Umuhimu wa mifumo ktk nchi hasa linapokuja suala la kitaifa kama Sensa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa mifumo ktk nchi hasa linapokuja suala la kitaifa kama Sensa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HGYTXK, Aug 29, 2012.

 1. HGYTXK

  HGYTXK Senior Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Habari zenu wadau,mifumo ya uongozi ktk nchi ni suala muhimu sana ktk kusimamia mambo mbalimbali inayowahusu wananchi.Mifumo hii iliyoenziwa sana kipindi cha Mwl Nyerere inaonekana kutokuwa na umuhimu ktk kizazi cha serikali zetu za Dot com za hizi zama.Tulifundishwa enzi hizo shule ya msingi ktk somo la Uraia kuwa nchi imegawanyika ktk sehemu mbalimbali za utendaji ikianzia nyumba moja moja hadi kufikia taifani.Nimesukumwa kuandika haya baada ya kuona jinsi zoezi la sensa linavyolegalega,nikichukulia mfano mimi mwenyewe mpaka hivi sasa siku ya takribani ya 4 toka sensa ianze bado sijafikiwa na na wahesabu sensa nikiwa nyumbani wala ofisini.Kwa nchi ambayo iko makini ktk kuangalia njia za kuwafikia wananchi wake zoezi la kujua idadi ya watu wake ktk nchi inaweza kupata ata kila baada ya mwezi kama ikitaka na taarifa zikawa sahihi kabisa.tuchukulie mfano wa kipindi ambacho mitihani ya darasa la saba inafanyika na usambazaji wa mitihani,ukusanywaji mpaka usahihishwaji unavyofanyika.Huku inawezekana labda kwa sababu ya u-smart wa waalimu ktk kufanya mambo yao.
  kwa mtazamo wangu zoezi la sensa lingeweza kusimamiwa na viongozi wa serikali kama sehemu ya kazi zao na ingeweza kuchukua muda mfupi sana.Tungeanza kutoa siku moja tu kwa kila balozi wa nyumba 10 nchi nzima kuhakikisha anatembelea nyumba zake na kukifanya hiki ambacho hawa wahesabu sensa wanakifanya hivi sasa,siku inayofuata ingekuwa ni wakati wa hao mabalozi kuwasilisha taarifa zao kwa mwenyekiti wa mtaa husika ambaye akishirikiana na wajumbe wake wa baraza la kijiji wangefanya majumuhisho ya mtaa mzima kwa siku moja tu kabla ya siku inayofuata kuwasilisha majumuhisho hayo kwa katibu kata wa kata husika na makatibu kata kuwasilisha majumuhisho yao kwa makatibu tarafa kwa siku hiyo hiyo kabla ya makatibu tarafa kuzipeleka taarifa hizo wilayani na wilaya kuoanisha taarifa kutoka kila tarafa na kuzipeleka mkoani ambako nako kungefanyika majumuhisho tayari kwa kutumwa taifani.Kwa mfumo huu ni Balozi wa nyumba 10,Mwenyekiti wa mtaa/wajumbe wake,Katibu kata,katibu tarafa,mkuu wa wilaya na sekretari yake na mkuu wa mkoa na sekretari yake ndio pekee wangeifanya hii kazi ktk siku zisizozidi 5 na wakiwa wanapokezana vijiti na kuwaacha wakiwa hawako bored na kazi.Ni mfumo huu pekee ndio ungehakikisha kila mtu anafikiwa ktk sensa hii kwani mabalozi wanawajua watu wao wote na ata hizo guest houses,hospitals na stand zipo ndani ya hii mifumo niliyoitaja.
  Kwa kuwa serikali haikuona umuhimu wa hii mifumo ktk kutekeleza kazi zake ndio yanatokea haya yanayotokea leo.Zoezi jepesi sana linaonekana kuwa ni ngumu kutokana na ugumu uliowekwa na serikali yenyewe.Kwa mfumo nilioutaja inaonekana ni mabalozi pekee ndio wangekuwa na kazi ya kuhesabu watu wao na wengine wote ni wajumuhishaji.
  hapa ni elimu ya uraia tu ya darasa la saba inatumika kuyafanya haya yote na wala haikuitaji kuutumia u-Dr uwe wa darasani wala kupewa.Viongozi wetu muwe wabunifu katika kutekeleza majukumu yenu mbalimbali ya kitaifa ili kuokoa rasilimali na muda wa wananchi.ilitosha kuwalipa viongozi husika posho kidogo tu ili kutekeleza zoezi hili kuliko kuweka utitiri wa wahesabuji ambao wanashindwa kuendana na kasi kutokana na kutojua wanafanya hii kazi kwa kufuata mifumo gani rasmi.

  Huu ni mtazamo wangu tu wadau,Nawasilisha.
   
Loading...