Umuhimu wa kuwapima watoto zetu macho na masikio

Faridi

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
672
274
Umuhimu saana kuwapima watoto wetu toka pale wanapozaliwa kuwa hawana hitilafu ya kuona au kusikia, nimesikitika kuona jamaa mmoja ndiyo kwanza amegundua mtoto wake wa miaka minane haoni jicho moja na mtoto hakuwa akijielewa ana hitilafu hiyo, baada kumpeleka hospitali ikaonekana inawezekana alikuwa ana hitilafu hiyo toka alipozaliwa au alipokua mtoto mchanga.
Kuna familia nyengine pia walikuwa wakiishi na mtoto wao bila kuelewa hasikii sikio moja, na kumfikiria ni mtoto jeuri akiitwa haitikii, na baadae kugundua mtoto hasikii sikio moja.
Nimeona niandike visa hivi viwili ili tujenge tabia ya kuwacheki watoto wetu wadogo macho na masikio.
 
Ni kweli kabisa mimi ilinichukua kama miaka miwili kutambua kuwa mtoto wangu anatumia mkono wa kushoto kuandika, kabla ya hapo alipata bakora sana, sasa najilaumi
 
Back
Top Bottom