Umuhimu wa ku-track metrics(data) za website yako, kila siku, masaa 24

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
85
131
JT6kRzGwV48_tMp8HA7xXaJzIiH3AIH1Zwix3Oq-nCzr76hSznvtxPTv9uznFuTPwgTKUVxKTdZ2k6GouTMnm_EoHb2NQMdqoLmDPvQPi3mgKbXQSxVlsIxK2nxyNdkoA3Owr3ST


(NB: UKITUMIA DAKIKA 7 KUTULIA NA KUSOMA NAKALA HII MPAKA MWISHO, UTAKUWA UMEONDOKA NA JAMBO KUBWA SANA LA KUBADILI BIASHARA YAKO MTANDAONI)

Moja ya sababu kubwa website nyingi za biashara zinakufa au zinadumaa, japokuwa website unakuta zinamuonekano mzuri, mpangilio mzuri na taarifa zilizowekwa zinaeweleweka, ni kuwa wamiliki wa websites hizi hawana taarifa(metrics au data) kuhusu utendaji kazi wa websites zao wa kila siku.

Makampuni yote makubwa unayoyafahamu duniani (AMAZON, MICROSOFT, ALIEXPRESS, AIRBNB, EBAY n.k ) yanafanya hii kazi ya ku-track metrics (data au taarifa) za website zao kila siku, masaa 24. Maana Taarifa hizi ndio ambazo zinawapa ushindi kwenye biashara zao mtandaoni.

Ninapoongelea Metrics za Website, kwa lugha rahisi ni vile vipimo ambavyo vinachukuliwa kwenye website ili kujua maendeleo ya website kila baada ya muda fulani. Vipimo hivi ni kama:


  • Idadi ya watembeleaji wa website na taarifa zao.
  • Bounce Rate (asilimia ya watembeleaji waliofungua website na kutoka ghafla).
  • Kurasa alizofungua mtu kabla ya kuondoka kwenye website.
  • Muda aliotumia mtu kwenye website yako.
  • Asilimia ya watu waliofungua website yako walipoiona kwenye google search.
  • Kasi ya watu kuondoka kwenye website yako na kurasa watu wasizokaa mda mrefu.
  • Idadi ya watembeleaji waliorudi mara ya pili au zaidi kwenye website yako.
  • Mda anaotumia mtu kwenye kurasa moj ya website.
  • Utimiaji wa malengo na matukio kwenye website.
  • Idadi ya watu walio-share website yako social media.
Kwahiyo unapokuwa na taarifa(website metrics) hizo kuhusu website yako inamaana itakusaidia kujua wapi ndani ya website yako panahitaji kupafanyia kazi ili kufikia malengo yako yale, uliyojiwekea wakati ulipokuwa unatengeneza hiyo website.

Kabla sijakuonesha namna ya ku-track hizo metrics bure kwenye website yako, ngoja kwanza nikuoneshe faida 9 kubwa za ku-track taarifa(data au metrics) za website yako kila siku;


Kupima na Kujua Idadi ya Watembeleaji wa Website yako.
  • Ukiwa unafuatilia taarifa za website yako, utaweza kutambua idadi ya watu wanaotembelea website kila siku. Na sio hilo tu utajua taarifa zaidi za muhimu kuhusu watu hao wanaokutembelea, taarifa kama;

  • Wametokea maeneo gani?
  • Wanatumia vifaa gani vya internet?
  • Wanafanya nini kwenye website?
  • Muda wanaotumia kwenye website? n.k
Taarifa hizi na nyingi zaidi ukiwa nazo zitakusaidia kuwatambua watu wanaokutembelea na kujua nini cha kufanya ili kuboresha utendaji kazi wa website yako.

Kutambua “Bounce Rate” ya website yako.

  • Bounce rate ni asilimia ya watembeleaji wanaofungua website yako bila kufanya chochote kile na kuondoka ghafla, aidha hawajapenda muonekano au hawajaona walichokua wanakitaka.
  • Bounce rate ikiwa kubwa inamaana kuwa, ni watu wengi wanaondoka ghafla na kwahiyo ukiwa unalifahamu hilo itakusaidia kuepusha watu zaidi kuondoka ghafla kwenye website kwa kufanyia kazi mambo mawili makubwa nliyokutajia hapo juu yanayosababisha watu kuondoka kwenye website.
Kujua utendaji kazi wa website yako, kimasoko zaidi.
  • Hapa ninacho maanisha ni kuwa unahitaji kujua kampeni zako za kimasoko zinaendaje kila siku. Ninaposema kampeni za kimasoko namaanisha, kuna vitu au huduma ambazo kupitia website unazitangaza kwa namna yoyote ile unayofanya.

  • Sasa ni vema kujua kila hatua ambayo mtu anaipitia kwenye kampeni yako ya kimasoko uliyoiweka kwenye website yako.

  • Mfano; unaweza ku-track watu wanaobonyeza button fulani, au waliofika kwenye ukurasa fulani ambao upo kwenye mtiririko wa kampeni yako.
Kushika nafasi za juu zaidi kwenye Google Search.

  • Kupitia taarifa utakazokuwa unapata kila siku kuhusu website yako, unaweza kujua mambo gani yanayokuzuia wewe kuwa nafasi ya juu zaidi kwenye google.

  • Mambo haya mawili ni muhimu sana kwa Google katika kuifanya website iwe nafasi ya juu. Moja, ni “Bounce Rate” na mbili ni “Click-Through-Rate (CTR) “ (CTR - ni Asilimia ya watu waliofungua website yako mara wanapoiona kwenye google search)

  • Kwa hiyo kushindwa kujua mienendo ya website yako katika hayo mambo mawili, kwa kweli unapoteza nafasi kubwa sana ya kuifanya website yako ishike nafasi za juu kwenye google search.
Kupata wateja na wafuasi sahihi kwenye website yako.

  • Hili ni suala ambalo watu wengi linawasumbua, na njia rahisi zaidi ni kwa ku-track taarifa kuhusu watembeleaji wa website yako wanapokuwa online.

  • Ukiweza kujua watembeleaji wako wengi wanapenda kufanya nini wanapokuwa kwenye website yako, basi utaweza kuongeza nguvu katika hilo na moja kwa moja ukapata watu sahihi na wanaofaa kwenye biashara yako.
Kuongeza utendaji kazi wa website yako na huduma zake.

  • Ukiwa na uwezo wa ku-track taarifa za website yako, ina maana utakuwa unaona pia matatizo watu wanayopitia wanapokuwa humo, hivyo ukiweza kuyajua na kuyatua utakuwa umeboresha huduma kwa watu wako.

  • Mfano; kupitia Analytics, ukaona watumiaji wote wa simu wakiingia kwenye website wanageuza ghafla na kuondoka, inamaana utachukua hatua na kuangalia website yako kwa kutumia simu, ukagundua muonekano wa website kwa watumiaji wa simu si mzuri, then ukifanya marekebisho utakuwa umeongeza kitu kikubwa na umesaidia watu wako.

Kuongeza asilimia ya kutimia kwa malengo yako kwenye website.

  • Kwa lugha ya kiufundi kidogo tunaita “Conversion Rate Optimization (CRO) “, hiki ni kitendo cha kufanyia kazi mambo ambayo yanasabisha malengo yako ya kibiashara kwenye website kuwa hafifu.

  • Hutoweza kulifanya suala hili, kama hutokuwa unafahamu taarifa za kila siku za website yako na watembeleaji wake. Na kwahiyo ukiweza kutambua taarifa za website yako utaweza kuona kuwa malengo yako yapo kiwango gani na wapi upafanyie kazi ili kuongeza zaidi.

Kufuatilia matokeo ya malengo ya biashara yako kwenye website.

  • Pia ukiwa una-track data za website yako, kwa kuweka malengo yako katika mfumo wa kidigital kutumia kifaa kama analytics, utaweza kuona matokeo ya malengo uliojiwekea kila baada ya muda fulani.

Kuboresha matokeo ya matangazo yako ya kulipia ya mtandaoni.

  • Ukiwa una-track data za website yako kila siku, itakuja kukusaidia badae utakapoanza kufanya matangazo ya kulipia mtandaoni (kama, Google Ads na Facebook Ads).

  • Data zaidi unazokuwa nazo kuhusu watembeleaji wa website yako mtandaoni, zinasaidia Google na Facebook kukutangazia matangazo yako kwa aina ya watu unaohitaji matangazo yako yawafikie.

NAMNA YA KU-TRACK METRICS ZA WEBSITE YAKO BURE KILA SIKU MASAA 24.

Ku-track hizo metrics za website yako kila siku unahitaji msaada wa vifaa ambavyo vitakuwa vinafanya kazi ya kusanya hizo taarifa kuhusu website yako masaa 24.

Kuna vifaa vya bure na vya kulipia, lakini bado vifaa vya bure vinatosha sana kukusaidia kupata taarifa zote unazohitaji kuhusu matukio ya website yako ya kila siku.

Hivi ni vifaa vya bure ambavyo ni muhimu sana kuvitumia;


  • Google Analytics
  • Google Tag Manager
  • Google Search Console
  • Facebook Pixel

Niliamua kuandaa NAKALA rahisi ya hatua kwa hatua (ikiwa na picha), ambayo itakuonesha namna ya kuvitumia vifaa hivi ili kuweza kupata (ku-track) taarifa(metrics/data) zote muhimu kuhusu website yako kwa matumizi ya sasa na hata badae pia.

Nakala hiyo ni BURE kabisa na vifaa hivyo kuvitumia ni BURE pia. Bonyeza link iliyopo chini hapo ili uweze kupakua (DOWNLOAD) nakala yako bure.

DOWNLOAD HAPA:
https://track.erickngimba.com/


Have a Great Day!
 
Back
Top Bottom