sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Dini yoyote ile bila mwongozo haijawa dini,ndiyo maana kuna msahafu na biblia takatifu ambavyo ndivyo mwongozo wa mwenyezi Mungu kuwaongoza waja wake. Yeyote yule awaye akitenda kinyume na maandiko hayo matakatifu atakuwa ametenda dhambi,si kwamba watu hawatendi dhambi,la hasha mara wanapogundua wameangukia kwenye dhambi au mifarakano hurudi kwenye vitabu hivyo na kumrudia Allah kwa kufanya toba.
Halikadhali kwenye uongozi wetu wa kidunia tuna katiba zetu tulizojiwekea kama mwongozo katika maisha yetu ya kila siku,mwongozo huo hupelekea viongozi wetu kutuongoza kwa kufuata amri(sheria) katika kuwatumikia wananchi wake.
Tofauti ya katiba zetu na katiba ya Mwenyezi Mungu ni kuwa mwongozo wa Allah haufanyiwi marekebisho na binadamu,lakini pia mwongozo huo ni amri na maarimsho halali yasiyopingwa na kiumbe chochote isipokuwa Mwenyezi Mungu mwenyewe hali iliyopelekea kuandika vitabu hivyo vitakatifu kupitia wahayi. Lakini katiba ama mwongozo wa dunia huandikwa kwa matakwa ya wananchi kwa kuridhia serikali za kidunia kuongozwa kwa matakwa ya sheria waliyojiwekea wananchi husika kupitia katiba zao. Hivyo basi katiba hizi hubadilika kutokana na matakwa ya wananchi wenyewe kwa wakati huo.
Mahitaji makubwa ya wananchi wa Tanzania ni katiba,katiba itokanayo na matakwa ya wananchi itakayoendana na wakati uliopo. Tanzania haijawahi kuwa na katiba iliyotokana na maoni ya wananchi,katiba iliyopo haikuhusisha au kushirikisha wananchi zaidi ya viongozi wachache kama nitakavyoelezea hapo chini.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ilitokana na tume ya rais iliyokuwa na wajumbe 20(10 toka kila upande wa Muungano) ikiongozwa na sheikh Thabit Kombo katibu wake akiwa mh. Pius Msekwa. Tume hii ilianza kwa kutunga katiba ya CCM ambayo ilizaliwa baada ya kuungana ASP name TANU terehe 5 mwezi 2 mwaka 1977. Katiba hiyo ilijikita katika misingi mikuu mitatu, urais(uliomtengeneza na kumfanya rais-mfalme),mfumo wa chama kimoja cha siasa na muundo wa serikali mbili. Katiba hii ya mwaka 1977 ikapitishwa na bunge maalum lililogeuzwa toka bunge la kawaida.
Katiba hii imefanyiwa mabadiliko 14 toka kupitishwa kwake mwaka 1977,mengi ya mabadiliko yake yamekuwa yakikwepa ushirikishwaji wa wananchi isipokuwa mabadiliko yaliyofanywa 1983-1984 ambayo angalau ushirikishwaji wa wananchi uliguswa kwa namna moja au nyingine. Katika mabadiliko hayo NEC ilianzisha mjadala kwa wananchi badala ya kufanya maamuzi pekee yake.
MABADILIKO YA KWANZA
Madiliko haya yalifanyika miaka miwili tu baada ya kuandikwa kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Jambo kuu katika mabadiliko haya ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Rufani inayofanya kazi katika Jamhuri yote ya Muungano.
1980
MABADILIKO YA PILI
Mabadiliko haya yalikuja kama sehemu ya kujaribu kushughulikia kero mbalimbali za muungano. Lengo lilikuwa kujibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiibuka toka Zanzibar. Ilitarajiwa kuwa marekebisho haya ya pili ya Katiba yangesaidia kuimarisha muungano jambo ambalo kwa bahati mbaya halikutokea na kupelekea marekebisho mengine mwaka huohuo.
1980
MABADILIKO YA TATU
Mabadiliko haya ni ya pili katika mwaka huohuo wa 1980. Kitaaluma, hii huwa ni dalili ya katiba mbovu. Mabadiliko haya yalikuja kuweka sawa mfumo wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, mfumo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na muundo wa Baraza la Wawakilishi.
1982
MABADILIKO YA NNE
Mabadiliko haya yalilenga kuboresha utaratibu wa uteuzi wa wakuu wa mikoa. Hata hivyo, mabadiliko hayo bado yaliendelea kulalamikiwa kwa kutoweka bayana uwajibikaji wa viongozi hao wa mikoa na wilaya.
1984
MABADILIKO YA TANO
Mabadiliko haya yalikuja kufuatia madai ya muda mrefu ya kutaka kuwepo kwa uhuru mpana zaidi pamoja na haki za binadamu katika Katiba. Hatimaye mabadiliko haya yaliingiza tamko la haki za binaadamu kwenye katiba ya nchi sehemu nzima ya tatu.
1990
MABADILIKO YA SITA
Mabadiliko haya yalianzisha rasmi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yakiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 1995. Kabla ya hapo maswala ya uchaguzi yalisimamiwa na chama. Hata hivyo kiu ya wananchi kutaka demokrasia halisi ya uchaguzi haikumalizwa na mabadiliko haya.
1990
MABADILIKO YA SABA
Katika mwaka huohuo yalikuja mabadiliko ya saba ya Katiba ya Tanzania ambayo yaliweka utaratibu wa kupata mgombea mmoja wa Urais kwa Zanzibar. Mfumo uliotangulia ulikosa uwazi wa namna ya kumpata mgombea wa urais kwa upande wa Zanzibar.
1992
MABADILIKO YA NANE
Mabadiliko haya yalikuja wakati kukiwa na vuguvugu la mabadiliko kidunia kuelekea demokrasia ya vyama vingi. Mabadiliko ya nane yalifuta rasmi mfumo wa chama kimoja nchini na kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa. Aidha muundo wa bunge la muungano ulibadilika na kuanzisha viti maalumu vya wanawake kufikia asilimia 15 na viti vitano (5) toka Baraza la wawakilishi. Uandikishaji wa vyama vya siasa na uteuzi wa wagombea kupitia vyama vya siasa ulianzishwa na mabadiliko haya.
1992
MABADILIKO YA TISA
Miezi sita baada ya mabadiliko ya nane, mabadiliko mengine yalifanywa kurekebisha utaratibu wa uchaguzi wa Rais wa Muungano, kutamka kuwa Rais anaweza kuondolewa kwa kura ya bunge kutokuwa na imani naye, kuanzisha nafasi ya Waziri Mkuu kikatiba na namna ya kumwondoa kwa kura ya kutokuwa na imani naye pia.
1993
MABADILIKO YA KUMI
Mabadiliko haya yalikuja kuhamisha chaguzi za madiwani kuweza kufanyika pamoja na uchaguzi wa Rais na Wabunge. Pia, mabadiliko haya yaliipa mamlaka Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kusimamia chaguzi hizo.
1994
MABADILIKO YA KUMI NA MOJA
Mabadiliko haya yalikuja wakati nchi ikijitayarisha kwenda kwenye Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi vya siasa mwaka 1995. Mapendekezo ya mabadiliko haya yalitokana na ushauri wa Tume ya Jaji Mark Bomani ambayo ilipendekeza kuwepo kwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano. Mgombea mwenza huyo angekuwa ndiye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuanzia hapo, Rais wa Zanzibar aliacha kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano lakini alibaki kwenye Baraza la Mawaziri kama mjumbe tu.
1995
MABADILIKO YA KUMI NA MBILI
Mabadiliko haya yalipitishwa mwishoni mwa mwaka 1995 kabla ya bunge kuvunjwa rasmi na kuruhusu uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi. Aidha mabadiliko haya pia yaliweka kiapo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Makamu wake, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar kula kiapo cha kulinda muungano. Mabadiliko haya pia yaliweka ukomo wa Rais kuwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.
2000
MABADILIKO YA KUMI NA TATU
Mabadiliko haya yalikuja baada ya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Tanzania. Kwanza, kwa mara ya kwanza Rais anaweza kuchaguliwa na kutangazwa mshindi kwa kupata kura zozote zile ili mradi awazidi wengine. Kabla mabadiliko haya, Mgombea urais asingeweza kutangazwa bila kupata angalau asilimia 51% ya kura zote zilizopigwa. Kwa sasa, hoja ni wingi wa kura tu na hivyo kuondoa uwezekano wa kura kurudiwa. Pia, mabadiliko hayo yalimpa Rais uwezo kuteua watanzania 10 kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano. Aidha, mabadiliko hayo pia yaliongeza viti maalum vya wanawake toka 15% hadi 20%.
2005
MABADILIKO YA KUMI NA NNE
Mabadiliko ya mwaka 2005 yaliongeza viti maalum vya wanawake kutoka 20% hadi asimilia 30. Pia, mabadiliko haya yaliweka bayana zaidi uhuru wa kuabudu, uhuru wa kushiriki na watu wengine, uhuru wa maoni na kujieleza na kuondoa vizuizi vyote vilivyokuwepo kwenye Katiba. Kingine ni kwamba mabadiliko haya yaliweka utaratibu wa kuteua wabunge wa viti maalum vya wanawake kutegemeana na uwiano wa ushindi wa kila chama katika kura za ubunge majimboni.
Ukitazama mabadîlikô haya hutaona ni kwa nini kuna uhitaji wa katiba mpya,pamoja na mabadîliko ya 1992 kuelekea mfumo wa vyama vingi,bado katîba hii imeendelea kumtengeneza rais-mfalme asiye ambilika mwenye kiburi kutokana na madaraka aliyo limbikiwa.
Katiba hii pamoja na mabadiliko yake 14 bado inaakisi mfumo wa chama kimôjà kwa nafasi za uteuzi unaosababisha mgongano wa upèndeleo kimamlaka kwa lengo la kumbeba mtawala,mathalani tume ya taifa ya uchaguzi inayo teuliwa na rais ambaye mwenyekiti chama cha siasa kinacho shiriki uchaguzi unaosimamiwa na tume hiyo.