Umuhimu wa kuwa na utulivu kipindi hiki

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,765
18,619
Wana JamiiForums habari?

Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake mwingi sana.

Wanabodi napenda tushirikishane kupitia andiko hili, wakati huu tupo katika kigumu Sana ambacho dunia na mataifa zake yapo kwenye "mfarakano mkuu" kwa sababu ya huu ugonjwa wa Covid-19. Watu mbalimbali wameingia katika hofu nzito ya wasiwasi wa kupoteza maisha yao.

Tanzania ikiwa moja ya mataifa duniani imo katika taharuki kubwa Sana hasa wananchi wake ambao tumekuwa na maoni mbalimbali, wengine wakidai fungiwe ndani, wengine wakiungana na rais wetu.

Ushauri wangu tufanye yafuatayo:
1. Tufuate ushauri wa wataalamu kuhusu namna ya kuepuka maambukizi ya Corona.

2. Tuache dhana ya kumlalamikia mtu au serikali juu ya huu ugonjwa. Katika nchi Ya Marekani rais wao aliwatangazia mapema Wamarekani kuwa hakutakuwa na vifo vya Corona, walifunga mipaka mapema, wakafanya lockdown, lakini Leo hii vilio vimeitawala Marekani sababu ya Corona. Je, sisi ni bora kuliko Marekani? Hapana.

3. Tumuombe Muumba wetu Mwenyezi Mungu atuvushe katika janga hili. Hii kuna baadhi wataanza debate whether Mungu yupo au la! Lakini ukweli unabaki kuwa Mungu ndiye Muumba wetu na vyote.

4. Tusiwe wepesi wa kutoa taarifa juu ya Covid-19 kiholela, tuepuke kusambaza taarifa za taharuki ambazo zinasababisha wengine kuzidisha hofu. Wizara ya afya, Waziri mkuu, au Rais wa JMT ndiyo wenye mamlaka hayo. Hii Ni sawa na Vita, vitani hapapaswi kuwa sehemu ya kulaumiana na kutoa taarifa kiholela.

Mwisho, kaa ndani kama huna shughuli ya kukutoa nje ya makazi yako, tujenge nchi yetu pamoja. Rais hawezi kuizuia Corona ila ni Mungu pekee, tusilaumiane Bali tushikamane pamoja kuliko kipindi chochote kile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom