Demokrasia: Umuhimu wa kushiriki kupiga kura

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
UCHAGUZI 2020: UMUHIMU WA KUPIGA KURA KWENYE NCHI YA KIDEMOKRASIA

photo_2020-09-29_16-57-33.jpg

Katika Jamii ya Kidemokrasia ni muhimu kuhakikisha Serikali inafuata matakwa ya Watu na sio watu kulazimishwa kufuata matakwa ya Serikali hivyo ni muhimu kushiriki kupiga kura ili uwe mmoja wa waliochagua Serikali wanayoitaka

Uzuri wa Demokrasia ni pale hata wale wanaoonekana wachache kupata nafasi kusema mawazo yao na wale ambao ni wengi wanapata fursa ya kufanya yao

Demokrasia iliyo hai inaonekana pale ambapo Wananchi wana uwezo wa kushuhudia jinsi Serikali waliyoipigia kura inavyoendesha nchi yao

Kupiga kura hujumuisha mkusanyiko wa watu kwa ajili ya kuamua hatma ya nchi au maslahi yao. Kupiga kura ni haki ya Wananchi wenye vigezo vya kushiriki zoezi hilo

Siku zote inashauriwa Watu kushiriki uchaguzi ili waweze kuamua hatma yao na kuchagua Serikali wanayoitaka.

Makosa ya kuepuka
Kama mpiga kura, unafahamu ni kitu gani ambacho hustahili kukifanya utakapokuwa kwenye kituo cha kupiga kura?
  • Ni makosa kutumia utambulisho wa kupiga kura ambao si wako yaani kadi ya kupiga kura au kitambulisho kisicho chako.
  • Hustahili kwenda kwenye kituo cha kupiga kura ukiwa umevalia sare zinazoashiria mrengo fulani.
  • Ni makosa kuanza kushawishi watu waliopanga foleni kwa nia ya kuwataka kumpigia kura mgombea fulani.
  • Ni makosa kuanza kuhonga wapiga kura kwa ajili ya kuwataka kumchagua mgombea.
  • Pia ni makosa kuanza kupiga picha bila idhini maalumu wakati zoezi la kupiga kura likiendelea.
  • Ni makosa kuchana au kuharibu karatasi ya kupiga kura bila kuruhusiwa kufanya hivyo.
  • Hairuhusiwi kupiga muhuri au kuweka alama yoyote kwenye karatasi ya kupiga kura.
  • Karatasi za kupiga kura haziuzwi kwa yeyote.
  • Pia huruhusiwi kupeana karatasi ya kupiga kura kwa yeyote tu unayemuona bila idhini maalumu.
Ukimaliza kupiga kura, karatasi za kupiga kura inastahili kuwekwa kwenye sanduku husika wala sio popote tu unapojisikia.
  • Hairuhusiwi kuweka kitu kingine chochote kwenye masanduku ya kupiga kura zaidi ya karatasi ya kupiga kura.
  • Ni makosa kuondoka na karatasi ya kupiga kura kutoka kituo cha kupiga kura.
  • Pia, usiharibu chochote ambacho kinaweza kutatiza shughuli ya upigaji kura.
  • Ni makosa makubwa kupiga kura zaidi ya mara moja.
  • Ni makosa kupatikana na karatasi ya kupiga kura ukiwa nje ya eneo la kupiga kura.
 
Sisi wanaccm hobby yetu ni kupiga kura kule chadema ni maneno maneno
 
Sisi wanaccm hobby yetu ni kupiga kura kule chadema ni manenomaneno
JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv,simu,games nk.

Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu... wameyakosa haya kwa miaka mi5.
 
nasikiaga DENON CRACIA ina uhusiano mkubwa na SHETANI ?

au masikio yangu ?
 
Sisi wanaccm hobby yetu ni kupiga kura kule chadema ni maneno maneno

Ccm haitegemei kura kushinda uchaguzi wowote, bali wanategemea nguvu ya mwenyekiti wao kwa kofia ya urais, kuagiza tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi, na vyombo vya dola kulinda ushindi haramu fullstop.
 
My vote counts only if there prevail a democratic system of elections from day one. Short of it, hakuna kitu.
 
Ccm haitegemei kura kushinda uchaguzi wowote, bali wanategemea nguvu ya mwenyekiti wao kwa kofia ya urais, kuagiza tume ya uchaguzi kumtangaza mshindi, na vyombo vya dola kulinda ushindi haramu fullstop.
We suppose to focus according our direction according our environment that's only way we can help our peoples no body should come and say that he is there to save the problems of our peoples we are the one we are leader we suppose to change the direction ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom