Umuhimu wa mazoezi ya kunyanyua vitu vizito, kupiga chuma (Weight Training) kwa wanaume

George Betram

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
4,018
4,909
Heshima kwenu wanajukwaa.

Leo nataka niwape faida 7 wanazozipata wanaume wanaofanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito "wapiga nondo", kama haujawahi kufikiria kufanya aina hii ya mazoezi naamini baada ya kuziona faida hizi utaanza kufanya mazoezi haya.

1. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANAONGEZA UWEZO WA AKILI KUFANYA KAZI VIZURI

Mazoezi ya kunyanyua vyuma yanachochea uzalishaji wa homoni kama BDNF (Brain-Derived Neurotrophic Factor), homoni hizi husaidia uzalishaji wa seli mpya za ubongo. Bila kusahau mazoezi ya kunyanyua vitu vizito yanachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ukubwa wa " hippocampus",hii ni sehemu ya ubongo inayohusika na uhifadhi kumbukumbu.
Unataka kuwa "smart" kwa kichwa?

Kama jibu ni ndiyo,basi anza kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito,lakini usiache kusoma vitabu pia.

2. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANAONGEZA FURAHA
Watu wanaonyanyua vitu vizito ni watu wenye furaha sana. Ni kawaida kumuona mtu anayefanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito akiwa na tabasamu muda wote. Hali hii inasababishwa na uzalishaji mkubwa wa kemikali za "endorphins" kwenye miili ya watu wanaonyanyua vitu vizito. Kemikali hizi huzalishwa mwilini kwa lengo la kuufanya mwili usihisi maumivu pindi unapofanya mazoezi ya Kunyanyua vitu vizito.

3. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANALETA ULALAJI MZURI

Watu wanaonyanyua vitu vizito huwa wanalala usingizi mzuri sana, huwa hawana matatizo ya kukosa usingizi. Ulalaji mzuri ni sehemu ya kujenga afya, anza kufanya mazoezi haya.

4. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANAONGEZA HOMONI ZA KIUME

Watu wanaonyanyua vitu vizito wana kiwango kikubwa sana cha homoni za testosterone, hizi ni homoni muhimu katika kujenga mwili wa mwanaume. Kiwango kidogo cha homoni za testosterone huweza kusababisha uchovu, kudumaa na kukosa nguvu za kiume.

5. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANAONGEZA UWEZO WA KUJIAMINI
Watu wanaonyanyua vitu vizito ni watu wanaojiamini sana,hii inasababishwa na miili yao kujengeka vizuri. Lakini pia utafiti unaonesha kuwa kitendo cha kunyanyua vitu vizito pekee kinatosha kukufanya ufurahie muonekano wa mwili wako hivyo hiyo hali inakuongezea uwezo wa kujiamini mbele za watu.

6. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANAONGEZA MVUTO
Watu wanaonyanyua vitu vizito ni watu ambao misuli yao imejengeka vizuri,hivyo hiyo inawafanya kuwa watu wenye mvuto wa kipekee.

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wengi huwa wanadata/wanavutiwa sana na wanaume wenye mabega na vifua vipana. Unataka kuongeza mvuto na kupendwa na wanawake?
Piga chuma lakini tafuta pesa pia.

7. MAZOEZI YA KUNYANYUA VITU VIZITO YANAONGEZA UWEZO WA MWANAUME KUFANYA MAPENZI

Watu wanaofanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito wana uwezo mkubwa wa kufanya mapenzi muda mrefu bila kuchoka.

Utafiti unaonesha kuwa mazoezi ya kunyanyua vitu vizito yanaongeza uwezo wa sehemu za kiume kusimama vizuri na muda mrefu.

Unataka kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito lakini hauna vifaa vya kufanyia mazoezi haya?
Unataka kufanya mazoezi ya kunyanyua vitu vizito lakini hauna muda wa kwenda gym au haupendi kwenda gym?
Usijali, ninatengeneza mashine ya kufanyia mazoezi ya kunyanyua vitu vizito ambayo unaweza kuitumia kufanya mazoezi ya kujenga misuli ya mgongo, kifua, mabega, miguu na mikono.

Tofauti na mashine za kisasa kutoka nje,mashine hii ina uwezo wa kukaa muda mrefu bila kuharibika. Ukiagiza mashine hii nitakuletea mahali popote ulipo (Hii ni kwa mkoa wa Dar es Salaam tu). Mashine inapatikana kwa shilingi za kitanzania 450000/=

Kwanini ununue mashine hii kutoka kwangu?

I. Ni mashine unayoweza kuitumia kufanya karibia mazoezi yote ya kujenga viungo,hivyo mashine hii moja inakuepushia gharama ya kuwa na mashine nyingi kwaajili ya mazoezi tofauti tofauti.
II. Ni mashine inayopatikana kwa gharama nafuu ukilinganisha na mashine za kisasa kutoka nje (Tsh 450000)
III. Ni mashine imara kulinganisha na mashine za kisasa kutoka nje.
IV. Ukinunua mashine hii nitakupatia na chuma chenye uzito kilogram 10 bure.

Mawasiliano:
0692288398
0716418668

MASHINE NI HOME MADE (Ni ubunifu ambao nimeufanya mwenyewe)

IMG-20191024-WA0003.jpg


Chini ni videos jinsi mashine inavyotumika.


 
danganya tu wenzako wapenda sifa mjomba wangu alikuwa anajifanya mtemi na mivyuma yake, sasa hivi kapata ugonjwa wa kushake mikono mpka matako,vijana wengi wanajiona wajanja kunyanyua mivyuma but time will tell
 
Takataka ya nini? Tafuta hela bwa mdogo bila hela huwezi kufanya mapenzi
Mbona tunavunjiana heshima Chief?

Hivi umesoma uzi wangu wote kisha ukaona nimejikita katika hoja ya mapenzi?

Chief, stress/hasira zako zinazotokana na changamoto za maisha usizihamishie kwa watu ambao hawana hatia..!
 
danganya tu wenzako wapenda sifa mjomba wangu alikuwa anajifanya mtemi na mivyuma yake, sasa hivi kapata ugonjwa wa kushake mikono mpka matako,vijana wengi wanajiona wajanja kunyanyua mivyuma but time will tell
Uandishi wako unaonesha una CHUKI binafsi na huyo mjomba wako!

Chochote alichokufanyia hakifanyi hizi faida nilizoziandika katika huu uzi kuwa za uongo!

Maliza matatizo yako binafsi uliyokuwa nayo na huyo mjomba wako,CHUKI zako usizihamishie kwa watu wengine..!
 
Mbona tunavunjiana heshima Chief..?
Hivi umesoma uzi wangu wote kisha ukaona nimejikita katika hoja ya mapenzi..!?
Chief, stress/hasira zako zinazotokana na changamoto za maisha usizihamishie kwa watu ambao hawana hatia..!
It's my bad
 
danganya tu wenzako wapenda sifa mjomba wangu alikuwa anajifanya mtemi na mivyuma yake, sasa hivi kapata ugonjwa wa kushake mikono mpka matako,vijana wengi wanajiona wajanja kunyanyua mivyuma but time will tell
Sijakuelewa yani kapata ugonjw wa kufanyaje?

ukoje ukoje huo ugonjwa
 
Kuna jamaa kipindi tunasoma alikua anabeba chuma/nondo alikua na bonge la bodi ila akili darasani sifuri anaingia na vikaratasi kwenye mtihani. Ukimkagua kipindi anaingia kwenye mtihani hivo vikaratasi kidastibini kinajaa.
So point zako namba ngapi na namba ngapi UWONGO
 
Kuna jamaa kipindi tunasoma alikua anabeba chuma/nondo alikua na bonge la bodi ila akili darasani sifuri anaingia na vikaratasi kwenye mtihani. Ukimkagua kipindi anaingia kwenye mtihani hivo vikaratasi kidastibini kinajaa.
So point zako namba ngapi na namba ngapi UWONGO
Sijakuambia kupiga chuma kunakufanya ufaulu mtihani aisee..! Kama huyo jamaa alikuwa hana utaratibu wa kutenga muda wa kujisomea ulitegemea atafaulu kwa kupiga nondo tu..?
 
Nondo ina madhara unasababisha bawasili kutokana na ule msukumo kunyanyua uzito mkubwa zaidi.
Mkongwe...
Kila kitu usipokifanya kwa kiwango stahiki kina madhara, hata unyanyuaji wa chuma bila kufuata utaratibu mzuri una madhara..!
Bawasiri utaipata kama unanyanyua uzito mkubwa kuliko uzito unaotakiwa kunyanyua..!
Ukiacha baada ya miaka kadhaa kifua kinauma mara kwa mara. Nimebeba chuma zaidi ya miaka 8 nayaona madhara now.
Dooh, pole sana mkongwe..!

Umepiga gym miaka 8 tu umepata matatizo..!?

Mkongwe, mzee wangu anakaribia miaka 60 bado anapiga gym, ameanza kupiga gym hata kabla sijazaliwa, sijawahi kumsikia.

anasumbuliwa na bawasiri au kifua kuuma ikitokea ameacha kupiga kwa muda mfupi, isipokuwa gym imemfanya asizeeke haraka, akisimama na watu anaolingana nao umri yeye anaonekana ni kijana mdogo.

Chief, wewe ulikuwa unapiga gym bila kufuata utaratibu mzuri..!
 
Sijakuambia kupiga chuma kunakufanya ufaulu mtihani aisee..!
Kama huyo jamaa alikuwa hana utaratibu wa kutenga muda wa kujisomea ulitegemea atafaulu kwa kupiga nondo tu..?
Nilikumisquote Mkuu hebu rejea points zako.

waswahili wanasema "muwamba ngoma huvutia kwake"
 
Haya tupe na mfano wa Mzee asiyefanya mazoezi anavyoshambuliwa na magonjwa angazia sana kisukari nk
danganya tu wenzako wapenda sifa mjomba wangu alikuwa anajifanya mtemi na mivyuma yake, sasa hivi kapata ugonjwa wa kushake mikono mpka matako,vijana wengi wanajiona wajanja kunyanyua mivyuma but time will tell
 
Back
Top Bottom