Umuhimu wa kulima na kutunza kumbukumbu na matukio ili tupate urahisi wa masoko

Konki kichaa

Senior Member
May 18, 2018
103
72
Habari wakulima wenzangu

Kwa miaka ya Nyuma kidogo ilionekana kulima ni umasikini na ufukara yani kuajiliwa ilikua ndo mwake mwake. Miaka hii kilimo ndo mpango mzima yani unakuta hata waajiriwa wanakumbuka kilimo yani kilimo kimekua dili na biashara

Ilinibidi nitafakari kidogo kipindi nimemwona Mzee JAKAYA KIKWETE na Mzee PINDA walivyostaafu wakaludi kwenye kilimo kwnn waludi kwenye kilimo wakati wana mahela ya pension. Nilivyowaza hivyo ikanibidi nikumbuke hadithi ya shuleni KAMA MNATAKA MALI MTAZIPATA SHAMBANI. Nikazidi kuwaza haya maswali

Kwanini nilime?
Nilime zao gani?
Nikilima nauzia wapi?
Mtaji wa kulima natoa wapi?

Nikapiga moyo konde nikaona suruhisho ya maswali yangu lazma nipate majibu. Kifupi sikutaka nilime ilimladi nionekane nimelima Bali natakiwa nilime kwa akili hata kama ni kidogo ila kiwe na tija

Mwanzo wa safari yangu ya kilimo nilianza kulima Maharage mwaka juz maeneo ya Songea. Mvua zilikua nyingi ziliharibu Maharage lakini nilibahatika kupata gunia 18 tu za Maharage katika heka 7. Nilikata tamaa lkn nikajiona bado nafasi ninayo ya kufanikiwa

Sasa nikakumbuka kua kila mwaka ktk miezi fulani kuna baadhi ya mazao huadimika au kupotea kabisa hii ni kwa sababu wengi hushindwa kuzalisha kwa sababu mbali mbali

Hapo nikatafuta mbinu za kuchunguza aina ya mazao ambayo baadhi ya miez huadimika kiukweli sikupata jibu Bali nilipata chance ya kumtembelea mjomba wangu yupo huko DSM kuna siku nilienda gengeni kununua nyanya nakumbuka ilikua mwez wa 2 aisee bei niliyoikuta huko nilimchukia hadi muuzaji yani nyanya moja 500/=

Hapo nikagundua kua hili zao limeadimika ndio mana limekua na bei hiyo nikajaribu kufuatilia uzalishaji wake kwa misimu tofauti tofauti nikagundua kua msimu wa masika ni ngumu kuzalisha nyanya kwa wingi

Ndipo mwaka Jana niliingia shambani mwez November na kulima heka moja nilipitia wakati mgumu kuzihudumia lkn mwez wa 1nikaanza kuvuna aisee wateja wanakufata shambani na wanakuabudu ndipo nikagundua kua ule usemi wa NYANYA NINYANYUE NA NYANYA NINYANYASE ni sahihi yani ukikosea kulima kulingana na msimu zao hili utaona baya kwa maana tenga la debe 7 utauza hata kwa 5000 lkn ukipatia msimu mzuri utapiga hela na zao hili litakunyanyua kiuchumi

MAMBO YA KUJIFUNZA

1: Nimejifunza ukitaka uwe mkulima mzuri lazma uwe mtunzaji wa kumbukumbu na matukio yani tutambue kua kuna baadhi ya matukio yakitokea kabla utaweza kujua mbeleni kutakua na upungufu gani

Mfano: Kenya walikumbwa na nzige kivyovyote vile wangekua na upungufu wa chakula wangelazimika kuja kununua kwetu

Pia, nchini mvua zilikua nyingi kana kwamba ziliharibu mazao hivyo itafanya upungufu wa chakula achilia mbali nchi za Jirani kuanza kutangaza njaa sasa hapa wakulima wenye mazao ndo fulsa kwetu kuuza kwa bei nzuri

2: Kupunguza muhemuko wa kuuza mazao. Wakulima wengi wanauza mazao kwa bei ya chini (hasara) kwakua amezalisha mazao mengi hii itatufanya wakulima tusiendelee

3: Kuhifadhi mazao mpaka yatakapoadimika ndipo tuyauze. Hii itatufanya tuepuke madalali yani wanunuzi watatufata wenyewe huko vijijini

ANGALIZO

Kwa wakulima wenzangu wenye nafaka Mahindi, mpunga ,ulez n.k huu mwaka ni wa neema kwetu hebu tuhifadhi nafaka zetu mpaka wastani mwez December hadi January hapo tutapiga hela nzuri

Nawakaribisha songea mje tulime ugumu wa huku ni mbali na dar hivyo uzalishaji upo na mazao yanapatikana lakini soko ndo tunalaliwa tu

Karibuni kuvuna Mahindi mana ndio msimu wetu huku kwetu

IMG-20190705-WA0003.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom