Umri wa Makamu wa Rais na Rais katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania utazamwe upya

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,540
46,077
Nafahamu katiba inasema wazi mtu atakayeshika nafasi ya urais wa JMT anapaswa kuwa na miaka 40 na kuendela ila sifahamu katiba inatoa maelekezo gani kuhusu umri wa makamu wa Rais. Aliye na ujuzi wa hali anifahamishe.

Pia tumeshudia Rais Magafuli alivyowependwa na watu kiasi cha kuanza kufiria kuibadili katiba na kumuongezea muda jambo ambalo nafikiri lingekuwa hatari katika nchi ambayo bado demokrasia haijakomaa kiasi cha kutosha.

Kusema hayo ni kwamba tunaweza kuja kupata Rais amabaye ni kijana wa miaka 40 au hata miaka 50 na akapendwa kuzidi magufuli kisha ukomo wa muda Urais ukaondolewa kabisa na tukajikuta na Rais wa muda mrefu kama Museveni au Kagame.

Hivyo basi napandekeza yafanyike mabadiliko angalau madogo katika katiba yetu kuongeza umri wa kushika nafasi ya Urais hadi miaka 60 kutoka 40 ya sasa ili hata kama akipendwa sana na katiba kubadilishwa kwa sababu yake akiwa na miaka 70 bado asiwe na muda mrefu wa kukaa madarakani.
 
Mapendekezo ya humu yanachekeshaga sana mtu anaamka anasema umri wa kua Rais uwe 60 sijui akija kufa awe 70 kwamb asikae sana madarakani ni vichekesho.

Mjumbe hauwawi Mjumbe hauwawi. Haki ya Mungu Tundu hatokaa awe raisi hata siku moja ni Ujumbe tuu wakulungwa, Kama itawauma nisameeni.
 
Unafikiri nini kifanyike tusije kuwa na Rais atakeyakaa madarakani muda mrefu kama Gaddafi, Kagame au Museveni?
Mapendekezo ya humu yanachekeshaga sana mtu anaamka anasema umri wa kua Rais uwe 60 sijui akija kufa awe 70 kwamb asikae sana madarakani , ni vichekesho...
 
Unafikiri nini kifanyike tusije kuwa na Rais atakeyakaa madarakani muda mrefu kama Gaddafi, Kagame au Museveni?

Waliokuwa wanataka kuongeza muda wa Magufuli si wananchi wala chama chake bali ni yeye mwenyewe kupitia genge lake.

Njia nzuri na rahisi ya kuzuia hilo lisitokee ni kuweka masharti magumu sana ya kubadili katiba.

Kwanza viwepo vipengele vinavyozuia katiba kubadilishwa kwaajili ya kukidhi matakwa ya mtu.

Pili kubadili katiba lazima wananchi washirikishwe kwa asilimia zote kuanzia kutoa maoni na kupiga kura.Ili katiba ibadilishwe lazima ziwepo sababu za msingi si sababu za kisiasa ambazo zina malengo ya kumnufaisha mtu au kikundi cha watu.

Iwe ni kosa la jinai kutamka ndani ya bunge au nje ya bunge kuongeza muda wa Rais kuongeza muda wa kutawala.Kipengele kitazuia wanasiasa wajinga wajinga kujipendekeza au kujinufaisha kwa namna yoyote.
 
Wapo wananchi wengi walikuwa wanataka ukomo wa Urais uondolewe kwa sababu yake, wengine ni wasomi kabisa na mimi nimezungumza nao huku mitaani.

Magufuli inawezekana hakuwa hata na huo mpango kabisa ila kuna watu walikuwa wanataka hivyo ndio maana wabunge kama Kessy na Deo Sanga wakafikia kusema ikibidi alazamishwe hata kama yeye hataki!
Waliokuwa wanataka kuongeza muda wa Magufuli si wananchi wala chama chake bali ni yeye mwenyewe kupitia genge lake...
 
Wapo wananchi wengi walikuwa wanataka ukomo wa Urais uondolewe kwa sababu yake, wengine ni wasomi kabisa na mimi nimezungumza nao huku mitaani...
Wewe binafsi ulifurahi alipojenga
Chato International Airport
Chuo cha kanda Veta Chato
CRDB Chato
Hospital ya rufaa Chato
Hotel ya 3 star Chato TANAPA
Jengo la Zimamoto chato
Jengo la mahakama chato
Bohari kuu ya madawa kanda Chato
Stand ya kisasa
Stadium 🏟 proposed

Nitajie Wilaya yoyote hapa Tanganyika ambayo imepelekewa miradi yote hiyo.Hao wasomi ni mapunguani wa kutupwa wamesoma lakini hawajaelimika.Fikiria kiongozi wa aina hii aingezewe muda wa 15 au 20 !.Miradi mingi iliyopelekwa Chato ni level ya majiji si Wilaya.

Hapo bado hatujaweka suala la utawala bora,upendeleo,ubaguzi,uvunjifu wa katiba,wasiojulikana .....
 
Back
Top Bottom