Umuhimu wa huduma za ushauri wa kitaalamu (consultancy)

shilla de sam

Member
Jan 7, 2013
8
3
Habari Tanzania!

Umewahi kujiuliza ni kwa kiwango gani Ushauri wa Kitaalam (Consultancy) ni muhimu katika uanzishaji, endelezaji na kufanikisha shughuli zetu za Kibiashara, Miradi mbalimbali, Ujasiriamali, n.k?

Pia, kwa kiasi gani watanzania tumekuwa tukipata ushauri toka kwa Wataalamu wetu kuhusu masuala tofauti tofauti.

a. Je, umewahi kwenda kwa mtaalamu mshauri kupata ushauri wowote kwa kuchangia pesa kidogo?
b. Kama hujawahi kufanya hivyo, unadhani nini ni changamoto?
c. Je, tuna wataalamu wenye uwezo wa kutoa ushauri kwa Watanzania?
 
Wengi tunaogopa gharama lakini nakubaliana na wewe kabisa, ukitaka ufanikiwe tafuta consultant .....
Sidhani kama gharama ni kubwa kiasi cha kuogopa, changamoto ni kwamba kulipia ushauri siyo utamaduni wetu watanzania!
 
Waafrika hawana ethics anaweza uza idea yako

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ndo haswaa, na pia consultants wengi, ukiwasikiliza, they don't know deeply the consultancy they are offering, huwa hainiingii akillini unakutana na consultant badala ya yeye kukushauri, anaishia kuuliza uliza maswali tuu na kushangaa kila unchokisema
 
Hii ndo haswaa, na pia consultants wengi, ukiwasikiliza, they don't know deeply the consultancy they are offering, huwa hainiingii akillini unakutana na consultant badala ya yeye kukushauri, anaishia kuuliza uliza maswali tuu na kushangaa kila unchokisema
Kitaalam kuna hatua za kufuata katika utoaji wa huduma ya ushauri wa Kitaalam kwa wateja, kama mtu anajiita consultant na hafuati hatua hizo basi huyo hafai kuwa Mtoa Huduma. Lakini ni muhimu kujua kuwa Consultant ili atoe ushauri stahiki ni lazima ajue tatizo/changamoto inayomkumba client wake!
 
Changamoto ni Mtanzania unaye mpa ushauri anajua kukuzidi wewe mtaalamu. Mtanzania anaheshimu ushauri wa daktari tu pale anapoona anakaribia kukata rohoo🤣
Huu ulioongea mkuu ndio ukweli halisi wabongo ni wajuaji to infinite and beyond
 
Back
Top Bottom