Umuhimu wa Katiba mpya umeendeleea kuonekana

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
269
511
Sakata la kurushiana maneno kati ya wakuu wa mihimili linaloendelea linatoa funzo kuhusu mambo yafuatayo.

1. Madaraka makubwa aliyonayo Rais - Vyama pinzani waliteswa na wanaendelea kuteswa na mfumo huo lakini sasa mkono huo mpana wa Mhimili huo umetua kwa ndugu zake. Hii ilianza kipindi cha Jiwe ambapo akina Nape, Makamba, na Kinana walitengwa na kuonekana wasaliti sasa ni zamu ya Ndugai, Polepole n.k.

2. Umuhimu wa Mgombea binafsi katika nafasi za kisiasa.
Kama Job Ndugai angekuwa Mbunge kutokana na kundi hili huenda yanayoendelea yasingekuwa na impact kubwa kwake. Vyama vya siasa pamoja na nafasi yake kubwa ktk siasa lakini vinatuangusha sana wananchi linapokuja suala la maslahi ya vyama kupokwa na wachache dhidi ya maslahi ya Taifa.

3. Tume huru ya uchaguzi - Viongozi imara na walio huru kutoa mawazo yao kwa maslahi ya Wananchi watatokana na uchaguzi ulio huru na wa haki. Asilimia kubwa ya Wabunge waliopo bungeni hawakuchaguliwa na Wananchi ndiyo maana wako radhi kumtetea mtu katika mhimili flani wakiamini kuwa watabebwa tena ktk chaguzi zijazo.

4. Uwazi wa mikataba ya nchi na uendeshaji wa serikali - Kama wananchi wangekuwa wanawekwa wazi kwa kila hatua ya mikopo iliyokuwa ikichukuliwa na matumizi yake yanayoendelea sasa yasingetokea.
 
1641379370253.png
 
Wanasema kila mara mikopo ni ya masharti nafuu, ila hawasemi hayo masharti nafuu ninyapi kwa kila mikopo.
 
Back
Top Bottom