Haya ni maoni yangu binafsi.
Kwanza nianze kusema inaelekea baada ya robo karne ya vyama vingi, sasa kuna mwelekeo mpya duniani.
Haiwezekani mfumo wa vyama vingi hadi Leo Afrika ndio sababu ya mauaji na chuki na kwamba walioleta vyama vingi wameshindwa kuweka nguzo imara ili kila taifa likalazimika kufuata.
Lazima kuna ombwe na hilo ombwe ndio limeleta balaa.
Nirudi kwenye mada.
Maalim hakuna ubishi kwamba ni gwiji wa siasa na mweledi, anayekubalika na asiyeyumba.
Huyu mzee kamuanika kila mnafiki wakiwemo CCM, mabeberu na vitimbakwiri wa CCM wakiwemo masheikh, maaskofu na taasisi mbali mbali.
Licha ya kuporwa ushindi Mara kadhaa alikubali maridhiano zaidi ya Mara 3 hadi kufikia kuyaingiza kwenye katiba ya Zanzibar. Hapa inaonekana CCM ndio imeifanya iwe peak ya kisiasa ya vyama vingi Zanzibar.
Baada ya CCM kuona kuwa wamekataliwa Zanzibar walikubali hadaa hii ambayo iliwagharimu vile vile.
Mwaka 2015 ulikwa ndio wa majaribio ya ghilba na kilichotokea ndio kimewalazimisha Leo kuchukuwa mwelekeo wa kufuta vyama vingi.
Ama kwa kuzidiwa au kwa mission za tokea awali sasa CCM imelazimika kufuta upinzani uliouumba kwa robo karne.
Kwa upande wa Maalim Seif kama asemavyo mwenyewe yeye na Zanzibar na wazanzibari. Mara zote amekuwa akitanguliza maslahi ya umma ndio akalazimika kukubali hadi maridhiano limradi jamii iwe pamoja.
CCM wameshindwa Mara nyingi na wameonesha unafiki wao kuhusu demokrasia ya vyama vingi bara na Zanzibar.
Yaliyotokea 2015 ilikuwa ni zamu ya kuwaaibisha wazungu na demokrasia yao. Huyu nguli amewafundisha wazungu maana ya political science na ile digrii yake ya houner pale UDSM.
Wazungu kimya na mfumo wao wamekubali demokrasia kuchezewa na kunajisiwa.
Uchafuzi wa 2020 umezidi kuwavua nguo na sioni dalili za kupatiwa suluhu.
Kama hivyo ndivyo basi nashauri Maalim Seif aufikirie upya msimamo wa kushiriki offer ( ya kinafiki) ya Dr Hussein Mwinyi kwa sababu zifuatazo.
1. Kwa kuwa 2015 hakuna kilichotokea kuhusu kuwajibishwa waliovuruga basi atumie fursa finyu iliyopo aridhie na kukubaliana baadhi ya mambo ili viongozi wenziwe wapate japo huruma ya teuzi chache kwenye nafasi 10 za Rais, wengine kwenye sifa za kuajiriwa waajiriwe serikalini ambayo yeye ni sehemu yake kwa maslahi ya Wazanzibari wote ilimradi dunia imeshindwa kusimamia haki.
2. Kukilea chama chake na upinzani kwa ujumla ikiwa tu dunia itashindwa kuja na suluhisho LA kurejewa uchaguzi.
3. Awasilishe mapendekezo ya kufidiwa mauaji yaliyofanywa na CCM na kujumuishwa wapinzani kwenye nafasi muhimu serikalini ili kuponya madonda.
4. Kuwemo serikalini kutampa fursa ya kushauri na kuitetea Zanzibar pale inapotaka kuangamizwa ingawa tayari amekatwa mikono na miguu kwa kunyimwa wabunge na wawakilishi kwenye ngome zake.
5. Atapata fursa za kujua kinachopangwa na kupata kujipanga mbadala kwenye kipindi hiki cha dhoruba ya udikteta uchwara hadi hapo hali itakapotulia.
6. Nje ya uingiliaji wa kimataifa, CCM haina cha kupoteza Zanzibar. Walishatamukiwa na kususia na sasa wameshachukuwa kwa mizengwe majimbo yote ya ngome za Maalim Seif. Hii ni kuwa wataendelea na mipango yao na ni jamii ya Zanzibar ndio itaumia na kutengwa, kunyanyaswa na kunyimwa fursa za ajira na ushirikishwaji. Kwa kuangalia mbele in bora tu kushiriki walau kupunguza makali ya hujuma.
7. CCM wanamuhitaji Maalim Seif kwa kiasi lakini inaonekana wamejipanga hata akikataa ndio maana wamechukuwa majimbo kwa ghilba kubwa ili wafanikishe azma yao. Bora aingie na japo watu wachache akaimarishe network nje na ndani kuliko kukosa yote ilimradi tu dunia imeitupa mkono demokrasia ya vyama vingi.
8. Kwa kuwa inaonesha dola imechukuwa mwelekeo huo, pengine ndio msimamo wa deep state zote, pengine mda wa vyama vingi umefika mwisho Afrika bora waingie na kujenga hoja ndani kuliko kutengwa nje na kutosikilizwa na mataifa na ndani.
9. Kuna kila dalili vyama kufutwa na kunyanganywa jukwaa LA kusemea. Hii inavihusu vyama vyote makini na huu in mtego. Ngamueni mtego na mkubali kwa lengo LA kuhami hata kama ni kubahatisha. Tangulizeni wengine ndani wengine wabaki nje. Maalim kuwa ndani hasa Zanzibar na wazanzibari ni muhimu sasa kuliko kuwa nje.
Masharti ya mtazamo huu in iwapo hakuna msimamo wa kurudiwa uchaguzi kutoka jumuiya ya kimataifa
Kwa sasa ni hayo tu
Kishada