Umri wa mtu kuteuliwa kushika nafasi yoyote Serikalini uwe ni walau kuanzia miaka 35

Kwa nini liwe taifa la wendawazimu kuruhusu kila mtu kugombea bila kujali vyeti wala umri?

Kuweka vigezo vya umri na vyeti ni ubaguzi unaoashiria walioweka vigezo hivyo hawaamini uwezo wa wapiga kura kufanya maamuzi sahihi pale wanapopelekewa mgombea kijana asiye na vyeti na yule mzee mwenye vyeti. Kama ni kweli wapiga kura sisi hatuwezi kutanabahisha mgombea anayefaa mpaka Katiba ituchagulie, huyo msomi mzee anashindwa nini kuja kutushawishi tumchague?

Naamini wapiga kura ni watu wazima (miaka 18+) na ni wenye akili timamu, wenye uwezo wa kujua ni yupi mgombea sahihi wa kupewa kura.
Kwa mantiki hiyo unataka utuaminishe kuwa wanaohombea wasiwekewe sharti ya elimu wala umri. Alafu hapohapo wanaopiga kura wawe kuanzia miaka 18+..!? Hhahahhhaa sasa hizo zitakua hesabu za wapi bwa shee??

Tumebarikiwa akili na utashi kiasi ili maisha yetu yaende vizuri tuweze kupangilia mambo. Na ndio tukawekewa utaratibu kuwa kila jambo lina Wenye. Sasa hii wenye hii ndio hizo qualifications and qualities
 
Kuhusu sabaya na bashite ishu sio umri bali ushamba na kubebwa na magu
 
Shida ambayo nimegundua ni kwamba vyama vya siasa especially the goddamn CCM, wanachagua disciples wao kwa kutazama vijana viherehere na wajuaji na kuacha wenye hekima na utulivu wa akili.

Katika akili ya kawaida, huwezi kukuta mtu kama mimi nina hangaika na siasa kushindana na wengine kugombea nafasi ambazo kuzipata kuna kujuana kwingi na ili upate cheo basi ni ulambe miguu ya waliokutangulia au ukubali kudhalilika ndipo upite, mimi bado sijafikia kiwango hicho cha kujishusha.

But upande mwingine, wale wenye vipaji vya kweli vya uongozi, tusifunjike mioyo. Platforms zipo nyingi sana ukitoa majukwaa ya vyama vya siasa. Politics ni game pana sana na kama una madini ya kusaidia jamii yetu then nafasi ipo nje ya vyama vya siasa.
 
Hao kina Baahite na Sabaya ni zao tu la kupewa madaraka yanayowazidi umri.
Bashite tokea hata hajawa mkuu wa wilaya wala hata hajawa pale CCM kwenye UVCCM. Akiwa chuo cha ushirika kama waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi nilijua tu hapa hakuna kiongozi bali kuna mtu anae tafuta kuwa superstar kupitia vyeo vya kisiasa.
 
Kwa mantiki hiyo unataka utuaminishe kuwa wanao[g]ombea wasiwekewe sharti ya elimu wala umri. Alafu hapohapo wanaopiga kura wawe kuanzia miaka 18+
Ndio. Ni kwa vile hudhaniwa kwamba mtu yeyote asiyefikia umri wa miaka 18 ni mtoto asiye mtu mzima, na wala akili zake hazijatimia bado.

Sekunde anayotimiza umri wa miaka 18 shurti aweze kupata stahiki zote za haki na wajibu wa mtu mzima. Iweje tena tuanze kumuwekea mizengwe kwamba hiki au kile asigombee?
 
Miaka 35 bado ni kijana sana kichwani. Kina Malcom X, Martin Luther, Nyerere ni watu wenye vipaji maalum na hutokea mara chache wakaishi.

35 bado ana akili za kujirusha, anajiona mwepesi kimwili na kiakili, mfano ndio hawa kina Sabaya na Makonda.
 
Naona wakati umefika tuweke kigezo cha umri kwa watu wanaoteeuliwa kushika nafasi au madaraka makubwa serikalini na katika Utumishi wa umma.

Katika nchi yetu, uteuzi hufanywa zaidi na Raisi na wateule wa Raisi wote hupewa dhamana au madaraka makubwa na hivyo kuna uwezekano baadhi hupewa madaraka makubwa kuzidi umri wao( wanakuwa hawajakomaa).

Vijana wengi wa kitanzania chini ya miaka 35 wanakuwa bado wanasumbuliwa na ujana na hivyo inakuwa rahisi kulewa madraka na pia ni rahisi zaidi kwa watawala wabovu kuwatu vijana kwa mambo yaliyo kinyume na maadili yetu na hata utu wa mwanadamu.

Mbali na kusumbuliwa na ujana( kupsndisha mabega, n.k) ni wazi pia watawala huwachukulia vijana wanaowapa madaraka kama watoto wao wa kuwazaa hivyo inakuwa rahisi kuwatumia kwa mambo ya hovyo.

Ukiacha katika majeshi ambako amri ndio hutawala hivyo inakuwa rahisi hata kuwatumia watu wenye umri mkubwa kufanya mambo ambayo ni kinyume na Sheria za nchi na maadili ya kitabzania, nii vigumu kwa watawala kuwatumia wateule wenye umri sawa na wao kutenda mambo ya hovyo kama wanavyoweza kuwaagiza au kuwatumia vijana waliowapa madaraka.

Hivyo, japo si vijana wote wanakosa busara za uongozi na wanaoweza kutumika vibaya, napendekeza umri wa wateule wote wa Raisi nchi hii kuanzia walau miaka 35 na ikibidi zaidi ya hapo.

Najua wako vijana wanafanya vizuri tu katika uongozi, ila ni bora tuweke hiki kigezo ili kuondoa au kupunguza risk ya kuwa na vijana wanaotumika vibaya na watawala au kuwa na vijana ambao bado hawajakomaa kupewa madaraka makubwa ya kuteuliwa na Raisi au Mamlaka nyingine za uteuzi.

Vijana wengi wa kitanzania wa leo hii sio sawa na wale wa miaka ya nyuma walioweza kupewa madaraka makubwa na wasiwaangushe waliowapa madaraka.

Kuhusu viongozi wa kuchaguliwa, hiyo ni agenda nyingine ingawa bado agenda hiyo inaweza ku-fit hata katika hii mad na hivyo hapa sitaiongelea.

Nawasilisha.
Hapa unamuogelea Makonda, Sabaya au Ally Hapi au wote

Vija a wametuangusha sana yaani wamefeli mbaya
 
Mwl Nyerere kawa Rais akiwa na miaka 38 lakini waliokuwepo wanasema hakuwai kufanya matendo ya kipumbavu na kihuni, Dr Salimu sijui aliteuliwa akiwa na miaka 22 kuwa Waziri lakini hakufanya upumbavu na uhuni, hizi ni tabia za watu, mwendazake alikuwa muuaji kwani alikuwa under 35?
Duuuh nyerere aliula at 38 ni presidaa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom