Umuhimu wa Kuanzishwa Majimbo ya Uchaguzi ya Vyuo Vikuu

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Bara la Afrika hivi sasa linahitaji kuona wasomi wake waliojengwa kwa gharama kubwa wakilitumikia kwa uhuru mkubwa sana wakiongozwa na dhamira za weledi wao na nguvu zao za kitaaluma na kitaalam pasina kuingiliwa kisiasa katika yale ambayo wanayaibua kwa ushahidi wa kisayansi na ambayo wanafikiri yanaweza kuipeleka Afrika hatua nyingine zaidi ya kimaendeleo dhidi ya mataifa makubwa, hii itaondoa dhana kuwa wasomi wa Afrika wametekwa nyara na wanasiasa na kwamba wamezisaliti jamii zao.

Kuna hoja kuwa kama wanasiasa wameshindwa [ingawa mimi naamini wameweza kwa kiasi hicho walichoweza kwa miaka hiyo ya uhuru] wasomi nao kwa ujumla wao nao wameshindwa basi kuna kila dalili kuwa wafanyabiashara [business community] wanatafakari uwezekano wa kada yao kujaribu kuchukuwa hatamu za uongozi wa Afrika na hata nchi zingine nje ya Afrika ambazo nguvu za wanasiasa na wasomi zinadhaniwa kuwa zimefifishwa na ufisadi wa kidemokrasia na kiuchumi.

Hivi sasa jamii inajadili dhana kwamba katika Afrika, kunahitajika ukombozi wa pili toka katika makucha ya ukoloni mpya ambao Mwafrika anamkolonisha Mwafrika mwenzake kwa tofauti ya kipato, mawazo na dhamira ambavyo hivi vimejenga matabaka ndani ya jamii. Huu ni ukoloni mbaya kuliko ule tunaoujuwa wa kawaida ambao Mzungu alimtawala Mwafrika kabla ya kupata uhuru na hata ukoloni mambo leo. Ni ukoloni ambao ni mgumu kuutokomeza kwa sababu pamoja na sababu zingine mkoloni Mwafrika anaishi ndani ya Afrika na Waafrika wenzake. Zifuatazo ni baadhi tu ya manufaa ya ndani na nje ya kuanzishwa kwa majimbo ya uchaguzi ya taasisi za elimu ya juu.

Majimbo ya uchaguzi ya vyuo vikuu yatasaidia kujenga na kuimarisha uwezo wa kifikra za madiwani na kuzielekeza katika kuboresha mijadala yenye tija kwa ajili ya kuleta mapinduzi katika mfumo wa utendaji wa halmashauri husika ili kuwanufaisha wanajamii wake.

Uwezo mkubwa na tabia ya kiutafiti wa mambo wa wanazuoni ambao watafanyika wawakilishi wa majimbo ya uchaguzi ya vyuo vikuu utasaidia kuamsha ari ya wawakilishi wengine katika bunge na mabaraza ya madiwani ili kusaidia mihimili hii [bunge na mabaraza ya madiwani] kuchagiza utendaji wa tija wa serikali ili kuleta mabadiliko tarajali ya kimfumo ndani ya jamii ya kitanzania.

Kuziba ombwe la usomi kwenye mabaraza ya madiwani na bunge ambapo sheria zetu zinaainisha sifa za kugombea za chini kabisa kuwa ni 3Ks yaani kujuwa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu hali ambayo jamii imeshuhudia kwenye mabunge mengine na mabaraza ya madiwani kukiwa kuna mdororo wa mijadala na kupitisha hoja na miswada mingine ambayo baadaye katika utekelezaji wake vimeonekana kupwaya na kulazimika kurejeshwa bungeni au kwenye mabaraza ya madiwani ili kujadiliwa upya.

Uwezo wa mwanazuoni mmoja wa taasisi ya elimu ya juu katika kutafakari, kuelewa na kuwasilisha jambo; unawakilisha vichwa vya wabunge na madiwani wa aina ya 3Ks wapatao idadi sawa na wanafunzi ambao wanazuoni hawa wanawafundisha vyuoni. Hii pia itasaidia kujaza pengo la uwezo wa mijadala bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani ambalo limesababishwa na wawakilishi 3Ks waliochaguliwa kwa nguvu za misuli ya fedha zao. Hivyo bunge na mabaraza ya madiwani vitakuwa vimeweza kupata uwiano mzuri utakaowezesha kupatikana fursa nzuri za kujadili, kupitisha na kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kibunge na mabaraza ya madiwani.

Upanuzi huu wa demokrasia pia utasaidia kuwarudisha wasomi wa Afrika wanaoishi nje ya Afrika [diaspora] ambao waliondoka kwa njia kama za kurubuniwa kwa ahadi ambazo hawawezi kutekelezewa hapa nyumbani Afrika [braindrain]. Wasomi hawa ambao ni wakimbizi wa kitaaluma walioikimbia Afrika kutafuta kufanyakazi kwa uhuru wa kuheshimiwa mawazo yao ya kitaaluma na kitaalam katika kuitumikia jamii, sasa watajisikia furaha na ujasiri mwingi kurudi nyumbani Afrika wakijuwa kabisa kuwa zama mpya zimechomoza Afrika ambapo sasa mawazo na ushauri wao wa kitaaluma na kitaalamu vitakuwa na nguvu ya kuleta athari-chanya kwa maslahi ya jamii kwa kupitia demokrasia ya uwakilishi wa majimbo ya uchaguzi ya taasisi za elimu ya juu. Na kwa jinsi hii wataalamu na wanataaluma hawa watakuwa wamejisikia ahueni kuwa sasa watalipa deni la fadhila la jamii zao zilizowaandaa kwa gharama kubwa kwa ajili ya kuzitumikia. “Baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere katika moja ya falsafa zake aliwahi kuwafananisha wasomi na kundi teule la watu katika kijiji kimoja kilichokuwa na baa la njaa ndipo kundi hili teule likapewa chakula chote kidogo cha akiba wale ili waende mbali wakatafute chakula na kuleta kwa ajili ya kijiji kile, hili kundi baada ya kula chakula kile cha akiba na kushiba waliondoka na kutokomea kabisa, nukuu isiyo rasmi.”

Demokrasia hii pia itazipa bunge na mabaraza ya madiwani uwezo mkubwa wa kudurusu kabla ya kuridhia matamko ya jumuiya za kimataifa na pia mikataba mama ya uwekezaji ambayo imekuwa ikiziwajibisha serikali zote kuu na za mitaa katika pande mbalimbali za Afrika na kuleta misuguano kati ya mihimili hii miwili nyeti ya bunge/mabaraza ya madiwani na serikali. Ni muhimu sana kuwa na majimbo haya ili kupeleka bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani wanazuoni wa taasisi za elimu ya juu katika kipindi hiki ambacho Afrika inanyemelewa na kugombaniwa upya na mataifa makubwa yaliyo ng’ambo ya bahari [overseas] mithili ya kipindi kile cha mwaka 1884 - 1885 cha kuligawa bara la Afrika kwa wakoloni. Kama nilivyosema hapo awali kuwa wasomi wachache wa Afrika waliokuwepo enzi za kudai uhuru na ukombozi waliweza kuipa Afrika uhuru na ukombozi huo, iweje leo ambapo Afrika ina wanazuoni waliobobea na wengi kwa idadi yao; jitihada zao zishindwe kuokoa meli ya Afrika inayozama kwenye bahari ya kina kirefu?.

Iwe mwisho sasa wanazuoni kuitwa na kutazamwa kama wasaliti wa jamii zao na kwamba ni njia hii pekee ya kuingia bungeni na mabaraza ya madiwani kupitia majimbo ya uchaguzi ya taasisi za elimu ya juu ndiyo itakayowafanya wasikilizwe sauti zao za ukombozi wa jamii zao kwa sababu maamuzi ya kibunge na mabaraza ya madiwani huwa yana nguvu ya turufu dhidi ya mhimili wa serikali popote duniani. Mbinu za wanazuoni za muda mrefu za utafiti na uandishi wa kuzishauri serikali kwa manufaa ya jamii zao zimeonekana kugonga mwamba na kwamba sasa mbinu mpya ni hii ya kuingia bungeni na mabaraza ya madiwani kwa kigezo cha unyeti wa taasisi, taaluma na utaalamu wao. Hii itawafanya wawe wanasiasa wanaofanya siasa kisayansi tofauti na wanasiasa wa kawaida wanaofanya siasa kisiasa. Ikumbukwe kuwa siasa ni sayansi katika dunia ya leo ili ziweze kuwa na tija.

Wawakilishi wanazuoni hawa wataweza kuboresha kiwango cha elimu nchini kwa sababu watakuwa wakiwafundisha wanafunzi wao kwa ushahidi wa uhalisia wa mambo yanayotukia katika jamii kupitia mijadala ya bungeni na kwenye mabaraza ya madiwani ambapo wanafunzi watapata uelewa mpana sana wa masuala ya jamii zao na kuwa wabunifu wazuri wa suluhisho la matatizo ya jamii pale watakapojiunga na jamii hizo baada ya kufuzu mafunzo yao.

Wawakilishi hawa pia watapata fursa ya kujuwa mambo ya kutafiti kwa faida ya bunge/mabaraza ya madiwani na vyuo vyao wanavyovitumikia. Kwa jinsi hii taifa litakuwa moto katika utafiti wa mambo yanayoihusu na hii itasaidia kusukuma kasi ya maendeleo ambayo ili yapatikane siku zote hutegemea sana utafiti. Wana-academia siku zote wanaishi maisha ya ki-utafiti kwa asilimia kubwa.

Uwepo wa wawakilishi wanazuoni hawa bungeni na katika mabaraza ya madiwani utasaidia kuamsha ari ya kusoma makabrasha ya miswada, hoja, bajeti na mada zingine za kuhitaji mijadala na kwa jinsi hiyo uwepo wao utakuwa umesaidia kufisha tabia hatari ya kutosoma makabrasha unaofanywa na 3Ks ambao husubiri kurubuniwa na makundi ya kimtandao ndani ya bunge na mabaraza ya madiwani ili kupitisha hoja za mijadala yenye mivutano na mwelekeo wa itikadi za makundi pasina kufanya tafakari na utafiti wa kina wa athari za kurubuniwa huko. Baba wa taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuwahutubia wahitimu wa chuo kimoja maarufu hapa nchini wakati wa mahafali akiwaasa juu ya kutambua kuwa usomi wao ni dhamana kwa jamii na wala siyo dhamana yao binafsi akasema Hamjui kuwa hamjui na kutokujuwa kuwa hamjui kumewafanya msijuwe kuwa hamjui mpaka mtakapojuwa kuwa hamjui” Nukuu isiyo rasmi.

Wabunge na madiwani hawa wa taasisi za elimu ya juu watakuwa na muda wa kutosha kujikita katika masuala yenye sura ya kitaifa kutokana na kwamba majimbo yao tayari yana miundombinu muhimu na miradi ya maendeleo ambayo hayajafikiwa na majimbo mengine ya kawaida.

Wigo wa demokrasia ya kibunge na mabaraza ya madiwani utakuwa umepanuliwa kwa kiwango stahiki ambapo patakuwa na kambi tatu ndani ya bunge na mabaraza ya madiwani i.e. kambi ya chama tawala, kambi ya upinzani na kambi ya wabunge na madiwani wa majimbo ya taasisi za elimu ya juu ambao hawa watakuwa hawana vyama vya siasa bali watakuwa nyutro [neutral] na kambi yao iwe na nguvu ya turufu katika kusawazisha hoja zenye mwelekeo wa kukwama na kuleta tafrani kwenye vikao vya bunge na mabaraza ya madiwani.

