Umuhimu gani wa kuvaa designer name kama kuvaa ni Kushiro maingo?

Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Kuna watu wanaishi kwa maigizo. Anataka vazi kulingana na bei yake bila kujali uimara na unadhifu. Mwingine atataka vazi flani kisa kuna mtu fulani maarufu kavaa la aina ile. Ni kweli lakini kuna profession zinahitaji mavazi ya kipekee na yenye ubunifu wa hali ya juu kama vile waigizaji, wanamitindo na wanamuziki. lakini utakuta mtu labda ni mwalimu au mwanasiasa au ni mfanyabiashara basi ana complicate kwenye mavazi hadi anasahau kufuatilia mambo mengine, inafikia anasahau hadi majukumu yake.
Ila mimi sijui nikoje, sichaguagi kabisa mitindo wala siishobokei. ninachojali ni nguo safi, za heshima na zinazonisetiri. Amini usiamini...... hata nikikutana na mtu huwa siangalii kavaa namna gani au kavaa mtindo gani, labda awe uchi au nguo zake chafu ndio nitagundua. vinginevyo hata akiniuliza baada ya kuachana alikuwa kavaa nguo gani sitakumbuka.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,675

Weusi wengi wanapenda sana kuvaa vizuri unakuta mtu ana suit ya $500 tena ni mbili au tatu lakini hana $500 kwenye accout. Kuna wakati ninawaza inaweza kuwa psychology effects za utumwa
 
SHAMAC

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
1,345
2,000
hata nikikutana na mtu huwa siangalii kavaa namna gani au kavaa mtindo gani, labda awe uchi au nguo zake chafu ndio nitagundua. vinginevyo hata akiniuliza baada ya kuachana alikuwa kavaa nguo gani sitakumbuka.

Sio kwa wanawake Mkuu.,, Wanawake wana kasumba ya kachunguza sana mavazi hata kama ulikua na kadoa kadogo kwenye shati atakaona...!! Kwenye hiyo sector wako vyema... Ila wanaume wengi tuko hivyo
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,934
2,000
Unakuta dhati la Gucci linauzwa shillingi laki tano za ki- bongo na wakati mashati mazuri ya Egyptian cotton yanauzwa Tshillings 50,000 lalakini kuna watu Watson a ufahari kumiliki shati la Gucci labatini mwake.
Kununua designer gear mi ufahari au hulks tu ya mtu?
Mahatma Gandhi aliuangusha Ufalme wa Uingereza kwa kueaongoza Wahindi wakatae kuvaa nguo za kigeni na kupenda kuvaa zao.

Binafsi moja ya kitu kinachoweza kunifanya nisinunue nguo ni kama ina m label mkubwa.

Nitajiona kama tangazo la biashara linalotembea.
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,934
2,000
Kuna watu wanaishi kwa maigizo. Anataka vazi kulingana na bei yake bila kujali uimara na unadhifu. Mwingine atataka vazi flani kisa kuna mtu fulani maarufu kavaa la aina ile. Ni kweli lakini kuna profession zinahitaji mavazi ya kipekee na yenye ubunifu wa hali ya juu kama vile waigizaji, wanamitindo na wanamuziki. lakini utakuta mtu labda ni mwalimu au mwanasiasa au ni mfanyabiashara basi ana complicate kwenye mavazi hadi anasahau kufuatilia mambo mengine, inafikia anasahau hadi majukumu yake.
Ila mimi sijui nikoje, sichaguagi kabisa mitindo wala siishobokei. ninachojali ni nguo safi, za heshima na zinazonisetiri. Amini usiamini...... hata nikikutana na mtu huwa siangalii kavaa namna gani au kavaa mtindo gani, labda awe uchi au nguo zake chafu ndio nitagundua. vinginevyo hata akiniuliza baada ya kuachana alikuwa kavaa nguo gani sitakumbuka.
Wanawapata sana hawa.

Nike wanatengeneza viatu vinauzwa mpaka $ 3,000 kwa sababu tu vimetengenezwa vichache.

Halafu Mchina anatengeneza copy anaviuza $50.

Ukiangalia mtu kavaa huwezi kujua nani kavaa vya Mchina na nani kavaa vya Nike.

Ujinga mtupu.

Lakini ndiyo maisha waliyochagua. Siwalaumu.

Wacheni waishi kivyao.

Inawezekana ni fursa ya biashara kwako pia.
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Wanawapata sana hawa.

Nike wanatengeneza viatu vinauzwa mpaka $ 3,000 kwa sababu tu vimetengenezwa vichache.

Halafu Mchina anatengeneza copy anaviuza $50.

Ukiangalia mtu kavaa huwezi kujua nani kavaa vya Mchina na nani kavaa vya Nike.

Ujinga mtupu.

Lakini ndiyo maisha waliyochagua. Siwalaumu.

Wacheni waishi kivyao.

Inawezekana ni fursa ya biashara kwako pia.
Wengine wapo kimaslahi hadi kwenye mavazi aisee
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Ushawahi kumuona Bill Gates, Mark Zuckerberg au Warren Buffet kavaa nguo zenye maandishi makubwa ya "Gucci" au lebo kama hizo?
Aaaa Wapi. Wale wanatupa simple zao tu na zinawato vizuri kuliko wale wanao complicate.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
49,881
2,000
Unakuta shati la Gucci linauzwa shillingi laki tano za ki- bongo na wakati mashati mazuri ya Egyptian cotton yanauzwa Tshillings 50,000 lakini kuna watu Wataona ufahari kumiliki shati la Gucci kabatini mwake.
Kununua designer gear ni ufahari au hulka tu ya mtu?
Good question
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
43,675
2,000
Wanawapata sana hawa.

Nike wanatengeneza viatu vinauzwa mpaka $ 3,000 kwa sababu tu vimetengenezwa vichache.

Halafu Mchina anatengeneza copy anaviuza $50.

Ukiangalia mtu kavaa huwezi kujua nani kavaa vya Mchina na nani kavaa vya Nike.

Ujinga mtupu.

Lakini ndiyo maisha waliyochagua. Siwalaumu.

Wacheni waishi kivyao.

Inawezekana ni fursa ya biashara kwako pia.
Nchi za magharibi sasa hivi wako macho sana na mizigo inayoingia kwao hizi fake products za mchina zinahatatisha uchumi
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
85,585
2,000
Sina tatizo kabisa na jinsi mtu aamuavyo kutumia pesa zake.

Matumizi ya pesa zake mimi hayanihusu kabisa.

Pesa ni zake na ana haki na uhuru wote wa kuzitumia atakavyo na apendavyo.

Kuna wengine wanapenda magari ya kifahari kama Rolls Royce na watanunua kila toleo.

Kuna wengine wanapenda Toyota Corolla na watanunua kila toleo.

Lakini yote hayo ni magari na yana uwezo wa kukutoa kutoka eneo A kwenda eneo B, C, D, na hata E.

Ni suala la mtazamo na mapenzi ya mtu.

Wewe kama unaona wenye kupenda kuvaa vitu vya anasa vya bei mbaya ni washamba au wenye kupenda kujionyesha na wenzio wanaweza kukuona wewe unayewaponda wanaopenda vitu hivyo vya anasa na bei mbaya unafanya hivyo kwa husda kwa sababu huna uwezo wa kuvinunua hivyo vitu na ili kujipa faraja unaona uwaponde kwa sababu kuwaponda huko kunakufanya ujisikie vizuri. Kuwaponda huko kunafidia ukosefu wako wa uwezo wa kuvinunua.

La msingi hapa ni kutambua tu kuwa watu tumetofautiana. Tuache watu waishi watakavyo na si kuhukumu hukumu kila mtu na kila jambo.

Mtu kuvaa nguo za anasa hakuathiri kwa namna yoyote ile maisha yangu [labda kama ninamwonea wivu na siwezi kuwa nacho alichonacho].

Zaidi ya hapo, live and let live.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom