Umuhimu gani wa kuvaa designer name kama kuvaa ni Kushiro maingo?

Unajua hela ikiongezeka unataka uwe tofauti na wengine na uonje radha tofauti na wengine
 
Weusi wengi wanapenda sana kuvaa vizuri unakuta mtu ana suit ya $500 tena ni mbili au tatu lakini hana $500 kwenye accout. Kuna wakati ninawaza inaweza kuwa psychology effects za utumwa
Aysee siwezi nunua suti moja kwa $500 mana kwa pesa hiyo nashona suti 3 kali kwa Muha, piar 3 za leather dressing shoes kwa Urio na pesa ya bia inabaki
 
Aysee siwezi nunua suti moja kwa $500 mana kwa pesa hiyo nashona suti 3 kali kwa Muha, piar 3 za leather dressing shoes kwa Urio na pesa ya bia inabaki
I know, mimi kwenye harusi ya rafiki wa karibu ninaweza kujipinda gauni la $500 lakini hiyo inamaana nilipanga mwaka mzima.
 
Kuna watu huvutiwa na vitu kwa sababu tu ni vya gharama kubwa. Yani ndivyo walivyo tu. Napendelea kitu kizuri chenye gharama nafuu. Siwezi nunua simu ya laki tano ambayo inafanya kazi sawa na simu ya laki mbili kisa tu ya laki tano ni Samsung na ya laki mbili ni tecno

Bado ujapata pesa extra ukipata tofauti utaiyona
 
Unakuta shati la Gucci linauzwa shillingi laki tano za ki- bongo na wakati mashati mazuri ya Egyptian cotton yanauzwa Tshillings 50,000 lakini kuna watu Wataona ufahari kumiliki shati la Gucci kabatini mwake.
Kununua designer gear ni ufahari au hulka tu ya mtu?
Fuatilia maisha yako kila mtu alizaliwa muda wake ,kuna wengine walipanga na wengine wa bahati mbaya.Hivyo ishu za uchafu ,usafi kila mtu na mawazo yake na familia yake.Wewe unatafuta pesa usaidie wazazi wenzako pesa ni zake binafsi hana majukumu hayo ya wazazi.Anaweza amua mshahara wake wote anunue kandambili hana shida wala mtu wa kumtegemea.Usifuate ya watu
 
brands hizo zina raha yake,hata quality inakua iko poa sana...hata upate copy yake still quality inakua different na brands uchwara...

Kweli kabisa mimi nanunua tu brand za kati handbag kama Michael kors unabeba mpaka unachoka unagawa... sasa katizame copy yake mwezi limeanza kubanduka
 
Hahaaaaa

Siko peke yangu ambao hatupendi kuvaa nguo zenye maandishi makubwa.

Kwa mfano, kuna yale mashati ya Burberry yenye zile patterns kwenye shati zima.

Mimi huwezi kunikuta nimevaa nguo ya hivyo.

Lakini pia nina mashati kadhaa ya Burberry ambayo hayana kabisa hizo patterns na yana kile kinembo chao kidogo tu kifuani.

That's just my style. Sipo peke yangu kwenye hilo.
Mjanja yoyote hawezi kuvaa 'bango'....
 
Kuna watu wanaishi kwa maigizo. Anataka vazi kulingana na bei yake bila kujali uimara na unadhifu. Mwingine atataka vazi flani kisa kuna mtu fulani maarufu kavaa la aina ile. Ni kweli lakini kuna profession zinahitaji mavazi ya kipekee na yenye ubunifu wa hali ya juu kama vile waigizaji, wanamitindo na wanamuziki. lakini utakuta mtu labda ni mwalimu au mwanasiasa au ni mfanyabiashara basi ana complicate kwenye mavazi hadi anasahau kufuatilia mambo mengine, inafikia anasahau hadi majukumu yake.
Ila mimi sijui nikoje, sichaguagi kabisa mitindo wala siishobokei. ninachojali ni nguo safi, za heshima na zinazonisetiri. Amini usiamini...... hata nikikutana na mtu huwa siangalii kavaa namna gani au kavaa mtindo gani, labda awe uchi au nguo zake chafu ndio nitagundua. vinginevyo hata akiniuliza baada ya kuachana alikuwa kavaa nguo gani sitakumbuka.
Ni Uchumi tu unaobana otherwise kila mtu angependa apate products za hizo brand kubwa kama Gucci, varsace nk ,napinga kabisa mtu akisema yeye hajali jina ili mradi hiyo product iko poa,ktk watu 100 inawezekana wakapatikana labda 2 yaani wako njema lkn and world top brands haziwasumbui Mara nyingi huitaji wa kitu cha high quality inategemea na status ya kipindi hicho hii nailinganisha na someone billionaire anaenda kupanga Nyumba Mbagala eti kisa ina kila kitu almost Sawa na zile zilizopo Mbezi Beach!Haina ubishi hizi products za top designers au hizi top brands zinakupa confidence pamoja na respect mbele za watu.
 
Ushawahi kumuona Bill Gates, Mark Zuckerberg au Warren Buffet kavaa nguo zenye maandishi makubwa ya "Gucci" au lebo kama hizo?
Hakuna Nguo /brands original za Gucci, Polo ,Versace au labda Van Hussein zina maandishi makubwa ya kuzitambulisha sana sana ukizigusa Dukani bei yake ndio itakutambulisha, ukiona za hivyo ni copy za kichina, hao celebrities ndio wako very sensitive na brands tena wana mpk special order from top world designers.
 
Hakuna Nguo /brands original za Gucci, Polo ,Versace au labda Van Hussein zina maandishi makubwa ya kuzitambulisha sana sana ukizigusa Dukani bei yake ndio itakutambulisha, ukiona za hivyo ni copy za kichina, hao celebrities ndio wako very sensitive na brands tena wana mpk special order from top world designers.
Abraham Mengi alikuwa na fulana nyeusi ina maandishi makubwa ya gold "Dolce & Gabbana".

Abraham simtu wa kuvaa kitu feki.

Unajiridhishaje kwamba hakuna brand originals hizo zenye majina makubwa? Umetembelea maduka mangapi ambayo hayauzi vitu feki ukahesabu nguo zao zote na kuona hakuna zenye majina hayo makubwa?

Hivi Van Huisen nayo ni luxury brand? Mbona mashati ya kila siku kwendea kazini hayo na bei zake wala si za ajabu. Ukiyavizia outlet mpaka $12 unapata.
 
Back
Top Bottom