Umuhimu wa kuwa na Katiba ya wananchi unazidi kujitokeza.

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,210
13,723
Ili nchi yetu ipate maendeleo ni lazima kuwe na muendelezo wa mipango kutoka Awamu moja kwenda kwenye Awamu nyingine. Iwapo kila Awamu mpya inapoanza kutawala itayatupilia mbali yale yaliyoanzwa na waliowatangulia basi kasi ya maendeleo itapungua!! Haya yamejitokeza sana katika utawala wa nchi yetu kwani kila Rais anapoingia madarakani anataka kuonesha kuwa yule aliyemtangulia hakufanya vizuri hivyo pale paliporekebishwa na huyo mnae atataka kurekebisha na mara nyingine kurudisha yale ambayo mtangulizi wake aliyaona hayafai naye anaona yanafaa!! Tumeona hayo kwenye uwekezaji wa Nishati enzi ya Kikwete kuwa na msisitizo kwenye gesi lakini alipoingia Magufuli msisitizo ukahamia kwenye uzalishaji wa nishati kwa kutumia maji!! Lack of continuity in policy implementation imeigharimu nchini yetu fedha nyingi sana ambazo hazikuwa na ulazima nchi kuingia.

Kwenye upande wa rasilimali watu ni hivyo hivyo, na hili nitalieleza kwa mfano hai uliotokea hivi karibuni katika teuzi alizofanya Rais Samia. Tarehe 25/6/2019 ofisi ya mkurugenzi wa ma wasiliano ikulu ilitangaza kuwa Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Dkt. Baghayo Abdallah Saqware kama Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania[TIRA] na juzi tena huyo huyo Saqware ambae Rais Magufuli alitengua uteuzi wake kwa barua kutoka ikulu hiyo hiyo ya tarehe 4/1/2022 inamteua tena kushika wadhifa ule ule ambao alionekana hafai!!! Je maamuzi ya namna hit yanaleta picha gani kwa wananchi na mustakabali wa nchi kwa ujumla?

Haya yote, inaonesha udhaifu mkubwa katika mienendo ya taasisi zetu. Ni udhaifu wa namna hii ndio unatakiwa kuondolewa kwa kuwa na taasisi madhubuti ambazo zitakuwa na uhalali wa katiba ya wananchi.
 
Back
Top Bottom