Umuhimu wa AVN Number kuomba Mkopo HESLB

RANGOE

New Member
May 23, 2022
3
0
Habari wakuu...

Naomba Kuuliza, kama nina AVN namba kuna umuhimu wa Kutumia Cheti cha Diploma Kuomba Mkopo elimu ya juu HESLB?
 
Kwenye system sijaona wakiomba Avn wanataka cheti
Duuh Ahsante mkuu.. Isha kula kwangu maana chuoni sijakomboa cheti nadaiwa lakini nimeverify Nacte Kumbe chuo walipeleka taarifa zangu
 
Duuh Ahsante mkuu.. Isha kula kwangu maana chuoni sijakomboa cheti nadaiwa lakini nimeverify Nacte Kumbe chuo walipeleka taarifa zangu
Dah noma aiseee Kama vipi umeshaona umekula kwako Fanya mpango wawekee tu hicho cheti cha Avn mkuu kama umekidownload
 
Au Kama inakubali kwenda mbele bila attachment achana nayo utakuja uweke dilisha la marekebisho huwa wanatoa siku za kurekebisa Kama utakua ushalipia cheti
Duuh Ahsante mkuu.. Isha kula kwangu maana chuoni sijakomboa cheti nadaiwa lakini nimeverify Nacte Kumbe chuo walipeleka taarifa zangu
 
Samahan ndug zangu,naomba kuuliza kwa waliotoka diploma mwaka huu,kwenye kuomba mkopo inahitajika na AVN au n matokeo tu,,,,afu pia naomb kuuliza kwenye kuomba AVN unaweka matokeo ya mwaka wa mwisho au miaka yote
 
Mkopo hawataki avn wanataka cheti cha Diploma tu afu kuomba Avn hakuna sehemu ya kuwekaa matokeo matokeo Yako yalishatumwa na chuo wewe ni kujaza taarifa zako kwa ukamlifu tu unapatiwa avn
 
Mkopo hawataki avn wanataka cheti cha Diploma tu afu kuomba Avn hakuna sehemu ya kuwekaa matokeo matokeo Yako yalishatumwa na chuo wewe ni kujaza taarifa zako kwa ukamlifu tu unapatiwa avn
Avn ndio nini?
 
wakuu niko nje ya mada naomba kuuliza mwaka jana diploma wa IT na uhandisi walipewa nafasi ya kuomba mkopo mwaka huu vp wanaruhusu?
 
Mkopo hawataki avn wanataka cheti cha Diploma tu afu kuomba Avn hakuna sehemu ya kuwekaa matokeo matokeo Yako yalishatumwa na chuo wewe ni kujaza taarifa zako kwa ukamlifu tu unapatiwa avn
Ndugu unaweza nijuza jinsi ya kuandika reg number za cert na dip chuo cha cbe maana kila nikiweka zinaanzia na 01 na 02 zinakataa
 
Ndugu unaweza nijuza jinsi ya kuandika reg number za cert na dip chuo cha cbe maana kila nikiweka zinaanzia na 01 na 02 zinakataa
Registration number ya chuo ni Ile Ile namba Yako ya form four mzee ila unaanza na NS Mfano NS1234/0123/2015
 
Registration number ya chuo ni Ile Ile namba Yako ya form four mzee ila unaanza na NS Mfano NS1234/0123/2015
Hapo sijakuelewa mkuu, mfano reg number ya certificate na diploma tunarudia kuweka namba ya form four au unamaana gani?
 
Kama Hauna cheti utakwama kwenye usajili wa chuo chuo watakuomba uje na vyeti vyako vyote original kwa ajili ya uhakiki ndipo usajiliwe, AVN ni awards verification number hiki ni kama cheti chenye GPA yake ambayo ni gpa ya mwaka wa mwisho wa diploma NTA Level 6 huwezi tumia AVN mbadala wa cheti , AVN Hutumika kuhakiki kwamba kweli umekuwa Awarded
 
tueleweshane kidogo mwaka wetu tuna maliza diploma na kuomba mkopo yan mkopo ss tuliombea matokeo ya semista one tu, then natukapata mkopo yani wao cha msingi upate adimision vyuoni tu, na kuhusu chet unaruhusiwa kuweka matokeo yako ya diploma kama huna cheti
 
Wanufaika wapya wa Mkopo zaidi ya elfu 20 HESLB 2022/2023 | Majina ya Waliopata Mkopo
Habari njema kwa waombaji wote wa mkopo wa HESLB, Allocation ya mkopo bechi ya kwanza sasa inapatikana mtandaoni kuangalia allocation ya mkopo Tembelea Tovuti ya HESLB ya Maombi ya Mikopo na Mfumo wa Usimamizi https://olas.heslb.go.tz/index.php/olas/Olas

Nifanye nini nikikosa mkopo kwenye bechi ya kwanza HESLB?
Kuwa mvumilivu na subiri kwa sababu bodi ya mkopo inatoa majina ya waombaji wa mkopo waliopata mkopo kwa Bechi. Bechi za majina ya waliopata mkopo ni nyingi wakati mwingine hufikia tano au sita

Je nikisubiri hadi bechi zote za majina zikatoka na ikiwa sioni jina langu, nifanye nini?
Bodi ya mikopo hufungua dirisha kwa waombaji kukata rufaa kwa hivyo ikiwa unajiona kuwa una hoja, unaweza kukata rufaa
Je, nifanye nini ikiwa sipati mkopo baada ya kukata rufaa?
  • Lipa ada ya masomo na chakula cha kujifadhili na gharama za malazi.
Naweza kuomba mkopo huku nikiendelea na masomo?

  • Ndio mwaka ujao bodi itafungua dirisha jipya la maombi
Maswali baadhi ambayo naweza kukupa msaada angalau wa majibu kuendena na uelewa wangu
Je, iwapo nilikatisha(disco) masomo nifanye nini ili niweze kupata mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) Soma hapa

Je, ni lazima nifuate taratibu gani ili nilipwe mkopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB)?

Ili bodi ifanye malipo, mnufaika lazima afuate taratibu hizi

1. Mfadhiliwa lazima ajiandikishe kikamilifu katika taasisi ya elimu ya Juu, vinginevyo itamfanya akose sifa ya kupokea fedha hizo.

2. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) lazima ipokee maelezo ya ziada ya wanufaika. Jukumu la kutuma taarifa hizo ni la taasisi ambayo wamekubali Wanufaika na kuwasajili kikamilifu.

Nyongeza:

iwapo mnufaika wa mkopo atajiandikisha katika taasisi ya elimu ya juu ambayo ni tofauti na ile ambayo TCU ilipeleka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), mnufaika hatapokea fedha za mkopo hadi aombe kupangiwa upya au Kuhamishiwa mkopo.

Ikiwa mnufaika atabadilisha programu yake aliyoichagua awali, kiasi cha mkopo wake hakitabadilika hadi aombe kutengewa tena.

Mwisho, bodi ya mikopo Huendelea kufuatilia maendeleo ya mnufaika katika Vyuo vya Elimu ya Juu mara kwa mara ili kufanya uamuzi wa malipo.

Recomended Posts

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom