Umuhimu wa Kutoa elimu kwa lugha ya kwanza (Kiswahili)

Mbona somo la Kiswahili kwenye continuous assessments na matokeo ya mwisho wanafunzi na wahitimu wote hawapati A wakati wanazungumza Kiswahili halafu kati yao wanafaulu vizuri Kiingereza kama somo.
Ni kwa sababu tuna kipuuza.. Tunakiona hakina maana kisa tunakiongea... Hatujui kama kinaweza kutuvusha sehemu moja kwenda nyingine.

Hatujawahi kuamini kama kuna kitu cha kwetu hata kimoja kinaweza kutuletea maendeleo...!
 
KUTOA ELIMU KWA LUGHA YA KWANZA AU LUGHA INAYOELEWEKA KUNAMPA MTOTO FURSA YA KUUNGANISHA ELIMU NA MAISHA YA KAWAIDA. KIINGEREZA KWA TANZANIA NI UKUTA UNAOZUIA MUUNGANISHO HUO.

PIA, KUNAMPA MZAZI FURSA YA KUCHANGIA KATIKA UELIMISHAJI. HADITHI ZA KITOTO HUWAELIMISHA MTOTO TOKA WANAPOKUWA WADOGO. HADITHI HIZO ZIMEBEBA ELIMU YAKIWEMO MAMBO YANAYOHUSU SAYANSI, HISTORIA NA BURUDANI. VITU HIVI HUPASWA KUENDELEZWA MASHULENI ILI KULETA UUNGANISHO WA KILE MTOTO ALICHOPATA KATIKA HADITHI NA ELIMU YA SHULE YA MSINGI, SEKONDARI HADI CHUO KIKUU.

WAZAZI WENGI WANAZUNGUMZA KISWAHILI. ELIMU INATOLEWA KIINGEREZA, HUONI KAMA UNAMNYIMA MZAZI HAKI NA JUKUMU LA KUFUATILIA ELIMU YA MWANAYE? MATOKEO YAKE NI KWAMBA JUKUMU LA ELIMU LIMEACHWA KWA WALIMU PEKE YAKE. NA WAZAZI WANAFIKIRI WAJIBU WAO NI KUWA NA PESA NYINGI YA KUMPELEKA MTOTO KATIKA SHULE BINAFSI ILI AKAPATE ELIMU BORA AMBAYO INAAMIKA ELIMU BORA NI ILE INAYOTOLEWA KWA KIINGEREREZA.

KUNA UMUHIMU WA WATU KUELIMISHWA NINI MAANA YA ELIMU NA TOFAUTI ILIYOPO BAINA YA ELIMU BORA NA LUGHA YA KIINGEREZA. ELIMU BORA INAWEZA KUWA KWA LUGHA YOYOTE.

KUNA UWEZEKANO WA KUJIFUNZA KIINGEREZA BILA KUFANYA LUGHA YA KUTOLEA ELIMU.

KUNA UWEZEKANO WA KUONGEA KISWAHILI BILA KUCHANGANYA NA KIINGEREZA. KUCHANGANYA SI UJANJA, NI UPUNGUFU WA USTADI KATIKA LUGHA. MTU STADI KATIKA LUGHA NI YULE ANAYEWEZA KUZUNGUMZA LUGHA MOJA KWA UFASAHA WAKE.

Mbona unaandika kwa maherufi makubwa? Katika protokali za mtandaoni, kuandika kwa herufi kubwa ni kupayuka. Sasa sijui kama unapayuka ama la! Hata sijamalizia kusoma yote....
 
Usiifananishe German na nchi za kishenzi....
Sijui unamaanisha nini kwa "kishenzi". Maendeleo makubwa katika nchi za Ulaya ni historia ya kuhamia lugha za kitaifa kama lugha ya shule na vyuo. Karne ya 19 mwanzoni nchi nyingi za Ulaya zilitumia lugha za kigeni kama Kilatini au baadaye pia Kifaransa (wakati ule lugha ya maendeleo) kwenye shule zao. Ziliweza kupata wataalamu lakini zilishindwa kuwaelimisha vijana wote. Tofauti kati ya wasomi na watu wa kawaida ilibaki kubwa.

Baadaye nchi zote zilihamia lugha za kitaifa, hata mataifa madogo kama Denmark, Czech. Basi sasa idadi ya wasomi ililipuka na matokeo ya elimu yaliboreka, watoto wote walijifunza na vipaji (talents) vilivyokuwepo katika kila taifa viliweza kutumiwa. Hii msingi wa maendeleo ya kiuchumi an kijamii.

Hapo balaa ya nchi zilizokwama katika historia ya ukoloni. Nakubali si kila nchi itakayoweza kuhamia lugha ya kienyeji kwa sababu Uhindi au Ghana hakuna lugha 1 inayoeleweka kirahisi kwa wote kutokana na uwingi wa lugha na tofauti kubwa kati ya hizi. Lakini Tanzania karibu wasemaji wote wanatumia lugha za familia ya Kibantu na hapo kuna nafasi nzuri - ambayo haitumiwi ipasavyo.
 
Kwani kabla ya kuanza kusoma hayo maneno ya sayansi... Uliwahi kuyaona wapi...!? Na unataka kusema hayaku kusumbua kipindi unaanza kujifunza...!?

Hio sio sababu... Haina mashiko kabisa. Maneno yapo changamoto ipo kwa watumiaji na utayari wetu wa kutambua kua Kiswahili ni kipana na kinakidhi mahitaji ya kila idara.
Hii ni kwa mfano wamasai wawe na mitaala ya kimasai na vyuo vyao ni kimasai tupu baada ya chuo itakuwa ngumu kupata ajira nje ya umasaini watakuwa wamejitenga na watanzania wengine ndo kama tanzania itajitenga na dunia kupitia kiswahili chako utapata wapi iyo ajira.
 
Haya ndiyo màajabu ya Watanzania, wote wanaopiga chapuo kiswahili kiwe ndiyo lugha mama kwenye nyanja zote na hususan elimu, watoto wao wanasoma International schools, Hatuwaelewi. Nchi ulizotaja zina maendeleo makubwa katika nyanja ya sayansi na teknolojia na pia maarifa mengi yanapatikana katika vitabu na mitandao mikubwa iliyo katika lugha ya kiingereza, kifaransa, kijapan, kijerumani, kichina na lugha nyingine.Sisi waswahili tunasubiri wabuni au wavumbue halafu sisi tutafute tafsiri. Mbona somo la kiswahili wanafunzi huko sekondari wanafeli sana kuliko hicho kingereza mnachokipiga vita!!? Heri nusu shari kuliko shari kamili. Tuendelee hivi na utoaji elimu tulio nao. Vinginevyo tuanze kwa utafiti na sio maneno. Utafiti wenyewe ufanyike hivi, zianzishwe shule za majaribio za kufundisha kwa kiswahili kuanzia chekechea hadi chuo Kikuu na hizi za mfumo wa kiingereza ziendelee halafu huko mbele tuje tupime mafanikio, na nyie mnaolilia kiswahili muwe wa kwanza kuwapeleka watoto wenu huko na sio kutoa kafara kwa watoto wa wenzenu
 
Soko la ndani tu hata robo hatujafika... Lazima tujiweze kujimudu ndio tuangalie nje... Hatuthamini vyetu... Em tuvikuze tuviboreshe vya kwetu kwanza ndio tuangalie nje.
Mfano wa Wamasai ni tofauti kabisa.
 
Haya ndiyo màajabu ya Watanzania, wote wanaopiga chapuo kiswahili kiwe ndiyo lugha mama kwenye nyanja zote na hususan elimu, watoto wao wanasoma International schools, Hatuwaelewi. Nchi ulizotaja zina maendeleo makubwa katika nyanja ya sayansi na teknolojia na pia maarifa mengi yanapatikana katika vitabu na mitandao mikubwa iliyo katika lugha ya kiingereza, kifaransa, kijapan, kijerumani, kichina na lugha nyingine.Sisi waswahili tunasubiri wabuni au wavumbue halafu sisi tutafute tafsiri. Mbona somo la kiswahili wanafunzi huko sekondari wanafeli sana kuliko hicho kingereza mnachokipiga vita!!? Heri nusu shari kuliko shari kamili. Tuendelee hivi na utoaji elimu tulio nao. Vinginevyo tuanze kwa utafiti na sio maneno. Utafiti wenyewe ufanyike hivi, zianzishwe shule za majaribio za kufundisha kwa kiswahili kuanzia chekechea hadi chuo Kikuu na hizi za mfumo wa kiingereza ziendelee halafu huko mbele tuje tupime mafanikio, na nyie mnaolilia kiswahili muwe wa kwanza kuwapeleka watoto wenu huko na sio kutoa kafara kwa watoto wa wenzenu
Unafikiri msemo wa "Penye miti hapana wajenzi" unaingia wapi Bright...!?

Basi kama kumpeleka mtoto International huna haki ya kupigia kelele kiswahili.. Na wasio na Ukimwi wasipige vita ukimwi.

Huwezi kutafuta Faida/mazuri ya kitu ikiwa bado una fikra hasi juu ya kitu hicho.

Tutakapo kua tayari kuwaza kuamua kubadilisha fikra zetu ndio tutakapo fanya maamuzi.

Natumai hatutakua tumechelewa.
 
Back
Top Bottom