Umuhimu wa maji mwilini

D

Dk BS

New Member
Joined
Jul 9, 2019
Messages
4
Points
45
D

Dk BS

New Member
Joined Jul 9, 2019
4 45
ATHARI ZA KUTOKUNYWA MAJI YA KUTOSHA :

Watu wengi wanadharau maji ya kunywa. Wanaona kula ndio muhimu kuliko kunywa maji. Wanaona vinywaji vingine ndio bora kuliko kunywa maji. Hawajui ni hasara kubwa kiasi gani wanajisababishia katika miili yao na afya na urembo wao au uzuri wao kiujumla. Ni wengi ambao hawathamini maji ya kunywa kabisa.

ATHARI KUBWA ZA KUTOKUNYWA MAJI :

1. Hufanya ngozi kua kavu na kuleta makunyanzi mwili mzima.

2. Huua nuru ya macho.. kusababisha matongotongo mengi machoni na kuleta wekundu machoni na pia kuleta utandu machoni kusababisha kutokuona vizuri mpaka ufikiche jicho ndio uone.

3. Husababisha machunusi usoni na mwilini. ( body acne) mgongoni,mapajani,mabegani,matakoni na hata shingoni. Kama huna maji mwilini uchafu (toxic inabakia katika figo na kuleta joto katika mwili ambalo huleta machunusi ya mwilini.

4. Husababisha kuua figo. Figo zinahitaji maji ili kutoa uchafu unaojikusanya ndani yake. Uchafu unaobakia huleta madhara makubwa kiafya.

5. Husababisha mdomo kutoa harufu mbaya. ( mouth odour )

6. Husababisha nywele kunyofoka. Ngozi ya kichwa hua kavu na kufanya mzizi wa nywele kukosa nguvu na nywele kutoka nzima nzima na pia kukatikakatika.

7. Husababisha kupunguza damu na kuharibu mzunguko mzima wa hedhi kwa mwanamke na pia hata unapopata siku zako uchafu hautoki vizuri na badala yake kukata hata siku hedhi.

8. Husababisha mkojo kua wa njano sana na pia kua na harufu kali sana.

9. Husababisha magonjwa mengi ya ngozi na pia husababisha kupatwa kwa allergy bila ya kutegemea na allergy hiyo kujirudia mara kwa mara.

10. Husababisha kutokupata haja kubwa na hata kama ukipata haja kubwa hua ( kigumu sana na pia husababisha mchubuko katika njia ya haja kubwa na na hatimae kupata ugonjwa wa bawasiri ).

11. Husababisha kukosa usingizi na kuleta weusi machoni na pia kuumwa kichwa mara kwa mara.

12. Husababisha kua na harufu mbaya na kali sana ya jasho.

13. Husababisha mwili kuchoka na kujisikia kukosa nguvu na pia hamu ya kula.

14. Husababisha kushusha presha na sukari mwilini. Mwili huuma kama mtu aliepigwa na fimbo.

15. Husababisha dawa yeyote ya kupaka katika ngozi iwe cream au lotion au dawa ya tiba yeyote kutokufanya kazi. Kwasababu tayari wakati huo ngozi inakua dhaifu na kukosa virutubisho.

16. Husababisha kupata UTI na matatizo mengi katika kibofu na mwishowe kuathiri kizazi.

17. Husababisha kuongezeka kwa uzito wa mwili. ( kilograms )

18. Husababisha kuumwa sana kwa miguu na nyayo. Haswa sehemu za kisigino na pia mishipa kuvutana na kuuma sana wakati wa kulala au kukaa.

Madhara ni mengi.. haya nimeyataja hapa ni baadhi tu. Maji ni kitu muhimu sana katika mwili wa binaadamu. Wengine hata akinywa maji glass 1,2 au 3 kwa siku anajiona kanywa maji mengi. Hapana ni kosa kubwa hilo. Unatakiwa unywe kulingana na uzito wako mfano litre 2=50kg, 3=65kg, 4=80kg na nk, kwa siku. Lakini lazima kunywa maji kila siku. Kukaa bila ya kunywa maji ni hatari sana kwa afya yako.
Epukana na mengi kwa kunywa maji ya kutosha.

Sio lazima uanze moja kwa moja kunywa litre 1 au 2 au 3 kwa siku. Anza kwa kunywa maji kiasi na pole pole kuongeza idadi kila siku
 
M

Mtumishi wa Bwana89

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Messages
1,201
Points
2,000
M

Mtumishi wa Bwana89

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2018
1,201 2,000
Asante ndugu,pia yanasaidia kuyeyusha lehamu (cholesterol) mwilini
 
M

Mtumishi wa Bwana89

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Messages
1,201
Points
2,000
M

Mtumishi wa Bwana89

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2018
1,201 2,000
Kunywa maji kwa faida yako mwenyewe
 

Forum statistics

Threads 1,313,896
Members 504,678
Posts 31,807,460
Top