Wabunge na madiwani wa majimbo ya taasisi za elimu ya juu waruhusiwe kuunga mkono hoja ya kambi yoyote kati ya chama tawala na upinzani kutegemea watakavyoona hoja ina maslahi kwa umma na siyo maslahi ya kichama na itikadi yake. Ili kufanikisha hili, wabunge na madiwani wa majimbo ya taasisi za elimu ya juu waruhusiwe ku-declare interest [kutoa tamko la kutokuwa/kuwa na maslahi] waingiapo kwenye vikao na shughuli zingine za kibunge na mabaraza ya madiwani ili kutohusisha ajira zao rasmi na shughuli zao za kibunge na ki-udiwani.

majwalaoriko@yahoo.co.uk
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu bado ni wachanga mno kiakili na kifikra kuweza kupewa nafasi ya maamuzi ya mwisho ya taifa lolote duniani.
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu bado ni wachanga mno kiakili na kifikra kuweza kupewa nafasi ya maamuzi ya mwisho ya taifa lolote duniani.
Mwambie CCM ilianzishaga na blah blah za sijui nini nini shirikisho la vyuo na wakawa wanawanec wao, yaani kifupi ilikua ni mkoa wa kichuo kikuu ukiwa na full reps hadi kwenye vikao vya juu vya chama mwisho wa siku wakatandua daruga

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu bado ni wachanga mno kiakili na kifikra kuweza kupewa nafasi ya maamuzi ya mwisho ya taifa lolote duniani.
Duh ! You can't be serious Mr. !! Kweli mwanafunzi wa chuo kikuu Ni mchanga!!! ,Mimi hapa Ni mtumishi wa umma , nategemea kwenda kujiendeleza miaka ya karibu mungu akipenda,sasa na Mimi unaniita mchanga with my 20+ years ya utumishi? Au wewe ukisikia neno mwanafunzi mawazo yako yanakimbilia darasa la kwanza na form one?


Vyuo vikuuu ukiachilia mbali fresh students from school,kule Kuna pia wazee wengi Sana wanaojiendeleza ili kuinua pensheni zao watakapo staafu.

Sina uhakika Kama wewe umesoma japo hata kufikia kidato Cha nne!!!

Unaowaona wakuu wa wilaya,wakurugenzi,nk. Ni zao la wanafunzi toka vyuo vikuuu

Poe Sana!!!!
 
Duh ! You can't be serious Mr. !! Kweli mwanafunzi wa chuo kikuu Ni mchanga!!! ,Mimi hapa Ni mtumishi wa umma , nategemea kwenda kujiendeleza miaka ya karibu mungu akipenda,sasa na Mimi unaniita mchanga with my 20+ years ya utumishi? Au wewe ukisikia neno mwanafunzi mawazo yako yanakimbilia darasa la kwanza na form one?


Vyuo vikuuu ukiachilia mbali fresh students from school,kule Kuna pia wazee wengi Sana wanaojiendeleza ili kuinua pensheni zao watakapo staafu.

Sina uhakika Kama wewe umesoma japo hata kufikia kidato Cha nne!!!

Unaowaona wakuu wa wilaya,wakurugenzi,nk. Ni zao la wanafunzi toka vyuo vikuuu

Poe Sana!!!!
Ukienda kijiendeleza chuo kikuu itakusaidia tu kuongeza salary scale yako ni kitu kizuri kwako. Nimesoma vyuo vikuu vitano viwili hapa nchini na vitatu nje. Utaalamu wangu ulifuata miaka mingi baada ya degree ya uzamivu. Sasa vile vitoto pale Mlimani ndio unataka vifanye maamuzi ya nchi hii? Kwa uzoefu upi!
 
Back
Top Bottom