Umuhimu wa kuwafundisha vijana mahusiano yasiyo na hizi ngono zembe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Swala la ngono hovyo katika jamii limefikia hali mbaya. Boss kulala na wafanyakazi wa chini yake, akiyewekeza kidogo hata kwa mradi wa chai anataka kulala na wauza chai wake. Huko serikalini ndiyo usiseme. Mbali na utandawazi ambao umechangia sana ngono zembe ni hali mbaya ya uchumi.

Msichana anakua tayari kushiriki ngono zembe kwa iPhone 11 Pro Max. Kuna umuhimu wa kuwaelimisha vijana juu ya material things towards their humanity.

Hili swala lipotiliwa mkazo tutazaa dysfunctional society ambapo mtoto kubeba mimba akiwa na miaka 14 ni sawa na mjomba kuzaa na mtoto wake ni sawa.

Ni muhimu kuwafundisha vijana kuwa mahisiano kati ya mwanamke na mwanaume yanaeezekana pasi kuhusisha ngono. Shule zilizojengwa hapo awali zilikuwa ni za jinsia moja mfano Moshi Boys, Machame Girls, Tanga Schoo ilikua ni kwa wavulana na wasichana wakwenda Tabora Girls mbali na hapo kulikua na Tabora Boys. Hii ni mifano tu. lakini wahenga waliona umuhimu wa kuchanganya wavulana na wasichana baadae tulikua na shule za mchanganyiko.

Uhisiano wa kiko a kiume mbali na ngono unassidia utendaji kazi na ufanisi maofisini.
 
Uliyoongea ni ya kweli kabisa....nadhani kuna shida kubwa sana kwenye jamii zetu za Kiafrika hasa Tanzania.

Binafsi nadhani tatizo kubwa lipo kwenye malezi yaani kuanzia ngazi ya familia na kisha huko mashuleni. Vijana hawafundishwi lolote kuhusu positive relationship and negative relationship btn a teen male and female.

Badala ya kutumia elimu, Bado tumeendeleza Utamaduni wa kizamani wa kutumia vitisho na mikwara isiyomjenga vema kijana wa kike au wa kiume...matokeo yake ndo haya tunayoona.

Kweli kuna shida kubwa tena kubwa sana.

Thank you for lighting this problem dear!
 
Jamii yetu ya kitanzania ime normalize ngono imeonekana ni kitu cha kawaida.
Shida inaanzia hapo

Na jamii yetu inachukulia powa.. imeshaona ngono ni sehemu ya tamaduni. Ndio maana familia na ndoa nyingi hazina stability sababu ya hii mentality.

Hii kitu lazima iondolewe kwakweli
 
Somo la HISIA ni somo kubwa sana .. hapa tunachotakiwa kutoa somo la kuchekewa kushika ujauzito na kama kitu hakiwezekani hivi ila HISIA somo pana sana ; na kama utafaulu hilo somo halihusiki na kupata ujauzito kwa wakati sahihi
 
Daahhh vijana siku hizi wanapelekeana moto hatari, halafu hawachagui hata kitundu gani cha kupelekea moto, juzi kati nmesikitika sana kibinti kidogo tu kinapelekwa gheto na wavulana wawili.
Vijana wa siku hizi wakishaangalia zile sinema zao za kusisimua viungo vya mwili basi na wao wanataka wapraktiz vilevile kama walivyoona kwenye runinga.
 
Swala la ngono hovyo katika jamii limefikia hali mbaya. Boss kulala na wafanyakazi wa chini yake, akiyewekeza kidogo hata kwa mradi wa chai anataka kulala na wauza chai wake. Huko serikalini ndiyo usiseme. Mbali na utandawazi ambao umechangia sana ngono zembe ni hali mbaya ya uchumi.

Msichana anakua tayari kushiriki ngono zembe kwa iPhone 11 Pro Max. Kuna umuhimu wa kuwaelimisha vijana juu ya material things towards their humanity.

Hili swala lipotiliwa mkazo tutazaa dysfunctional society ambapo mtoto kubeba mimba akiwa na miaka 14 ni sawa na mjomba kuzaa na mtoto wake ni sawa.

Ni muhimu kuwafundisha vijana kuwa mahisiano kati ya mwanamke na mwanaume yanaeezekana pasi kuhusisha ngono. Shule zilizojengwa hapo awali zilikuwa ni za jinsia moja mfano Moshi Boys, Machame Girls, Tanga Schoo ilikua ni kwa wavulana na wasichana wakwenda Tabora Girls mbali na hapo kulikua na Tabora Boys. Hii ni mifano tu. lakini wahenga waliona umuhimu wa kuchanganya wavulana na wasichana baadae tulikua na shule za mchanganyiko.

Uhisiano wa kiko a kiume mbali na ngono unassidia utendaji kazi na ufanisi maofisini.
Mkuu, umezungumza mada mbili kwa mkupuo saazingine bila ya wewe kujua!

"Ngono zembe" na "ngono holela" hesabia.

"Ngono zembe" inachukuliwa kama ni ngono hatarishi, "kavu kavu" bila kutumia kinga ama condom.

Mantiki yako hapo ni kufanya "ngono holela" bila kujali umetumia kinga ama kavu kavu(ngono zembe).

Muktadha wako kimantiki umejikita katika kujenga maadili katika jamii na si kufanya ngono salama, nadhani tungeongelea hivyo.

Unapotaja neno "ngono zembe" tayari unawasisimua vicheche waliolala, kuanza kufuatilia topic waone inakoishia na kilichomo kama kimo!

"Ngono zembe" ni mfumo wa kufanya mapenzi bila ya kinga unaopendwa sana na wazinzi na hutekelezwa kwa masharti ya gharama kubwa, ni biashara ya hisia na faida yake ni hisia pia ama faida hewa na madhara yake ni makubwa.

Cha kuwafundisha vijana na jamii yetu kwa ujumla ni kujikinga na kujiepusha na "ngono zembe" pamwe "ngono holela" visababishi vya mmomonyoko wa maadili na magonjwa.
 
Back
Top Bottom