Ni umri gani mtoto anapaswa kutembea?

The Dude

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
1,029
453
Hapa kuna mtoto katimiza mwaka mmoja jana.cha ajabu hajaanza kutembea.Anatambaa tu na kujivuta kwa kushikilia vitu na ukuta.Watu wengine wanadai km hadi sasa hajatembea basi hatatembea kamwe.

Kwani umri wa kutembea mtoto ni upi exactly,na nini husababisha wengine kuchelewa? Kwa anayechelewa kuna tiba yoyote?Na je kuna risk ya huyu mtoto kutotembea kabisa ie. Kuwa mlemavu?
 
anaewahi sana ni kuanzia miezi tisa japo sio wengi na wapo wanaoenda mpaka mwaka na miezi hata miwili, mara nyingi watoto wa kiume huwa wanachelewa
 
Usiwe na shaka ndugu hilo ni jambo la kawaida kabisa. Mwanangu wa kiume ameanza kutembea karibia mwaka na miezi 6 na hata kuongea alichelewa sana. Leo hii ana miaka 5 yupo gado ile mbaya.

Tuliza pressure kama keshaanza kutembea kwa kushika ukuta basi ndo safari imeanza. Ukienda kuwauliza wazaramo watakutia pressure bure - watasema mtoto kabemendwa kumbe wala.

cheers!
 
Anayewahi Mara Nyingi ni ktk miezi tisa na anachelewa agharabu anafika hadi mwaka na miezi miwili. Sababu ni kwamba wato wengi huwa hawafanyiwi mazoezi ya viungo na mazoezi mengine mfano kukaa au kutembea. Unashauriwa asubuhi unakuwa unamfanyisha mazoezi na kumnyoosha nyoosha viungo vyake.

Tatizo la kutembea pia linasababishwa na wazazi kufanya mapenzi kabla mtoto hajakua vyakutosha (kumbemenda). Tatizo Hakuna ila ni aibu tu kuonekana kuwa hamumtendei mtoto haki yake na mara nyingi watoto hawa wana kuwa sio wachangamfu kama watoto wengine pia hata kiakiri.

N.B huu ni mtazamo wa kimazingira na hali halisi na sio wakitaalamu hivyo unaweza kukinzana na wakitaalamu.
 
Huyo atatembea ondoa shaka jitahidi kumzoeza kutembea huku unamshikia au nunua baby worker ni nzuri sana hasa ile ya kienyeji (ya mbao). Kilimsaidia bint wangu akaanza kutembea akiwa na miezi nane na nusu.
 
Ajitahidi tu kumtembeza au kumfanyisha mazoezi ya kila kitu
 
Atatembe usihofu. Mi nilichelewa kuongea hadi watu wakafikiri nitakuwa bubu.

Na ulivyoanza kuongea ukawa kama umetiwa funguo hahahahahah lol! Nasikia Mama akawa anasema huyu tangu ajue kuongea imekuwa shida tupu! :):) Wala usiwe na wasiwasi kwa mtoto wa mwaka mmoja kutotembea wengi tu huwa wanachelewa lakini sidhani kama atamaliza mwaka huu kabla ya kuanza kutembea.
 
Na ulivyoanza kuongea ukawa kama umetiwa funguo hahahahahah lol! Nasikia Mama akawa anasema huyu tangu ajue kuongea imekuwa shida tupu! .

yaaani kama ulikuwepo. Nilikuwa natema cheche balaa ila siku hizi siongei ongei sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
yaaani kama ulikuwepo. Nilikuwa natema cheche balaa ila siku hizi siongei ongei sana.


Naam ndio huwa hivyo.....Mhhhhh ya kweli hayo? Mbona bado unaendelea kutema cheche hapa JF? :):)
 
Naam ndio huwa hivyo.....Mhhhhh ya kweli hayo? Mbona bado unaendelea kutema cheche hapa JF? :):)

we mwenzio siku hizi sio mwongeaji hadi najiona zoba.
Bado kidogo niwe bubu kama wewe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom