Umuhimu wa Makanisa na misikiti uwe kando kabisa

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kama tumeamua kupambana na CCM na utawala wake basi tujipange kwa kutegemea vyama vya siasa tu.

Mambo haya ambayo naona ni mchezo unaopangwa na CCM na serikali yake ni kutumia vyombo hivi katika kuwapindisha wananchi wazalendo.CCM na serikali yake wanatoaa muelekezo kwa vyombo hivi kwa umakini kabisa pengine hata vyombo vyenyewe havielewi kuwa vinatumia kutokana na umahiri wa mashushu kuingiza hoja katika vyombo vya dini.

Vyama vya siasa na wazalendo wapenda siasa waache kabisa kutegemea hoja kutoka katika mashirika au vyombo vya kidini naa badala yake viendeleze mapambano ya ana kwa ana ,jicho kwa jicho au uso kwa uso kutoka ndani ya vyama vyao kuikabili CCM na Serikali yake.

Nasema tusitegemee kauli kutoka kwa Mashekhe au maaskofu hawa sio wanaogombea ubunge wala umeya wala uraisi ,wala sio wanaoanzisha hoja ndani ya bunge,hivyo maelekezo na makaripio yote yatoke ndani ya vyama vya siasa,ikiwa kwenye mikutano au kutoka kwenye vyombo vya habari.

Ni ukweli usiopingikaa kuwa kutegemea vyombo hivi kutavifanya vyama vya siasa kuwa dhaifu na visivyojiweza katikaa kuamsha hisia na hoja mbele ya wananchi na mwishowe hata wanachama wataviona vipo kama wasindikizaji.Ni lazima kwa hali yeyote ile vyama vya siasa vya upinzani viwe vya mwanzo na vyenye kauli kali dhidi ya CCM na serikali yake.
 
Kanisa heri linyamaze na kufunga mdomo maana kila nikikumbuka mauaji ya kimbari Rwanda huwa nasikitika sana Kanisa linapoongelea juu ya haki! kila nikikumbuka mauaji ya Mwembechai Dar, na kauli alieitoa Padri Lwambano kuwa Serikali iwashugulikie Waislamu wa Msikiti wa Mwembechai na siku ya pili Polisi waliitikia wito huo na kuuwa wananchi wenzetu! nasikitika tena Kanisa kuhubiri haki!

Kila nikikumbuka mauaji ya raia huko visiwani na kauli ya Muadhama Kardinali Pengo kuwa waliouliwa na Polisi huko Zenji ndio wabebe lawama kwa kutokutii amri ya Serikali ya kutokuandamana!!

Sasa, leo Kanisa na Baraza la Maaskofu watakuwa na ubavu gani wa kujitokeza na kulaani mauaji ya Arusha?

Kuna watu wengine wapumbavu watakao fikiri kuwa mimi nafurahia mauaji ya Arusha lakini kwa hakika kila binaadamu mwenye hisia hatafurahia kitendo hicho cha Askari wetu kufyatua risasi za moto na kuua wananchi! ni tendo la kulaaniwa lakini sio Maaskofu wajitokeze leo ghafla na kutoa kilio cha kinafiki! kwanza waombe msamaha kwa maovu waliofanya huko nyuma kwa kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Benjamin Mkapa ya kuuwa raia wa nchi hii na ndipo wafungue ukurasa mpya wa kudai haki za wananchi kinyume chake itakuwa vigumu kuelewa lengo la Kanisa ni nini!
 
Back
Top Bottom