wa makubaliano husika. Yote hayo huchochea maendeleo, uwajibikaji, na mabadiliko katika jamii zetu.

IFUATAYO NI BAADHI YA MIKATABA ILIYOZUA UTATA KATIKA UTENDAJI NCHINI

1. MKATABA WA WANUFAIKA WA MKOPO WA ELIMU YA JUU NA BODI YA MIKOPO(heslb).

Mkataba huu wa bodi ya mikopo ulieleza kiasi ambacho kingerejeshwa na mnufaika wa mkopo kuwa ni asilimia 8 lakini utawala wa Hayati John Pombe Magufuli ulibatilisha na kuongeza marejesho yawe kwa asilimia 15. Ongezeko hilo la makato limepelekea wafanyakazi kulalamikia japo hawakufika katika vyombo vya sheria lakini liliwaathiri kiuchumi. CAG alithibitisha hili alisema:-

"Nilibaini upungufu huu unatokana na sheria mpya ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyoongeza makato ya wanufaika kutoka asilimia nane hadi 15 ya mshahara,” amesema CAG kwenye ripoti yake.(Nukuu ya CAG Charles Kichere, Mwananchi).

2. MKATABA WA MCHEZAJI BERNARD MORRISON NA TIMU YA MPIRA YANGA SC.
Kwa wapenda mpira wote nchini hakuna asie kumbuka hili. November 22, 2021 Mahakama ya Usuluhishi katika Michezo CAS, Ilitoa maamuzi katika kesi ya mchezaji Morrison na Timu ya Yanga kwa kutupilia mbali rufaa ya timu ya yanga kwa kuona dosari zilizopo kwenye mkataba wa Yanga walioupeleka kule CAS.

Screenshot_20211122-170056_WPS Office (1).jpg

Picha maamuzi ya CAS baina ya Morrison vs Yanga. (Picha kutoka mtandaoni).

3. MKATABA WA MWANAMUZIKI RICH MAVOKO NA WASAFI.
Mkataba wa mwimbaji wa bongo fleva Rich Mavoko na lebo ya Wasafi nao uliingia katika mgogoro. Kwa maana mwimbaji Rich Mavoko alitambua kuwa mkataba ule ulidhamiria kuathiri taaluma yake pamoja na mapato yake. Kwa msaada wa (BASATA) Baraza la Sanaa Tanzania mwimbaji Rich Mavoko alishinda kesi na mkataba ukavunywa. (Taarifa zilitangazwa mitandaoni)
Rich.jpg

Rich mavoko akisaini kujiunga na WCB ya diamond platnumz. (Picha kutoka mtandaoni)

4. MIKATABA BAINA YA WAMILIKI WA VIWANDA NA WAFANYAKAZI WA VIWANDA.
Mikataba inayotolewa na wamiliki wa viwanda nchini kwa wafanyakazi wa viwandani hususani wale wa kazi ndogo ndogo kama kupanga bidhaa, kupakiza bidhaa, kufanya usafi, kushona mabox na mifuko. Mikataba wanayopewa kundi hili huwa haina msaada kwa wafanyakazi. Haiwalindi, muda wowote hata bila kosa wanaweza kufukuzwa au kutolipwa. Mikataba hii kwenye viwanda ni bora vyama vya wafanyakazi pamoja na serikali ikaitazama kwa faida ya wote.

5. MIKATABA YA SHULE NA HOSPITALI ZA MASHIRIKA BINAFSI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WAKE.
Mikataba inayotolewa na mashirika ya shule binafsi nchini kwa baadhi sio yote haipo sawa. Zipo shule nyingi walimu wanafundisha kwa kukubaliana kwa njia ya mdomo bila kupeana mkataba unaoeleweka. Jambo hili ni hatari kwa mwajiriwa kwa maana anaweza dhulumiwa au kufutwa kazi bila taarifa ya kueleweka. Katika hospitali za binafsi baadhi nazo zinafanya hivyo hivyo.

6. MIKATABA YA MAUZIANO NA SHUGHULI ZINGINE NDOGO NDOGO KATIKA JAMII ZETU.
Mikataba inayotolewa katika mauziano mbali mbali kwenye jamii zetu hususani katika kuuziana ardhi, mikataba mingi ina mapungufu yanayopelekea kuibuka kwa migogoro. Zipo kesi nyingi za migogoro ya ardhi zilizosababishwa na mikataba mibovu. Zipo mali nyingi zimewekewa zuio na mahakama kutokana na sintofahamu iliyopo katika mauziano kwenye mikataba husika. Jambo hili ni kubwa katika jamii zetu.

7. MIKATABA KWENYE ASASI ZA MIKOPO BAINA YA MKOPAJI NA WATOA MIKOPO.
Mara nyingi katika kukopa wengi wanashindwa kusoma na kuelewa mikataba husika. Jambo hili huzua simtofahamu au migogoro kwenye kufanya marejesho. Ni vyema mkopaji na mkopeshaji wakakaa pamoja na kuandaa mkataba utakao bainisha hatua zote za kufanya ili kupata mkopo na njia zitakazo tumika kurejesha mkopo. Na sio mkopeshaji anaandaa mwenyewe mkataba na kuutumia bila kumsikiliza mkopaji. Jambo hili likisimamiwa litasaidia kupunguza kufirisiana katika jamii zetu. Kwa maana mlipaji akijieleza na kutoa mapendekezo yake yanayoeleweka na kukubalika katika mkataba yatasaidia kuondoa migogoro.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI, JAMII NA MASHIRIKA BINAFSI KUHUSIANA NA MIGOGORO YA KIMIKATABA.

1. Elimu itolewe kwa jamii kuhusu umuhimu wa mikataba kwenye mauziano, makubaliano na maamuzi. Jamii zetu zielimishwe kwa kuelezwa umuhimu uliopo iwapo mambo yakifanyika kwa mikataba inayozingatia taratibu za kisheria. Hii itasaidia kuondoa migogoro.

2. Mikataba iwe moja ya mada(Topic) katika mitaala yetu ya elimu nchini. Wanafunzi wetu nchini wafundishwe kuhusu mikataba kwenye somo la uraia(civics) na General Studies kwa advanced level. Hii itasaidia kuandaa kizazi kinachojua misingi na taratibu za mikataba. Dunia ya leo mambo mengi huendeshwa kwa mikataba.

3. Vyombo vya sheria kama mahakama, polisi na serikali za mitaa vitoe ushirikiano zaidi inapohitajika kwa wananchi. Wananchi wanapohitaji kutambua hatua za kufuata ili kufanya mikataba baina yao au na taasisi yoyote ni vema vyombo vya sheria vikawa tayari kuwa patia mwongozo.

4. Serikali ifuatilie mikataba inayotolewa na mashirika binafsi kwa wafanyakazi wake. Serikali yetu pia ifuatilie kwa kina mikataba wanayopewa wananchi wake kwenye viwanda, shule binafsi, hospitali binafsi ili itambue na kuona je mikataba hiyo inaeleweka na inakidhi vigezo vya kimikataba.

5. Viongozi waache kubatilisha mikataba kwa mihemko bali wafuate mashauriano na maridhiano ya kisheria kwa faida ya wote. Viongozi wetu wakifuatilia mikataba ni jambo jema ila wakibatilisha mikataba kwa mihemko na sio kwa kuzingatia sheria itazua migogoro. Mfano mkataba wa wanufaika wa bodi ya mikopo, uongozi wa awamu ya tano haukutumia sheria kuongeza makato kutoka asilimia 8 hadi 15.
 
Andiko langu litakuwa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza itakuwa ni utangulizi hapa nitaelezea maana ya mikataba na faida ya mikataba, sehemu ya pili nitaelezea mikataba iliyoleta migogoro au sintofahamu katika mambo mbali mbali nchini. Sehemu ya tatu itakuwa ya mwisho hapo nitatoa ushauri pamoja na maoni yangu.

MKATABA
Mkataba, kwa ufafanuzi rahisi zaidi, ahadi inayotekelezeka kwa sheria. Ahadi inaweza kuwa kufanya jambo fulani au kutofanya jambo fulani. Uundaji wa mkataba unahitaji idhini ya pande zote ya watu wawili au zaidi, mmoja wao kwa kawaida akitoa ofa na mwingine akikubali. Iwapo mmoja wa wahusika atashindwa kutimiza ahadi, mwingine ana haki ya kusuluhishwa kisheria.

Sheria ya mikataba inazingatia maswali kama vile mkataba upo, nini maana yake, kama mkataba umevunjwa, na ni fidia gani inastahili kulipwa mhusika, (Maana kutoka Britannica).

Mikataba ina faida kama, kuonyesha makubaliano ya watu wawili au zaidi pamoja na mashahidi. Husaidia kupunguza migogoro sheria ikisimamiwa vizuri na Husaidia vyombo vya kisheria katika kufanya maamuzi iwapo kutatokea sintofahamu katika mkataba husika, pia huhakikisha ulinzi wa makubaliano husika. Yote hayo huchochea maendeleo, uwajibikaji, na mabadiliko katika jamii zetu.

IFUATAYO NI BAADHI YA MIKATABA ILIYOZUA UTATA KATIKA UTENDAJI NCHINI

1. MKATABA WA WANUFAIKA WA MKOPO WA ELIMU YA JUU NA BODI YA MIKOPO(heslb).

Mkataba huu wa bodi ya mikopo ulieleza kiasi ambacho kingerejeshwa na mnufaika wa mkopo kuwa ni asilimia 8 lakini utawala wa Hayati John Pombe Magufuli ulibatilisha na kuongeza marejesho yawe kwa asilimia 15. Ongezeko hilo la makato limepelekea wafanyakazi kulalamikia japo hawakufika katika vyombo vya sheria lakini liliwaathiri kiuchumi. CAG alithibitisha hili alisema:-

"Nilibaini upungufu huu unatokana na sheria mpya ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iliyoongeza makato ya wanufaika kutoka asilimia nane hadi 15 ya mshahara,” amesema CAG kwenye ripoti yake.(Nukuu ya CAG Charles Kichere, Mwananchi).

2. MKATABA WA MCHEZAJI BERNARD MORRISON NA TIMU YA MPIRA YANGA SC.
Kwa wapenda mpira wote nchini hakuna asie kumbuka hili. November 22, 2021 Mahakama ya Usuluhishi katika Michezo CAS, Ilitoa maamuzi katika kesi ya mchezaji Morrison na Timu ya Yanga kwa kutupilia mbali rufaa ya timu ya yanga kwa kuona dosari zilizopo kwenye mkataba wa Yanga walioupeleka kule CAS.

View attachment 2292264
Picha maamuzi ya CAS baina ya Morrison vs Yanga. (Picha kutoka mtandaoni).

3. MKATABA WA MWANAMUZIKI RICH MAVOKO NA WASAFI.
Mkataba wa mwimbaji wa bongo fleva Rich Mavoko na lebo ya Wasafi nao uliingia katika mgogoro. Kwa maana mwimbaji Rich Mavoko alitambua kuwa mkataba ule ulidhamiria kuathiri taaluma yake pamoja na mapato yake. Kwa msaada wa (BASATA) Baraza la Sanaa Tanzania mwimbaji Rich Mavoko alishinda kesi na mkataba ukavunywa. (Taarifa zilitangazwa mitandaoni)
View attachment 2293052
Rich mavoko akisaini kujiunga na WCB ya diamond platnumz. (Picha kutoka mtandaoni)

4. MIKATABA BAINA YA WAMILIKI WA VIWANDA NA WAFANYAKAZI WAVIWANDA.
Mikataba inayotolewa na wamiliki wa viwanda nchini kwa wafanyakazi wa viwandani hususani wale wa kazi ndogo ndogo kama kupanga bidhaa, kupakiza bidhaa, kufanya usafi, kushona mabox na mifuko. Mikataba wanayopewa kundi hili huwa haina msaada kwa wafanyakazi. Haiwalindi, muda wowote hata bila kosa wanaweza kufukuzwa au kutolipwa. Mikataba hii kwenye viwanda ni bora vyama vya wafanyakazi pamoja na serikali ikaitazama kwa faida ya wote.

5. MIKATABA YA SHULE NA HOSPITALI ZA MASHIRIKA BINAFSI PAMOJA NA WAFANYAKAZI WAKE.
Mikataba inayotolewa na mashirika ya shule binafsi nchini kwa baadhi sio yote haipo sawa. Zipo shule nyingi walimu wanafundisha kwa kukubaliana kwa njia ya mdomo bila kupeana mkataba unaoeleweka. Jambo hili ni hatari kwa mwajiriwa kwa maana anaweza dhulumiwa au kufutwa kazi bila taarifa ya kueleweka. Katika hospitali za binafsi baadhi nazo zinafanya hivyo hivyo.

6. MIKATABA YA MAUZIANO NA SHUGHULI ZINGINE NDOGO NDOGO KATIKA JAMII ZETU.
Mikataba inayotolewa katika mauziano mbali mbali kwenye jamii zetu hususani katika kuuziana ardhi, mikataba mingi ina mapungufu yanayopelekea kuibuka kwa migogoro. Zipo kesi nyingi za migogoro ya ardhi zilizosababishwa na mikataba mibovu. Zipo mali nyingi zimewekewa zuio na mahakama kutokana na sintofahamu iliyopo katika mauziano kwenye mikataba husika. Jambo hili ni kubwa katika jamii zetu.

7. MIKATABA KWENYE ASASI ZA MIKOPO BAINA YA MKOPAJI NA WATOA MIKOPO.
Mara nyingi katika kukopa wengi wanashindwa kusoma na kuelewa mikataba husika. Jambo hili huzua simtofahamu au migogoro kwenye kufanya marejesho. Ni vyema mkopaji na mkopeshaji wakakaa pamoja na kuandaa mkataba utakao bainisha hatua zote za kufanya ili kupata mkopo na njia zitakazo tumika kurejesha mkopo. Na sio mkopeshaji anaandaa mwenyewe mkataba na kuutumia bila kumsikiliza mkopaji. Jambo hili likisimamiwa litasaidia kupunguza utaifishaji katika jamii zetu. Kwa maana mlipaji akijeleza na kutoa mapendekezo yake yanaoeleweka na kukubalika katika mkataba yatasaidia kuondoa migogoro.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI, JAMII NA MASHIRIKA BINAFSI KUHUSIANA NA MIGOGORO YA KIMIKATABA.

1. Elimu itolewe kwa jamii kuhusu umuhimu wa mikataba kwenye mauziano, makubaliano na maamuzi. Jamii zetu zielimishwe kwa kuelezwa umuhimu uliopo iwapo mambo yakifanyika kwa mikataba inayozingatia taratibu za kisheria. Hii itasaidia kuondoa migogoro.

2. Mikataba iwe moja ya mada(Topic) katika mitaala yetu ya elimu nchini. Wanafunzi wetu nchini wafundishwe kuhusu mikataba kwenye somo la uraia(civics) na General Studies kwa advanced level. Hii itasaidia kuandaa kizazi kinachojua misingi na taratibu za mikataba. Dunia ya leo mambo mengi huendeshwa kwa mikataba.

3. Vyombo vya sheria kama mahakama, polisi na serikali za mitaa vitoe ushirikiano inapohitajika kwa wananchi. Wananchi wanapohitaji kutambua hatua za kufuata ili kufanya mikataba baina yao au na taasisi yoyote ni vema vyombo vya sheria vikawa tayari kuwa patia mwongozo.

4. Serikali ifuatilie mikataba inayotolewa na mashirika binafsi kwa wafanyakazi wake. Serikali yetu pia ifuatilie kwa kina mikataba wanayopewa wananchi wake kwenye viwanda, shule binafsi, hospitali binafsi ili itambue na kuona je mikataba hiyo inaeleweka na inakidhi vigezo vya kimikataba.

6. Viongozi waache kubatilisha mikataba kwa mihemko bali wafuate mashauriano na maridhiano ya kisheria kwa faida ya wote. Viongozi wetu wakifuatilia mikataba ni jambo jema ila wakibatilisha mikataba kwa mihemko na sio kwa kuzingatia sheria itazua migogoro. Mfano mkataba wa wanufaika wa bodi ya mikopo, uongozi wa awamu ya tano haukutumia sheria kuongeza makato kutoka asilimia 8 hadi
Safi sana.
 
Mifano ya watu wasioheshimu mikataba ipo mingi na kwa wadau manaosoma uzi tunaomba mawazo yenu na mifano yenu ikiwepo. Pia msisahau kura zenu
 
Back
Top Bottom