Umuhimu na faida ya kula matunda na mboga majani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu na faida ya kula matunda na mboga majani

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  APPLES
  Protects your heart, prevents constipation, Blocks diarrhea, Improves lung capacity Cushions joints  APRICOTS Combats cancer, Controls blood pressure ,Saves your eyesight ,Shields against Alzheimer's ,Slows aging process  ARTICHOKES Aids digestion, Lowers cholesterol, Protects your heart, Stabilizes blood sugar Guards against liver disease  AVOCADOS
  Battles diabetes, Lowers cholesterol, Helps stops strokes, Controls blood pressure Smoothes skin  BANANA Protects your heart, Quiets a cough, Strengthens bones, Controls blood pressure, Blocks diarrhea  BEANS Prevents constipation, Helps hemorrhoids, Lowers cholesterol, Combats cancer, Stabilizes blood sugar  BEETS Controls blood pressure, Combats cancer, Strengthens bones, Protects your heart, Aids weight loss  BLUEBERRIES Combats cancer, Protects your heart, Stabilizes blood sugar, Boosts memory , Prevents constipation  BROCCOLI Strengthens bones, Saves eyesight, Combats cancer, Protects your heart, Controls blood pressure  CABBAGE
  Combats cancer, Prevents constipation, Promotes weight loss, Protects your heart, Helps hemorrhoids  CANTALOUPE Saves eyesight, Controls blood pressure, Lowers cholesterol, Combats cancer Supports immune system  CARROTS Saves eyesight, Protects your heart, Prevents constipation, Combats cancer, Promotes weight loss
  Baada ya utambulisho wa umuhimu na faida ya kula matunda na mboga kwani kila mboga na kila tunda vina nafasi tofauti ya kujenga na kulinda mwili. Watoto wengi wanasumbua sana kwenye kula hasa mboga majani asilimia kubwa sio wapenzi angalu upande wa matunda watoto wengi hupenda matunda lakini kwa kuchagua sio matunda yote watapenda kula tabia hii hujitokeza kwa kila mtoto hakuna aliekamilika nakumbuka hata mimi nilipokua mtoto nilikua nasumbua sana kula kiasi ikapelekea kua na afya dhaifu wakati wa kukua kwangu mpaka nilipobadili tabia na kuanza kula bila ya kufatiliwa.

  Unaweza badilisha tabia ya mtoto wako au mtu yeyote unaeishi nae nyumba moja asiyependa kula mboga majani au matunda kwa kubadilisha muonekano wa chakula hicho au tunda hilo kwa kulinakshi kwa mtindo wowote ule ilimradi kionekane kitu tofauti na kinachovutia hii itakua njia rahisi sana kumvutia mtoto au mkubwa chakula kizuri au upambaji wa chakula sio mpaka hotelini hata nyumbani unaweza fanya sanaa hii na wala haiitaji muda mrefu wa maandalizi muonekano bora wa chakula hutia hamasa kwa mlaji leo tutaangalia utengenezaji wa salad na kuipamba na uandaaji wa mboga ktk muonekano wa kuvutia upande wa kuchonga matunda tutaangalia wakati ujao fata maelezo jinsi ya kutengeneza salad yenye mchanganyiko wa mboga mboga hapo chini.


  [​IMG]  Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usalama sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni mahindi mabichi ya njano kabla huifadhiwa katika kopo tayari kwa matumizi, karoti iliyokwaruzwa, Lime stone lettuce, chicory, Radish iliyokwaruzwa, zucchin iliyokwaruzwa, rollo nyekundu, rollo ya kijani, matango yaliyokatwa, celeriac salad, curly endive, chicory nyekundu.  [​IMG]


  Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe  Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara nusu sahani tu kama mduara wa nusu mwezi kati kati acha nafasi kiasi.  Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chini utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.  Kisha liweke juu ya zile mboga mboga pembei yake kata kipande cha tikiti maji rangi yeyote ile kama ni la kijani, jekundu au rangi ya chungwa pamba kama invyoonekana katika picha.  Kisha kata slice nyembamba ya chungwa katikati yake weka tunda lolote dogo la mviringo kama zabibu au strawbery chomeka toothpick ili ishikilie chungwa juu ya tikiti maji.  Salad hii unaweza mwagia dresing yeyote ile mfano italian dressing, french dressing au siki na chumvi inatosha salad hii unaweza kula na kipande cha kuku, samaki wakuchemsha au wa kukaanga na unakua umekula mlo safi kabisa bila stach kwa watu wanaofanya dayati hapa ni mahala pake mvuto na muonekano wa sahani utamfanya mlaji avutie hata kama si mpenzi wa mboga na matunda.  [​IMG]  Hili ni jokofu la kutunzia mchanganyiko wa mboga katika nyuzi joto 4 hadi 5 tu kwa hali ya usafi sana kwa manufaa na afya ya mlaji tukianzia juu kushoto ni nanasi iliyopikwa katika sukari, embe mafuta, cappers, vitunguu vidogo vya kopo, chopped chives, chopped onion, olives nyeusi, asparagus, matango machanga yaliyosindikwa, olives zakijani, Nyanya  [​IMG]


  Katika sahani yako anza kupanga mboga ambazo zimekatwakatwa ambazo ni karoti, matango, mahindi machanga ya njano, celeriac salad na radish nyeupe.  Chota kidogo kidogo kila moja panga kwa mtindo wa duara kuzunguka sahani yote katikati acha nafasi.  Baada ya hapo chukua jani la salad moja moja toka kila aina ya salad pagange sambamba majani hayo kisha zungusha yabane kama unataka kuyafunga kamba kisha kata kiasi upande wa chi utakua umepata kitako safi utakua umetengeneza kama uwa rozi.  Kisha liweke pembeni ya zile mboga mboga katikati ya sahani unaweza weka mchanganyiko wowote ule wa nyama ya kuku, ngo'mbe, samaki au sausage iliyochemshwa ikapoa.  Kata saizi ya kuweza kuingia mdomoni kisha changanya na vitunguu vilivyochopiwa safi pamoja chives.  Mchanganyiko huo unaweza malizia na chaguo lako la dresing yeyote uipendayo kisha unamwagia kati kati ya sahani mwisho kata nyanya kipande weka pamoja na tango dogo la kopo na olive moja ya kijani na moja nyeusi kwa kupamba salad yako.

  [​IMG]


  Kwa upande wa mlo kamili baada ya kupika chakula chako kikaiva kama ni ugali au wali  Chemsha njegere zisiive sana  Kisha kata vitunguu vidogo sana kaanga katika siagi dakika 1 tu  Kisha weka hizo njegere zilizoiva katika sufuria kwa dk 2 usiasahau chumvi kisha zitoe  Chukua nyanya nzuri ngumu iliyokwisha iva kata nusu pia kata kidogo katika kitako ili iweze kukaa katika sahaki  Kisha toa mbegu zote katikati ya nyanya tumia kijiko kuchota na jaza zile njegere kwanye nyanya  Kisha save nyanya hiyo yenye njegere kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku.  Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.

  [​IMG]


  Sasa hapa ndio utawakamata kweli kweli wasiopenda kula mboga za majani,  Chukua maharage mabichi yachemshe kiasi yasiive sana yabaki na rangi yake nzuri ya kijani  Kisha unachukua bacon slice zipo aina mbili zipo bacon za nguruwe na bacon za ng'ombe chaguo ni lako mlaji.  Kisha chukua maharage hesabu kumi na tano kisha zungushia bacon katika maharage hayo weka katika ubao wa kukatia kata ncha za mwisho ili kuweka usawa na muonekano mzuri zaidi.  Ukishamaliza weka kikaango kwenye jiko la moto wa wastani tu weka mafuta kiasi katika kikaango yakishapata moto weka maharage yaliyozungushiwa bacon kaanga kiasi tu ili ile bacona ikauke.  Kisha toa tayari kwa chakula pia sevu kama mboga majani itakayo ambatana na chakula chako kama ni cha mchana au cha usiku. Muonekano na mchanganyiko wa rangi inakua kivutio kizuri sana kwa mtu asiependa kula mboga majani.  KWA KUFATILIA MAELEZO HAYA YOTE UTAKUA UMEFANIKIWA KUMREKEBISHA KAMA NI MUME AU MTOTO ASIEPENDA KULA MBOGA ZA MAJANI AU MATUNDA IKIWA UMESHAFAHAMU PIA UMUHIMU WA VYAKULA HIVYO KWA BINADAMU  [​IMG]


  Nashukuru sana mdau aliezungumzia upatikanaji wa bacon ya ng'ombe, nikweli kwa ulaya kupata bacon ya ng'ombe ni adimu sana ila hapa kwetu Tanzania zinapatikana kwa wingi ukienda katika supermaket kubwa au maduka makubwa ya nyama utapata.  Endapo umekosa basi chukua mboga hiyo hapo juu inaitwa leeks kata jani lake lisafishe vizuri kisha zungushia vizuri maharage yako hatua za upishi ni zile zile unaikaanga kidogo tu itaiva na italeta harufu nzuri sana kwahiyo kwa asie kula kabisa nyama atakua nae kafaidika. CULINARY CHAMBER Tanzanian Executive Chef Issa Kapande: TAMBUA UMUHIMU NA FAIDA YA KULA MATUNDA NA MBOGA MAJANI


   
 2. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu kwa Elimu.
   
 3. S

  Smarty JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  we jamaaa!!!!!! M.Mungu akujaalie Umri mrefu, afya njema, na akufanyie wepesi katika mambo yako ili tuzi kunufaika na elimu hii.. asante sana MM
   
 4. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante,
  je una vitabu au kitabu ulichotoa kinachohusiana na mambo ya chakula?, au tiba mbadala?,
  na kama jibu ni ndiyo, je ki/vinapatikana duka gani la vitabu kwa hapa dar es salaam ?.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @nnunu Nina Mpango kufanya hivyo lakini nikiwa teyari nitakufahamisha.
   
 6. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  asante, mungu akusaidie kutimiza mipango yako,
  ili hivyo vitabu viwe msaada kwetu na vizazi vyetu vijavyo.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Food for thought
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  APRICOTS


  Also known botanically as Prunus armeniaca,or "Armenian plum", this well-known fruit is native to the Asian regions of Himalaya, China, Armenia and is currently grown in several regions with climates ranging from sub-tropical to temperate and mediterranean.
  [​IMG]
  A sliced apricot showing the "stone"
  Apricot trees are very prolific: they can reach 12-15 feet in height and yield fruit for up to 20-25 years.These trees grow with ovate leaves, about 5-10 cm in diameter and length, with a pointy tip.Flowers have light pink petals, and only reach a size of about 3-4 cm. Apricot trees produce a fruit similar to peaches, with a yellow, pale color that becomes deep orange when ripe, and it often becomes red on the region most exposed to sunlight. Apricots also contain a single seed, surrounded by a hard, woody shell called "stone".The inner seed can be eaten and has a taste very similar to almonds, but it contains small quantities of cyanide and should therefore be consumed with caution: it can lead to cyanide poisoning.Nowadays, apricots are cultivated in several countries with different climates, with the most important being Turkey, Iran, Italy, Pakistan and Greece, but several other countries contribute heavily to apricot production.In the USA, most apricots are produced in California (about 95% of total output), while in Australia apricots are confined to the southern regions.
   
 9. Dachr

  Dachr Senior Member

  #9
  Apr 21, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni matumaini yangu litakuwa ni darasa lenye manufaa.
   
 10. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mkubwa nimeikubali ila michanganyiko mingine ni mingeni kwetu tumechazoea mlenda
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @ummu kulthum Jaribu kutumia tu itakusaidia kiafya yako na mwili kuwa mzuri huko uliko matunda yote ninafikiri yapo au siyo bibie?
   
 12. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Thanks Mkuu
  Ila hatuna maelezo ya matunda pori yetu?
  Kwetu kuna mantonga, mbula (wachaga mnisamehe), ntarali, mabungo etc!

  Kwa mboga tuna mlenda, majani ya kunde, mnafu, tembele n.k

  Tungejua nutrion values za hivo vitu ambavyo ni endemic kwa maeneo yetu tungeweza kupromote; kuliko kutegemea bidhaa za nje ambazo zapatikana masupermarket tu!
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @Kaunga Mkuu kama ni matunda pori yanaliwa basi yatakuwa na Faida kwa binadamu na mboga pia zina faida nyingi katika mwili wa binadamu itabidi tuwe tunakula matunda yetu na mboga kwa wingi ili tuweze kuimarisha afya za mwili wetu asante kwa ushauri wako.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ubarikiwe mno.
   
 15. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante kwa elimu kaka.
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mzizi mkuu tunashukru sana maana mbonga mbonga tunazipata na nirahisi hata kupanda na upatiakanaji wake si mungumu
   
 17. rom

  rom Senior Member

  #17
  Apr 24, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  asante sana , pia nimeona vyakula vingi hapa baejti yake si kubwa ... hivyo hat sisi wa mtaani tunaweza kumudu kusonga na maisha ya kila siku... asante sana Mungu akupe umri mrefu na uendelee kutuelimisha.
   
Loading...