Umuhimu na uzito wa taarifa za kilimo nchini Tanzania

Bwana Mpanzi

Senior Member
Jun 28, 2019
180
165
Moja ya mambo yanachanganya na kuvuruga watu hasa wakulima nchini Tanzania ni taarifa yaani mnyororo wote umeathiriwa hapa na upungufu wa vyanzo vya taarifa rasmi au taarifa zisizo rasmi ambazo zinaathiri na kufanya kilimo kichukiwe na wanaolima au kuishi kwa kutegemea kilimo katika maisha yao.

Ukizungumza KILIMO kuna watu hawaelewi na hawakuelewi kutokana na bahati nasibu zilizowavuruga waliowahi kuwaona na kuna waliofilisika kabisa au kufa kutokana na kilimo tu.

Kuna kundi kubwa Ambalo limetoa maisha yao na kusema kwetu kilimo ni kila kitu ila wanaishi kwa uzoefu na sio utaalamu na taarifa kwao ni 35-50% ila kuna unafuu Wameuona na ndio maana bado wamebakia na wanaendelea kuwekeza katika sekta hii ambayo ni mama kwa nchi yetu.

HIVI KWANINI KILA TAJIRI AU ALOFANIKIWA KATIKA KUNDI FULANI LA MAISHA ANALIMA AU ANATAMANI KULIMA?

Changamoto za kilimo ni magonjwa,wadudu,wafanyakazi,mabadiliko ya tabia ya nchi na soko ila vyote huenda sambamba na taarifa,sasa je,mamlaka ndio zilaumiwe au wakulima?

Ukitaka kuwekeza ni lazima utafute taarifa katika vyanzo vinavyoeleweka,je,watu wanazingatia hilo au hatujifunzi kwa makosa ya kila siku?

Sasa kufikia tija walau tuone taarifa ambazo tunazihitaji ili kulinda au kujaribu kutafuta tija katika kilimo:
Soko: Hii ni taarifa ambayo ni elekezi ya kile unachotaka kwenda kukifanya shambani.

Hapa kuna uchaguzi wa eneo au kama umechagua masuala ya matunzo na Mwongozo wa shamba lazima uwe nao yaani hapa tugawanye namna mbili.

1. Mazao ya muda mrefu (Perennial crops) utahitaji ujue huo mwaka walau soko limekaaje hapa vyanzo vitatofautiana kuna wizara, bodi na vyombo mbalimbali kisha uandaaji wa shamba katika kulifufua kama haulilimi kipindi chote, unatakiwa ujue taarifa za soko ili utoe gharama za kuendeshea shamba katika msimu nzima mfano korosho, parachichi, kahawa, kakao na kadhalika hii itakusaidia baadae uaiangukie pua sana na hii hapa kuna muda utahitaji timing ili usifeli sana aidha sokoni au shamba, taarifa za magonjwa ya mlipuko kama mnyauko au inabidi ujue ili uandae bajeti mapema nk.

2. Mazao ya muda mfupi kama yale ya bustani unahitaji uwe na taarifa za kisoko, aina gani ni bora shambani na sokoni iko vizuri,msimu nzuri wa kulima,msimu nzuri wa soko,wadudu waharibifu na magonjwa ukishapata hivi itakusaidia baadae kwanza kwa kuandaa bajeti mapema na kuandaa ramani yote vizuri kabisa na miongozo.

Hali ya hewa: huwa hatuna kawaida ya kuwafuatilia watu wa TMA ila kwa ushauri kama unataka uwe una miongozo bora bhas uwe karibu na watu wa hali ya hewa nadhani kila wilaya wana vituo wao watakupa muongozo nini usikifanye na nini ukifanye na kuna uhusiano wa hali ya hewa na milipuko ya wadudu au magonjwa kwa hivyo tija utaipata pamoja na kuunganisha na mawazo yao na mambo ya bajeti mfano suala la kilimo cha umwagiliaji kinakuwa na mtazamo sana ila ukifahamu ratiba za mvua inakusaidia ili kupunguza gharama au katika kuvuna maji.

Taarifa za magonjwa,mbolea na wadudu waharibifu, kila kukicha aidha ofisi za kanda au bodi au wizara imehusika kutoa matamko ya taadhari ila kiukweli kuna muda wengi huwa hawayafuatilii sasa imekuwa tatizo sugu na imeathiri kabisa mzunguko nzima wa kilimo na kufanya watu waendelee kupata hasara, kuna matumizi hatarishi ya viuatirifu nayo huwa yanasahaulika na kufanya wakulima wawe na wakati mgumu (TPRI) wanafanya sana na kuorodhesha matumizi ya viuatirifu fulani haitakiwi kutumia pia mbolea limesahaulika ila taarifa zake ukitoa kupima udongo kila mwaka na suala la matumizi linahitaji taarifa kwanza ya bei na pili ya matumizi,tukizingatia hapa itatufaa sana kuelekea kwenye utija.

Taarifa za bodi na wanunuzi: kila mwaka kuna maelekezo aidha ya madaraja au namna ya ununuzi utafanyika na hii inachangiwa na aina ya kilimo mfano hai na hiki cha matumizi ya kemikali ambacho kimeathiri sana upande wa pili,kwa ufupi bei zake zinaathiri kila aina so ni vyema kuwa na taarifa kuelewa masharti ya bodi na wanunuzi katika mwaka husika.

Mtangi ( Bwana Mpanzi),
Bwana shamba wa kijiji,
0714600575/0620598113,
Morogoro.
 
Mkuu unatoa vitu konki sana. Ukitaka kufanikiwa kwenye kilimo hapa tz unatakiwa ujibebe mwenyewe kwa kila kitu ondoa kabisa neno serikali kichwani
 
HABARI wakuu

SHAMBA+ ni mtandao unaotumia App, Whatsapp channel na SMS utakaokutanisha wadau wote wa kilimo ie Wakulima, Bwana shamba, wauzaji pembejeo na mbegu na madawa, na masoko ya bidhaa za kilimo. Kazi/dhumuni la huu mtandao ni : (i) Ushauri wa kilimo kutoka kwa agronomist - NI BURE kama unatumia WHATSAPP au APP, kama ni SMS utalipia (ii) Maswali na majibu kati ya mkulima, Agronomist, wauzaji pembejeo - NI BURE kama unatumia WHATSAPP au APP, kama ni SMS utalipia (iii) Agronomist kuweza kuona maduka ya pembejeo/mbegu, wakulima mbalimbali na Agronomists wenzao wa mikoa mbalimbali na kuweza kuwasiliana na kujitangaza - NI BURE ila ni kwa kutumia APP NA WHATSAPP tu (iv) Kuona masoko na kuwasiliana na wanunuzi wa mazao - NI BURE ila ni kwa kutumia APP NA WHATSAPP tu
 
habari wakuu....?
nimerahisisha kwa sasa unaweza kuingia kwenye hizo link ukajibu maswali ya survey kirahisi...

hii ni maalum kwaajili ya wakulima

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom