Umuhimu wa kuwa na rafiki mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa kuwa na rafiki mwema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mahmood, Nov 7, 2009.

 1. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  UMUHIMU WA KUWA NA RAFIKI MWEMA

  Ningependa kuwahusia enyi ndugu zangu kuhusu umuhimu wa kuwa na marafiki wema, kwa vile ni kawaida kwa sisi binaadamu kuhitaji marafiki. Kuchagua rafiki mzuri ni lazima hii kwa ajili ya kuhifadhi dini yetu.

  Waislamu wakiwa na tabia nzuri na wenye kufuata njia ya Allah, basi uislamu utakuwa na nguvu, ni hivyo ndivyo inavyotakikana. Kufanya urafiki na watu wema wenye tabia nzuri, ni mojawapo ya njia ya kutufanya sisi kuwa kwenye njia iliyonyooka.

  Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema: "Mtu yamkinika kufuata dini ya rafiki yake, kwa hivyo muangalie unaemfanya kua rafiki yako.”


  Lazima tuchague marafiki ambao wako radhi na dini yetu na tuepukane na wale ambao hawako radhi na dini yetu. Na tukiona marafiki zetu matendo yao sio mazuri, ni lazima tuepukane nao kwasababu tunaweza tukaiga tabia zao ambazo zinakwenda kinyume na dini yetu.

  Kutengamana na marafiki ambao wanakwenda kinyume na njia ya Allah SWT, inaweza ikatubadilisha tabia, fikra na mwenendo wetu. Lakini vile vile inatupasa kuwatendea wema.

  Katika Hadith, Mtume Muhammad (s.a.w.) anasema: "Mfano wa rafiki mwema na rafiki mbaya ni kama mfano ule wa muuzaji wa misk (mafuta mazuri) na mhunzi (mfua vyuma). Basi ukiwa kwa muuzaji wa misk, imma atakunusisha mafuta mazuri, au utanunua kwake hayo mafuta au angalau utafurahia harufu nzuri itokayo dukani kwake. Na ukiwa kwa yule mhunzi, imma atakuchomea nguo au utapata harufu mbaya ya moshi kutoka kwake.”

  Katika tafsiri ya Hadith hii, Imam An-Nawawy alisema; Mtume (s.a.w.w.) alilinganisha rafiki mzuri na muuzaji misk (mafuta mazuri) kwa sababu, kua na rafiki mzuri mwenye tabia ya upole, na elimu, utapata faida kutoka kwake.

  Na Mtume SAW alitukataza kukaa na wale wenye kufanya maovu.

  Mwanachuoni mmoja asema: “Kuweka uhusiano mzuri na watu wema matokeo yake ni kupata elimu iliyo na faida, tabia nzuri, na matendo mema, ambapo kuweka uhusiano na waliopotoka, huyazuia hayo mema yote."

  Allah Anasema katika Qur'an:

  "Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningeli shika njia pamoja na Mtume!
  Ee Ole wangu! Laiti nisingelimfanya fulani kuwa rafiki
  Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shetani ni khaini kwa mwanaadamu." (Quran - Al Furqan ) aya 25:27-29

  Allah, tena anasema:

  "Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachaMungu." (Quran - Azzukhruf) aya 43:67

  Ibn Katheer ameeleza kuhusu aya hii, kisa ambacho kimepokewa na Ali ibn Abi Talib(a.s) kuwa, urafiki wowote ambao sio kwa ajili ya Mungu, hugeuzwa ukawa wa uadui ispokuwa chochote kilichokuwemo kwa ajili ya Mungu.
  Watu wawili ambao ni marafiki kwa ajili ya Mungu; mmoja wao akifariki, hupewa bishara nzuri kuwa amejaaliwa pepo, basi humkumbuka rafiki yake na kumuombea dua akisema: “ Ewe Mola wangu, rafiki yangu alikuwa akiniamrisha Kukutii na kumtii Mtume Wako Muhammad SAW, na alikuwa akiniamrisha kufanya mema na alikuwa akinikataza kufanya maovu. Na aliniambia kuwa nitakutana na Wewe. Ewe Mola wangu, basi usimuache kupotea baada ya mimi kuondoka, na muoneshe haya ulionionesha mimi, Na Uwe radhi nae kama Ulivyoridhika na mimi.” Basi ataambiwa: “Laiti ungelijua aliyoandaliwa rafiki yako, basi ungefurahi sana na ungelia kidogo.” Kisha rafiki yake akifariki, roho zao zinakusanywa, na wote wanaambiwa watoe maoni kuhusu killa mmoja. Basi killa mmoja anamwambia mwenzake: “Ulikuwa ndugu mzuri kabisa, mwenzangu mzuri kabisa, na rafiki mzuri kabisa.” Na mmoja wa wale marafiki wawili wasioamini anapokufa na kupewa bishara za moto wa Jahannam, humkumbuka rafiki yake na kusema: “ Ewe Mola wangu, rafiki yangu alikuwa akiniamrisha nikuasi na nimuasi Mtume Wako Muhammad SAW, na likuwa akiniamrisha kufanya maovu na kunikataza kufanya mema, na akaniambia sitokutana na wewe. Ewe Mola wangu, usimuongoze baada ya mimi kufa, na Muoneshe haya ulonionesha mimi, na Usiwe Radhi nae kama ambavyo Huko Radhi na mimi.”Halafu yule rafiki mwengine akifa na nyoyo zao zikikusanywa, wote wawili wana ambiwa watoe maoni kuhusu kila mmoja. Basi kila mmoja anamwambia mwenzake: “Ulikuwa ndugu mbaya kabisa, mwenzngu mbaya kabisa, na rafiki mbaya kabisa."

  Kwa hivyo ni katika urafiki mwema ndio Allah SWT Humuokoa aliyepotea na kumuongoza aliyekosea. Faida ya kufungamana na marafiki wema ni kubwa kupita kiasi na inshaallah itakuwa wazi zaidi kwetu siku ya kiama, kama tulivyoona kwenye aya na visa vilivyopita.

  Na katika hadith nyengine pia, Mtume SAW ametuamrisha kufungamana na waumini peke yao.

  Na pia kuwa mtu atakuwa na wale awapendao.

  Kwa hivyo tukiwapenda na kuandamana na waliopotoka, basi lazima tujiogopee mwisho wetu.

  Ali (a.s.) alisema: "Fungamana na watu wema wapole, utakuwa mmoja wao; na epukana na watu waovu usalimike na maovu yao."

  Muumini ni kioo cha ndugu yake, akiona makosa ya muimini mwenzake inampasa, amueleze kwa uzuri na kumsaidia kurekebisha kosa hilo.
  Ibn Hazm amesema: “Yeyote anaekukosoa, anajali urafiki wako. Na yeyote ambae anachukulia wepesi makosa yako, basi hajali urafiki wako."

  Kwa hivyo ikiwa tunafikiria kuhusu mwisho wetu, lazima tutambue kuwa,wale ambao wanatuepusha na Kumkumbuka Mungu na kumfuata Mtume SAW, wale ambao hawatukumbushi swala zetu na wala hawatupi mawaidha mazuri kuhusu dini yetu, basi wao kweli ni maadui sio marafiki zetu.

  Allah SWT Anasema katika.

  Na atakayefanya urafiki na Allah na Mtume Wake SAW, na walio amini, basi hakika kundi la Allah ndilo lenya kushinda." Quran - Al Maida aya 56

  Namuomba Mwenyezi Mungu Atujaaliye tuwe miongoni mwa waja Wake wema na atupe marafiki ambao watatuepusha na ghadhabu zake, na watakaotuelekeza kwenye njia ya Allah na radhi zake. Namuomba Allah Atujaaliye tuwe miongoni mwa waja Wake wema ambao watakutana kwa furaha na kusifiana kama kile kisa tulichokisikia. Na atujaaliye tuingie katika pepo Yake ya Firdaus kwa rehma zake. Ameen
   
 2. S

  Shamu JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuwa na marafiki wabaya kama hawa majahili waliopo JF, ni dhambi. Kwa sababu, wanautukana Uislamu. Kitu chengine ni kwamba hii JF, imeundwa kwa ajili ya kuwatukana viongozi wa Kiislamu, pamoja na dini ya Uislamu. Ustadhi unalionaje jambo hili? Jambo jengine, je inaruhusiwa kidini kuchangia ktk MAJAHILI JF blog? Thanks.
   
Loading...