SoC01 Umuhimu wa kuhusisha kundi la vijana katika masuala ua uendelevu wa Mazingira kutokana na unyeti wake

Stories of Change - 2021 Competition

ROJA MIRO

Member
Jul 19, 2021
52
56
Sera ya vijana ya mwaka 2007 nchini Tanzania inatambua kwamba vijana ni watu wote wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35, ambapo kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ni asilimia 34.7 ya watu.

Uendelevu wa mazingira ni namna ya kuwa na jukumu la kuhifadhi maliasili,kulinda mazingira na ustawi wake kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Vijana ni mojawapo ya kundi muhimu sana katika Taifa lolote hata vitabu vya dini katika aya tofauti mara kadhaa vimezungumzia umuhimu wa kundi hili ,mfano kwenye Biblia kutoka kitabu cha,Timotheo 4:12 maandiko matakatifu yanasema,”Mtu yeyote asidharau ujana wako; Lakini uwe mfano wa waumini, kwa neno, kwa mazungumzo, kwa upendo, katika roho, kwa imani, katika usafi”.

Na kwenye Qur'an (11:14):. Mwenyezi Mungu anasema, “Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.” Kule utaulizwa ujana wako uliutumiaje?

Sasa turudi kuangalia umuhimu wa kundi la vijana katika suala zima la uendelevu wa mazingira kwa ujumla wake na hapa nitaonesha sababu na umuhimu wa kutumia kundi hili katika suala zima la uhifadhi na uendelevu wa mazingira na hizi ni mojawapo ya sababu na umuhimu wake:-

Kundi lenye idadi kubwa ya watu (Bilioni 1.8 Dunianini).Kama tulivyoona kwenye aya ya kwanza kwamba Tanzania ,34.7% ya watu wake wote ni vijana ambapo ni karibia watu 15,725,150 kati ya watu 44,929,002 kwa takwimu za sensa ya mwaka 2012 ingawa ripoti ya makadirio ya idadi ya watu ya Shirika la Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2017 Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 57,310,019 hivyo bila shaka idadi ya vijana pia inaweza ikawa imeongezeka.Umuhimu wa kundi hili katika masuala ya uendelevu wa mazingira ni kwa sababu endapo wakishirikishwa basi itakuwa elimu imefika kwa idadi kubwa ya watu na pia ndio kundi ambalo ni nguvu kazi kwa taifa.

Changamoto ya ajira huwasukumia kwenye mazingira. Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2016 inaonesha kwamba kila mwaka vijana 700,000 nchini Tanzania wanahitimu masomo katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo ni fursa 40,000 tu ndio huwa ajira za moja kwa moja hii ikimaanisha kwamba ni asilimia 6 tu ya vijana ambao wanapata kazi rasmi.

Baadhi ya vijana wanajikuta wakijishughulisha na shughuli ambazo zinapeleka uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti holela kwa ajili ya kuuza kuni,kuchoma mkaa,kupasua mbao na inakuwa ni kazi wanayoitegemea kwa ajili ya kipato kuendesha familia,hivyo Sera za kuunga mkono kazi zisizochafua mazingira ni shariti ziwe na mashiko na kujumuisha vijana.

Umri wa ujana (15-35) ni muda ambao wapo kwenye mfumo wa elimu.Kwa Tanzania mara nyingi mtu huanza shule akiwa na umri wa miaka 7 hivyo haadi anamaliza darasa la saba atakuwa na miaka 14,na akibahatika kwenda sekondari na elimu ya juu muda wake mwingi wa ujana atakuwa shuleni,hii ikimaanisha ni rahisi kulijumuisha kundi hili kwenye uelewa juu ya masuala ya mazingira kupitia mitaala ya elimu na pia kwa sababu ni kundi ambalo tunatarajiwa litakuwa limeelimika hivyo kutakuwa na kizazi kizuri baadae chenye elimu juu ya mazingira.

Kutokana na hayo nashauri yafuatayo yaweze kufanyika ili kuwa na uendelevu wa mazingira wakijumuishwa vijana katika jamii:-

Wapewe elimu ya utambuzi wa ajira zisizochafua mazingira.Idadi ya viongozi na vijana hususani barani Afrika waaokuza na kuboresha uchumi kwa kutumia bidhaa tena na tena (recycle) inaongezeka kwa kuchukulia mazingira kama chanzo cha ajira na kama kiteka uchumi. Sera za kuunga mkono kazi zisizochafua mazingira ni shariti ziwe na mashiko na kujumuisha vijana mfano,kutumia karatasi zilizotumika kubadili matumizi,chupa za plastiki,matumizi ya nishati jadidifu,mfano utengenezaji wa majiko yanayotumia kuni.

Masuala ya mazingira kutiliwa mkazo kwenye mitaala.Kwa kuwa tumeona kwamba muda wa ujana ndio ambao mtu anakuwa shule na amepevuka akili hivyo ni vyema agenda zinazohusu mazingira ni vyema zikawa kwenye mitaala ya shule hii itasaidia vijana ambao wapo shule wakutane za masuala ya mazingira na wale wa mtaani watakutana na vijana wenzao waliotoka shule na vyuoni hivyo kutokuwa na mchanganyiko mzuri utakaosaidia uendelevu katika masuala ya mazingira.

Mazingira ni ajenda muhimu sana kwani athari za uharibifu wa mazingira zimekuwa zikiathiri jamii moja kwa moja ,kumeshuhudiwa mafuriko ,ukame,onezeko la kina cha bahari na athari nyingine,mfano Kuanzia 1880 hadi 2012, wastani wa joto ulimwenguni uliongezeka kwa 0.85 ° C,na mwaka 1901 hadi 2010, kiwango cha wastani cha kina cha bahari kiliongezeka kwa cm 19 hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la la Umoja wa mataifa la mazingira (UNEP ) hivyo kwa ujumla jitihada zaidi zinahitajika kuchukuliwa na jamii,serikali na wadau mbalimbali wa mazingira bila kutosahau kuhusisha kundi hili la vijana ili kuhakikisha kunakuwa uendelevu wa mazingira.

ROJAMIRO.
 
PIGIA KURA STORI YANGU KIJANA MWEZANGU,PIA TOA MAONI YAKO JUU YA SUALA LA VIJANA NA UENDLEVU WA MAZINGIRA
 
Back
Top Bottom