Umuhimu wa Maamuzi ya leo kwenye kesi ya Mbowe na wenzake

Mbowe anatuhumiwa kwa ugaidi lakini mashahidi wote walioletwa hawana concrete ushahidi wa ugaidi aliofanya zaidi ya kubumba bumba tu na kubebwa na JAJI.
 
Hivi wanavyomtesa binadamu mwenzao aliyeumbwa kama wao na ambae hana kosa wanajua huu ukatili na laana hii watailipa wao na watoto wao?
 
😁😁😁
W.jpg
 
Msingi wa Ling’wenya na wakili wake kuandika barua kwa RPC Ilala kuomba nyaraka za uthibitisho dhidi ya shahidhi wa pili wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ndogo ni kwamba shahidi huyo hakuwa Central Dar es Salaam, mwaka 2020.

Hivyo kama mahakama itatupilia mbali pingamizi la Serikali, na ikaipokea barua yake hiyo basi upande wa mashtaka utakuwa mtegoni.

Maana hatua itakayofuata Ling’wenya ataiomba mahakama hiyo imuamuru RPC Ilala kumpatia au kuwasilisha mahakamani hapo nyaraka hizo alizoziomba ili kujiridhisha kama kweli mwaka 2020 DC Msemwa alikuwa akifanya kazi Central.

Lakini kama nyaraka hizo zisipopatikana au kuletwa na zisiwe na uthibitisho huo, ni dhahiri ushahidi wa shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka hautakuwa na miguu ya kusimamia.
Na kweli kama mahakama ina nia ya kutaka kujua ni kitu gani kipo au hakipo, hata mimi nilidhani ingekubali barua iwe kielelezo ili kujiridhisha ni jambo gani lilitokea siku hiyo. Otherwise, naona kama imejikita kwenye 'technicalities' kwa kuunga mkona pingamizi la upande wa Jamhuri.
 
Msingi wa Ling’wenya na wakili wake kuandika barua kwa RPC Ilala kuomba nyaraka za uthibitisho dhidi ya shahidhi wa pili wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ndogo ni kwamba shahidi huyo hakuwa Central Dar es Salaam, mwaka 2020.

Hivyo kama mahakama itatupilia mbali pingamizi la Serikali, na ikaipokea barua yake hiyo basi upande wa mashtaka utakuwa mtegoni.

Maana hatua itakayofuata Ling’wenya ataiomba mahakama hiyo imuamuru RPC Ilala kumpatia au kuwasilisha mahakamani hapo nyaraka hizo alizoziomba ili kujiridhisha kama kweli mwaka 2020 DC Msemwa alikuwa akifanya kazi Central.

Lakini kama nyaraka hizo zisipopatikana au kuletwa na zisiwe na uthibitisho huo, ni dhahiri ushahidi wa shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka hautakuwa na miguu ya kusimamia.
Wapiga kelele tayari wamebwagwa mkuu.
 
Msingi wa Ling’wenya na wakili wake kuandika barua kwa RPC Ilala kuomba nyaraka za uthibitisho dhidi ya shahidhi wa pili wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo ndogo ni kwamba shahidi huyo hakuwa Central Dar es Salaam, mwaka 2020.

Hivyo kama mahakama itatupilia mbali pingamizi la Serikali, na ikaipokea barua yake hiyo basi upande wa mashtaka utakuwa mtegoni.

Maana hatua itakayofuata Ling’wenya ataiomba mahakama hiyo imuamuru RPC Ilala kumpatia au kuwasilisha mahakamani hapo nyaraka hizo alizoziomba ili kujiridhisha kama kweli mwaka 2020 DC Msemwa alikuwa akifanya kazi Central.

Lakini kama nyaraka hizo zisipopatikana au kuletwa na zisiwe na uthibitisho huo, ni dhahiri ushahidi wa shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka hautakuwa na miguu ya kusimamia.
Good thinking
 
Watu wanashabikia kesi kama Simba na Yanga hawasomi hoja!
Na hii inafanya mawakili wa utetezi kuendelea kutoa maboko ili washangiliwe!
 
Jaji ameingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Leo 29 November 2021

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze nipo na
Pius Hilla Abdallah
Chavula Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naomba Kuwatambulisha
Nashon Nkungu
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Seleman Matauka
Khadija Aron


Jaji: Washtakiwa namba 1,2,3 na 4? Washtakiwa wote wanaitika wapo mahakamani..


WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo na tupo tayari Kusikiliza

Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia kwa Ruhusa yako tupo tayari Kupokea Uamuzi Mdogo pamoja na Kuendelea Jaji: anaandika Kidogo Mahakama ipo kimya!


Jaji: Siku ya Ijumaa 26 Mahakama ilihairisha Shauri Kwa ajili ya Kusoma Maamuzi ya leo, Maamuzi ni marefu lakini nitasema Kwa Kifupi, Nita' skip Kusoma Hoja za pande zote mbili lakini naomba mjue nimezingatia.. Mtakumbuka Shahidi Namba Moja wa Utetezi wakati anatoa Ushahidi

Alieleza Mahakama Kwamba alitaka Kutoa Kielelezo, Na Upande wa Mashitaka ulipiga na Sababu za Kupinga ilikuwa ni Shahidi Competence yake, Hakuweza Kuelekea Mnyororo Wa Kielelezo na hakuweza Kuelekea Relevance ya Kielelezo Chenyewe

Kwa Upande wa Mashtaka Abdallah Chavula na Pius Hilla ndiyo walitoa Hoja kwa niaba na Mawakili Wote, Katika Kueleza Hoja Wali cite Prison General Order, Na Sheria Mbalimbali pamoja na Sheria kesi Kwamba Sababu hizo Waliomba Mahakama Ikatae, Mawakili wa washtakiwa namba Moja,Mbili na Namba Nne walieleza Kuunga Mkono Kupokelewa kwa Kielelezo, Mr. Dickson Matata Na Fredrick Kihwelo na wao wwalitoa Hoja zao. Na baada ya Kumaliza Upande wa Mashtaka Walipata nafasi tena ya Kujibu Hoja za Utetezi, Naomba nisirejee Hoja Hizo lakini nimezizingatia.

Jaji: Mwisho katika Kuhitimisha walisema Kwamba Hoja walizotoa Hazikujibiwa na Kwamba Upande wa Utetezi Walishindwa Kuzitengua. Hizo Ndiyo Hoja za pande zote Mbili.
Eneo la Kwanza Lilikuwa Competence, Pili ilikuwa Mnyororo Wa Kutunza Kielelezo, Tatu ilikuwa ni Relevance ya Kielelezo na Mwisho Upande wa Utetezi na Shahidi Kushindwa Kutengeneza Misingi

Jaji: Katika Eneo hilo Mahakama Ya Juu Ilishatoa Maelekezo Nyingi. Na Kwamba Katika Kupokea Kielelezo Mambo Matatu yanapaswa Kuzingatiwa, Ambapo ni Material, Relevance, Competence na Shahidi Kuelewa Kielelezo hicho.

Jaji: Kesi za SHARIF ATHUMAN Vs DPP na CHARLES ABEL GEZILAHABO nimezipitia, Kesi Ya CHARLES GAZILABO wameeleza Kwamba Kuna Kanuni ya Kupima Kielelezo ambayo ni Authentication. Kwamba Katika Shahidi Kupima Kielelezo Chake anapaswa kupimwa kama Kielelezo kina Features ambazo ni Unique

Jaji: Kama ambavyo Nimeeleza Kwenye Sheria Kesi hizo, Kwamba DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN Imeelezwa Kwamba Kielelezo Kiwe Kipo vilevile tangu Siku ya Kwanza, Maeneo haya Mawili ni Wazi yatajwe Wakati anaitambua Kielelezo na Wakati anakitambulisha, Na anapokuwa anatoa

Jaji: Kielelezo Lazima akionyeshe, Shahidi ambaye yupo Mahakamani aliweza Kuvitambua Vitu kadhaa Vitu hivyo ni Majina, Mihuri ya Mahakama Kuu Divisheni, Majina na Sahihi, Na Kwamba Kwa Upande Wa Utetezi wanasema Kwamb aliweza Kutambua Kielelezo, Kwa Upande wa Mashtaka Wanasema Kwamba Hawaamini Kwamba alitaja Vitu husika, Kwamba Kwa sababu Hiyo Basi Wanaomba Iamriwe Kwamba Shahidi ameshindwa Ku authenticate Kielelezo, Mahakama Ikaombwa Irejee katika Maamuzi yake Kwamba Kushindwa Kutaja Kumbukumbu namba

Siyo Kigezo Pekee. Na. Mimi nakubaliana na Kwamba Kumbukumbu Namba siyo Unique Feature pekeee. Kama ambavyo Kielelezo Kimelezwa Kwamba Barua ina sahihi ya wakili. Ni sahihi Kwamba Saini ya Wakili inaweza Kuandikwa Kwa Barua Nyingine, Jina linaweza Kuwa katika Barua Nyingine

lakini Mahakama inaona Ni Vigumu Kukuta Barua Ina Vitu Vyote Vitatu. Kwa Maana hiyo basi Mahakama Inaona kwamba Shahidi ameweza Ku authenticate Kielelezo....

Jaji: Sasa Mahakama inahamia kwenye Mnyororo Wa Kielelezo, Katika Eneo hili Mahakama imeelezwa Kwamba Chain of Custody Imeshindikana Kuthibitishwa Na Kwamba Upande Wa Mashtaka umeeleza Kwamba ili Uweze Kutoa Nyaraka ya Mshtakiwa lazima Kwamba Barua hiyo iwe Imehusishwa na Prison Officer Kwa Kuzingatia order 685 ya Prison General Order..

Na Kwamba Kwa Sababu Afisa wa Magereza hajahusishwa basi Kielelezo kimeshindwa kuonyesha Chain of Custody. Kwa Upande wa Utetezi walisema Kwamba Shahidi aliweza Kuonyeshwa Barua hiyo Wakati wanamuandaa Shahidi huyo

Pia wakili wa Utetezi alisema Kwamba Kwa Mujibu wa Katiba, Wakili anayo Haki ya Kuwasiliana na Kumuonyesha Shahidi Barua, Pia Kwamba Barua hiyo haijawahi Kuingia Magereza, Shahidi alionyeshwa Barua hiyo Mahakamani

Hivyo basi Pande zote Mbili wanakubaliana Kwamba Mtu yoyote ambaye yupo Chini ya Magereza hawezi Kufikishiwa Nyaraka Bila Kupitia Kwa Afisa wa Magereza, Kwa namna hiyo basi Wakili anapaswa awasiliane na Afisa Wa Magereza


Isipokuwa tu shahidi anapokuwa Kwenye Kizimba, Akiwa Mahakamami Wakili anaruhusiwa, Kwa Maana hiyo basi ili wakili apate Ruhusa ya Kuwasiliana na Shahidi, Na Kwa namna hiyo ni wazi Kwamba wakili lazima akutane na Shahidi Wake wakati wa Kumuandaa kabla ya Kutoa Ushahidi Wake

Lakini kwa Bahati Mbaya Sana Maelezo haya yametolewa na Wakili na Siyo Shahidi,, Shahidi Hakusema ni wakati gani alipata nafasi ya Kuonana na Wakili

Jaji: Shahidi amekuwa Mchumi sana Wa Meneno ameshindwa Kueleza Mahakama Alikutana na Kielelezo Wakati gani na Kuonyesha Kwamba ana Uelewa na Kielelezo..

Na hii imerejewa Katika Sheria Kesi ya CHARLES GAZILABO I'm eleza Kwamba Jambo Kubwa la Kufanya Shahidi Aweze Kutoa Kielelezo Mahakamani lazima aoyeshe Kwanza akielezwa Kielelezo hicho anachotaka Kutoa Mahakamami

Pia imeelezwa katika kesi ya KHAMIS ADAM Vs JAMHURI, Katika Hali hiyo nakubalina na Upande wa Jamhuri Kwamba Shahidi alipaswa aonyeshe Kwamba ana ufahamu. Katika Sheria Kesi hiyo Tajwa hapo Juu na Kwamba Shahidi aonyeshe kuwa alielezwa Kielelezo hicho

Shahidi Kuona Pekee Ushahidi haitoshi Kuonyesha Kwamba alikuwa na Umiliki wa Kielelezo hichi. Hajaieleza Mahakama Kwamba aliifanyia nini. Katika Mazingira haya basi Mahakama Inashindwa Kuaminika Kwamba Alikiona Kielelezo hicho.

Ni kweli Kwamba Shahidi aliwaelekeza Barua Kuandikwa Kwa Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, na Nakala kwa Shahidi na Naibu Msajili. Upande wa Mashtaka unasema Kwamba Pamoja na Shahidi Kupewa Nakala ya Barua hiyo inashangaza Kwamba Barua anayotaka Kutoa siyo Nakala yake

Jaji: Wanajiuliza Je Barua hii ni Ile ambayo Shahidi alitaka Naibu Msajili Apokee au alitakiwa Apewe? Ni kweli Nyaraka iliyoombwa Kutolewa Hapa Mahakamani, Ni Barua iliyokuwa inatakiwa kwenda Kwa Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi

Kwenye Barua hiyo Shahidi alisema anataka Stationery Diary, Lakini Mahakama Inaona kwamba siyo Kila Mtu anaweza Kuwa Conversant, Kwa Maana hiyo basi Mahakama Ilisha Sema Kwamba Pale Mtu anapokuwa ametajwa kwenye Nakala, Basi Mahakama inachukulia Kwamba Shahidi ana Nakala hiyo

Huo Ndiyo Msimamo wa Mahakama, Lakini pia Kuna Vigezo Vya Kufikia hapo Kwamba Lazima Barua hiyo Ionyeshe Kwamba amepewa Nakala hiyo, Shahidi Kabla hajaonyeshwa Barua alisema Kwamba Barua ina Muhuri Wa Naibu Msajili, Ni Wazi Kwamba Barua hiyo siyo Nakala yake Bali ya Naibu Msajili

Kwa Maana hiyo haijasemwa Kwamba ni nani Aliyempelekea Naibu Msajili Barua, Ni wazi Kwa Namna Barua hii Ilivyo siyo Nakala yake Yeye, hayo yangeweza Kuthibitika Kwamba ni Barua Yake ambayo alim' serve Naibu Msajili, Kama Nilivyoeleza Kwamba Shahidi Alikuwa Mchumi wa Maneno

Mahakama inajiuliza Je Nakala hii Ndiyo aliyopelekewa RPC Ilala, Kwa namna hiyo Shahidi ameshindwa Kuonyesha Chain of Custody, Kwa sababu ya Kushindwa Kueleza Kwamba Ilikuwaje Kwamba Kielelezo alishindwa Kukitoa na akatoa Barua Iliyogongwa na Naibu Msajili..

Jaji: KWA SABABU HIYO BASI MAHAKAMA INAKATAZA KUPOKEA KIELELEZO HICHO, NATOA AMRI.
Msengerema huyu
 
Mawakili wa Serikali wamejipanga sana katika kesi hii. Hata kama ni kesi ya kupikwa ila tambua kwamba wamejipanga vilivyo na wanapambana sana.
 
Back
Top Bottom