Umri wa mwanamke kuolewa. Ukishapita huu anakuwa na wakati mgumu sana. Na muoaji uwe makini

Kwa mwanamke 30+ ni mtihani sana kwao linapokuja suala la ndao au hata watoto kama bado hajazaa...


Cc: mahondaw
 
Kuna umri flani ambao ndiyo hufaa sana kwa mwanamke kuolewa. Miaka 22-28 huu ni umri ambao wanawake wengi hudhani ni wakati mzuri kwao kuolewa na wanaume wengi hupenda kuoa wanawake walio katika umri huu huku wao wakiwa na miaka katika umri wa miaka kati ya 30-35.

Ifikapo miaka 30 wanawake wengi huwa katika wakati mgumu sana kimahusiano na wanaume wengi pia huwa hawako radhi kuwa na wanawake wa umri huu wakiamini tayari wameshakimbiliwa na utu uzima au uzee wanaamini kuwa katika umri huu mwanamke anakuwa ametumika sana, hii dhana haina uthibitisho.

Ingawa kiukweli wanawake wengi huwa na msongo wa mawazo na huomba sana katika kipindi hiki Mungu awasaidie waweze kupata waume ni kipindi ambacho mwanamke anapunguza hata zile sifa za mwanaume anayemtaka. Utamwona mwanamke ambaye yupo kwenye 30s hajaolewa namna ambavyo anahangaika ili apate mwanaume na wakati flani huwafanya wawe na hasira au kisirani.

Mwanamke katika umri huu anakuwa na wakati mgumu kwa kuwa inawezekana ameshahudhuria kwenye harusi nyingi za ndugu zake, rafiki zake na majirani. jamii inakuwa kama inamwangalia yeye kwa sasa ana uelekeo gani na kuna baadhi ya family huzuia mdogo asiolewe kabla dada hajaolewa hii huleta misuguano na migogoro au chuki katika family kuwa mdogo hawezi olewa kabla dada hajaolewa.

Sijafahamu kwanini lakini wazazi wengi na wataalamu wengi wanasisitiza kuwa mwanaume unapaswa umuoe mwanamke ambaye umemzidi kuanzia miaka 5-10. Wanasema hili huwa ni jambo zuri kwa kuwa mara nyngi wanawake huanza kukua kiakili na kimwili kuliko wanaume. So unapomuoa mwanamke ambaye mnalingana ujue obvious ameshakuzidi au unapomuoa mwanamke ambaye mmepishana naye mwaka 1-3 ni kama amekuzidi pia.

Katika hili napenda kuwashauri akina dada kuwa katika kipindi cha miaka 22-28 ndipo wanapoweza tengeneza tabia ya kuwa mke. Ndipo ambapo mwanaume anaweza mtizama mwanamke akaona huyu anafaa kuwa mke wake. So ni kipindi ambacho mwanamke anapaswa ajifunze tabia njema na aoekane mkomavu kwa maneno na matendo pia. Anapaswa achague nini cha kuongea na wakati gani. Pia matendo yake na mavazi ni vitu muhimu sana ili kumpata mume mwema.

Otherwise wanaume wataendelea kuwa na msichana wa namna hii kimahusiano ikifika kwenye kuoa wanaenda kuoa mwanamke mwingine na mwishowe akina dada wanabaki kuwalaani wanaume.
Ni kweli kabisa

Tatizo wakati mwingi sisi wanawake huwa tunadhani umri unatusubiri...kuna kile kipindi ambacho kila aina ya mwanaume anajitokeza na anaonesha interest ila mdada anaringa anatafuta mwenye pesa bila kujua yule asie na pesa mnaweza kuanza maisha na nmkatengeneza pesa kwa kushirikiana..

Wakati ambao yupo tayari kuolewa akuna serious guy anaejitokeza..wote. ni wapigaji tu halafu wanasepa

Hapo atainhia JF kuandika thread natafuta serious husband

Lakini pia kuna wengine wanakua kwenyw mahusiano serious tena kwa muda mrefu na wameweka expectations za ndoa ila mwanaume anakuja kumtenda mwishoni wakati ameshapiteza muda mrefu katika hayo mahusiano

Kuna wengine amekua kwenye mahusiano kumbe alie nae ni mume wa mtu na amekuja kugundua when its late

Kuna wengine wamekumbwa na mambo mengi mpaka wamekua wadangaji sasa muda unapofika wa kutaka kutulia hakuna anaejitokeza

Kuna wengine ni kwamba tu hajaata wa kumuoa na umri unaenda

Wanaume jitahidini kuoa basi na mjitahidi kuwa wakweli ili msiwapotezee muda hawa wadada


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamume anayetaka kuoa je umri mzuri wa kupishana kati ya mwanaume na mwanamke ni umri gani ili kuepusha kuitwa ameolewa na mzee
 
Back
Top Bottom