Umuhimu wa 'Conciliatory Politics' kwa wabunge wetu Katika Karne ya 21!

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Wadau salam,

naomba nitoe ushauri wangu kwa wanasiasa wanaohusika kwa maslahi yao na ya nchi yetu kwa ujumla.

Kiongozi/mwanasiasa hasa katika ngazi ya Ubunge/udiwani, kazi yake kubwa ni kushwawishi na wala si kutenda.Kazi ya mbunge kwa mfano, ni kushawishi serikali na idara zake,taasisi mbali mbali pamoja na wananchi katika eneo lake katika kuleta maendeleo ya eneo husika na wala si mbunge kuleta maendeleo ya eneo husika.Hivyo basi; kwa kadiri mbunge anavyofanikiwa kushawishi (ambayo ndio kazi yake ya msingi) ndivyo tunavyoweza kumuhesabu kama mbunge aliefanya vizuri!.

Ili kiongozi (mbunge/diwani) aweze kushawishi , ni lazima awe na vitu vitano kama ifuatavyo;

1.Uhusiano mwema na unaotaka kuwashawishi; Ni vigumu kumshawishi mtu ambaye uhusiano wenu ni wa mbwa na paka hata kama una hoja nzuri.

2. Lazima awe na dira (vision);Haiwezi kuingia akilini mtu akawa anawashawishi wenzake kueleke ambako hata yeye mwenyewe hapajui.

3.Hoja; Ni lazima mwanasiasa awe na hoja ambazo zinaweza kueleweka kwa anaowashawishi

4. Lugha ya busara: Binadamu/watu wazima hupenda kusemeshwa kwa adabu.Ukimsemesha vibaya hata kama una hoja nzuri,;badala ya kukusikiliza hukujengea uadui, na hayo ndio maumbile ya binadamu.

5. Kuwa flexible; Wakati fulani kiongozi huweza kuwa na wazo zuri na namna ya utekelezaji wa wazo lake lakini baada ya kuwasiliana na vyombo/watu wengine, ikaonekana kwamba wazo lake haliwezekani kutekelezwa kama lilivyo,au kuna wazo bora zaidi ya lake.Kama muhusika asipokuwa flexible hawezi kufanikiwa.

Ndugu zangu, kwa leo niongelee kwa undani kidogo, jambo la kwanza hapo juu, (Uhusiano na watu wengine). Inavyoonekana kuna tatizo kubwa la kutokuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya wanasiasa (wabunge/madiwani) na wadau wengine katika majimbo kadhaa hasa zaidi zaidi katika baadhi ya majimbo yanayoongozwa na upinzani.Unaweza kukuta Mbunge hawaelewani kabisa na RC, Haelewani kabisa na DC, haelewani kabisa na RPC, haelewani kabisa na DED, Haelewani kabisa na polisi kama taasisi, haelewani na OCD n.k. Kutokuelewana huko, kwa kiwango kikubwa hali hiyo ya uhusiano mbovu husababiswa na mbunge husika kushindwa kutumia "Conciliatory approach" katika siasa zake kwenye mambo ya msingi.

Ndugu zangu, katika karne ya 21, ambapo uongozi na utawala kwa kiwango kikubwa uko katika mifumo ya kitaasisi, maendeleo katika eneo fulani huletwa kwa ushirikiano wa watu na taasisi mbalimbali .Taasisi hizo ni mfano wa watu wengi wanaosukuma jiwe moja (maendeleo!).Sasa kama mbunge atakuwa yeye hana uhusiano mwema na taasisi nyingine, ni vigumu sana kuzishawishi taasisi hizo na wadau kutoka taasisi husika katika kutekeleza lile analodhani kwamba ndilo lingefaa kutekelezwa, kinyume chake nia njema hukosekana na wadau huanza kupigana mitama wakati wanasukuma jiwe na mwishowe jiwe huwarudia na kuwasaga wote!.Kushindwa huko huashiria kushindwa kwa kiongozi/mbunge husika.

Ninachoweza kushauri tu ni kwamba; hebu wabunge na madiwani ambao bado walikuwa hawajangundua ubora wa mfumo wa "Conciliatory politics" , waujaribu waone how worthy it is! japo ni muda mfupi tu umebaki kuelekea uchaguzi ila nadhani wanaweza kufanya jambo!.Mbinu hii ya maridhiano kwenye mambo ya msingi huleta hisia za "Good will " miongoni mwa wadau na kuwafanya wawe na ari ya kuleta maendeleo katika eneo husika!. Hebu jaribuni kufanya kazi kwa kuwa na ushirikiano na wadau wa taasisi nyingine zaidi ya vyama vyenu vya siasa halafu mtaona mafanikio yake!.Kinyume chake kuna wabunge watamaliza muda wao hakuna walichofanya kwenye maeneo yao.

anayeona inamfaa kazi iwake!

 
Ni lazima vilele vile tukaelewa kwamba maendeleo katika jamii kwa kiwango kikubwa huchochewa na nia njewa miongoni mwa wadau na kwa kiwango kikubwa nia njema hujengwa na uhusiano wa kijamii unaokuwepo.Kwa hiyo kwa mfano ufanisi mkubwa wa maendeleleo ya kiuchumi katika eneo, huchochewa na nia njema ya wadau wa eneo husika kuliko kitu kingine chochote na nia njema hiyo huchochewa na mahusiano yao wenyewe.Kwa mfano, Unaweza ukakuta DC, Ana wazo fulani la kimaendeleo na kuna jinsi anavyoweza kulisimamia likaleta tija, Mbunge naye lablda ana yake lakini uhusiano kati ya DC na mbunge husika ni mtafutano! kila mmoja hana imani na mwenzake, hivyo wala hawawezi kukaa chini wakazungumza vizuri isipokua linapotokea tukio ambapo hukutana na kuoneshana umwamba.Sasa katika mazingira kama hayo, kisaikolojia ni rahisi sana kwa DC, Kuacha kufanyia kazi wazo lake (licha ya kujua manufaa yake) kwa kuchelea kumpa credit mbunge ambaye hawana uhusiano mzuri! mwisho wa siku unakuta maendeleo katika eneo husika yanadorora. Jambo hili linaweza kuepukwa kwa kuwa na siasa za maridhiano, masikilizano, na kuheshimiana.
 
Vile vile katika siasa inawezekana anayekuunga mkono leo akakupinga kesho na anayekupinga leo akakuunga mkono kesho, hivyo hakuna haja ya kuendesha siasa za uadui, chuki,kudharauliana, kupuuzana, kuzalilishana, kutunishiana misuli n.k kwa sababu hhuwezi kuijua kesho yako.Ni bora kama jambo mtu hulijui, ukawauliza wanaojua kuliko kulazimishia mwishowe utaumbuka!. Ni bora kustahimiliana na kutofautiana kistaarabu huku wadau wote wakijua kwamba kila mtu ni mdau wa maendeleo katika sekta na fani yake na ni mtu mzima mwenye akili timamu.Kama tukifanya hivyo tutaweza kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia.vile vile yule atakayeshindwa katika uchaguzi; atakuwa hana haja ya kujificha sababu ya aibu.
 
dah! staki kuamini kama uzi umekosa wachangiaji.Yaani toka jana nyuzi zile zile! wachangiaji hawaonekani!. Aisee!!!
 
Wabunge wa upinzani na waende bungeni, watulie na waahirikiane na wenzao wa Ccm, Kwa pamoja wajadili na kupitisha mabadiliko ya sheria ya madini Kwa maslahi mapana ya nchi
 
Back
Top Bottom