Umuhimu wa Katiba Mpya Sasa ni Kikohozi Kisichozuilika

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
0
Wandugu,
Kama kuna wakati ambao umuhimu wa katiba mpya umedhihirika basi ni sasa. Kwa kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka huu, watanzania walio wengi sasa wametambua kwamba kikwazo kikubwa cha jitihada zao za kujikomboa kisiasa, kiuchumi na hata kijamii ni katiba. Wananchi wengi wameshuhudia jinsi uamuzi wao kwenye sanduku la uchaguzi unavyoweza kupindishwa na kikundi kidogo cha wananchi kwa maslahi yake. Kwamba chini ya katiba iliyopo wananchi wanaweza kuongozwa na watu wasiowataka.

Ndiyo maana sauti za kudai katiba zimeongezeka kutoka katika pande zote za nchi. Sasa ni dhahiri kwamba umuhimu wa katiba mpya umekuwa sawa na kikohozi. Jk na serikali yake wasidiriki hata kidogo kuzuia sauti hizo. Hazitazuilika kamwe hata nguvu ya kijeshi ikitumika. Wakati umefika na hauwezi kuahirishwa. Lazima nchi yetu iingie kwenye uchaguzi wa 2015 ikiwa na katiba mpya na bila kumwaga damu ya wasio na hatia, kama ilivyotokea Kenya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom