Dogo Lao
Member
- Nov 2, 2011
- 94
- 38
Na ashukuriwe Mungu muumba mbingu na nchi, Ndg. zangu wana JF, Asalamualeykhum.
Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu, kwa rehema zake na wema wake hata tumeweza kuiona siku ya leo. Ndugu zangu, sote tunajua jinsi mchakato wa uchaguzi unavyokuwa mgumu. Siyo kwa wagombea tu, bali hata kwa wanaowaunga mkono. Pamoja na ushindani mkubwa uliojitokeza ktk uchaguzi wa mwaka huu, hatimaye Rais ametangazwa.
Kwani ni siri? Siyo siri, ni dhahiri kuwa CCM imeshinda kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi. Yaliyopo nyuma ya ushindi huo siyo kazi yangu kuyasema, ila yaliyoonekana yameonekana, na yaliyosikika kama uvumi yamesikika. Mwisho wa siku tunasema CCM imeshinda kwa kishindo kikuu, upinzani umekosa ridhaa kwa wananchi.
Sasa, miaka 5 ni dhamana ya Chama Cha Mapinduzi. Katika kipindi cha miaka 5 inayokuja ndipo tutajua, Upinzani ulikuwa una umuhimu wake ama haukuwa na umuhimu wowote.
Muda ni mwalimu mzuri.