Umuhimu wa mbogamboga na matunda yenye rangi nyekundu

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1611556434244.png

Vyakula vyekundu kama vile mbogamboga na matunda vina muunganiko wa kemikali iitwayo Phytochemicals, ambayo ina faida kubwa katika afya ya mwanadamu. Phytochemicals hizo ni pamoja na flavonoids, lycopene, reservatol na capsaicin.

Matunda na mboga nyekundu kama vile Nyanya, Zabibu nyekundu, Kitunguu chekundu, Komamanga, Pilipili hoho nyekundu, Tikiti na Tofaa jekuku huwa na vitamini C, potasiamu, na folate.

Matunda na mbogamboga nyekundu hufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama vile:-

Kuimarisha afya ya Moyo,

Kurekebisha kiwango cha sukari kwenye mwili,

Kuimarisha afya ya tezi dume,

Kudhibiti Lehemu kwenye mwili,

Kuimarisha afya ya njia ya mkojo na;

Kuimarisha afya ya vinasaba.

Hivyo kwa kutumia vyakula hivyo unaweza kuuepusha mwili na magonjwa yafuatayo:-

Shinikizo la damu,

Magonjwa ya moyo,

Kisukari,

Magonjwa ya Tezi dume na;

Saratani za aina mbalimbali.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom