Umri wa kustaafu utumishi wa umma ni miaka mingapi?

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Tuna viongozi na watendaji wengi wana umri wa zaidi ya miaka 60 na bado wanamwagiwa vyeo chungu mzima. Hivi umri wa kustaafu ulishabadilishwa? Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa ni miaka 60 - au niko dunia nyingine?
 
Kuna umri wa kustaafu kwa nafasi za kawaida tu, kwenye nafasi zingine hakuna umri wa kustaafu eg ubalozini wafanyakazi wakifika umri wa kustaafu sehemu moja wanahamishiwa huko ubalozini, tume ya uchaguzi hiyo haina umri wa kustaafu kwa sababu wanawekwa kwa maslahi ya anayewateua, mahakama kuu na mahakama ya rufaa hakuna umri wa kustaafu, wajumbe wa bodi mashirika ya umma hiyo ni nafasi ya asante kwa watu wasio na mahali pa kwenda.
 
Umri wa kustaafu utumishi serikalini ni miaka 60........................majaji na mahakimu...........65..........mengineyo ni CCM wanavunja sheria tu
 
Muungulize Ngombale Mwiru....Jibu atakalokupa ndo jibu la swali lako.......
 
Naona kuna haja ya kuweka ukomo pia wa kuwa mbunge imagine mtu ana above 65 bado mbunge si ataishia kulala tuu kamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Naona kuna haja ya kuweka ukomo pia wa kuwa mbunge imagine mtu ana above 65 bado mbunge si ataishia kulala tuu kamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

mtumishi wa kuchaguliwa (kupigiwa kura) ni tofauti na yule wa kuajiriwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa Umma. Na hii inatumiwa karibu na mataifa yote ulimwenguni. My take ni bora kuwepo na sheria ya ukomo wa uwakilishi kwa mbunge, may be 4r 10yrs only.
 
Nchi ya Tz. inaongozwa na wafu. Watu wamezeeka mpaka leo wanataka kushika madaraka kama walizaliwa nayo. Wengi watafia kwenye viti vyao vya kazi subirini. Mimi nauliza hivi watu wooooooooooooote waliozaliwa baada ya UHURU wanafanya wapi kazi maana wengi wa waliopo madarakani ni wale waliozaliwa enzi za mkoloni Tz. bana ina vihoja kweli kweli.
 
Akili inakuwa imechoka, unakuwa hufikirii kwa kutumia kichwa bali Masaburi. Waangalie wote ambao wako above 60 uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, pia wanawaza kufa ndio maana ufisadi unakuwa mkubwa hawana future kwa Watanzania wenzao bali matumbo yao na familia zao tu. Wenye uchungu na taifa ni vijana wala si wazee.
 
ukapumzike kwa lazima usijekufia kazini,tena iliongezwa makusudi toka miaka 55 hadi 60 kwani ilionekana wengi waliokuwa wanastaafu kwa miaka 55 wanakuwa hwajachoka sana na wanaweza kuishi muda mrefu hivyo kuwa mzigo kwa mashirika ya pension kuwalipa mafao watu ambao hawachangii katika mifuko hiyo pili, ni kuwa wengi ya wafanyakazi wakati ule ilipokuwa inaanzishwa mifuko walikuwa hawakatwi pension hivyo ili mifuko iweze kuwalipa ilibidi waongezewe miaka 5 zaidi ili mifuko iweze kuwalipa ikazoeleka hivyo baada ya kuonekana ni faida kwa mifuko kuwa unachangia kwa muda mrefu pindi ukistaafu na miaka 60 unakuwa umechoka sana hivyo akiba yako uliyojilimbikizia inatumika kidogo kabla ya kukutwa na umauti na kiasi kinachobaki ni faida ya mifuko Fikiria jaribu kubadili huu unyanyasaji kwani life expectancy ya Mtanzania ni miaka 49 lakini kustaafu ni 60 kwanini? Hivi Askari mwenye miaka 55 au 60 anaweza kupigana vita? HUU NI UNYANYASAJI WA DHAHIRI NA NI DHAMBI MBELE YA MWENYEZI MUNGU Hivi vijana walio mtaani sasa ni wengi wanatafuta ajira wakati vibabu viko makazini havina tija eti mifuko itapata hasara wakistaafu na miaka 55 hii ni kweli? FIKIRIA CHUKUA HATUA SASA
 
Wabunge wapunguze muda wa kustaafu hadi miaka 55. Itatoa fursa kwa vijana kupata ajira na kuongeza uzalishaji. Mimi sijawahi kuajiriwa lakini nilipofikisha miaka 55 akili zilianza kupungua kwa kasi.
 
Nakuelewa sana mwanangu, ila unahisi ni kwanini sheria ilisema ukifikisha miaka 60 unapaswa kustaafu kwa lazima?

Maana yangu ni kwamba si vema baada ya miaka 60 mtu apewe tena mkataba. Chukulia mfano wa Kova. Hivi hakuna mtu ndani ya jeshi la polisi wa kuchukua nafasi hiyo. Kaziba mlolongo mzima wa watu kupanda vyeo na mtu kupata ajira.
 
ukapumzike kwa lazima usijekufia kazini,tena iliongezwa makusudi toka miaka 55 hadi 60 kwani ilionekana wengi waliokuwa wanastaafu kwa miaka 55 wanakuwa hwajachoka sana na wanaweza kuishi muda mrefu hivyo kuwa mzigo kwa mashirika ya pension kuwalipa mafao watu ambao hawachangii katika mifuko hiyo pili, ni kuwa wengi ya wafanyakazi wakati ule ilipokuwa inaanzishwa mifuko walikuwa hawakatwi pension hivyo ili mifuko iweze kuwalipa ilibidi waongezewe miaka 5 zaidi ili mifuko iweze kuwalipa ikazoeleka hivyo baada ya kuonekana ni faida kwa mifuko kuwa unachangia kwa muda mrefu pindi ukistaafu na miaka 60 unakuwa umechoka sana hivyo akiba yako uliyojilimbikizia inatumika kidogo kabla ya kukutwa na umauti na kiasi kinachobaki ni faida ya mifuko Fikiria jaribu kubadili huu unyanyasaji kwani life expectancy ya Mtanzania ni miaka 49 lakini kustaafu ni 60 kwanini? Hivi Askari mwenye miaka 55 au 60 anaweza kupigana vita? HUU NI UNYANYASAJI WA DHAHIRI NA NI DHAMBI MBELE YA MWENYEZI MUNGU Hivi vijana walio mtaani sasa ni wengi wanatafuta ajira wakati vibabu viko makazini havina tija eti mifuko itapata hasara wakistaafu na miaka 55 hii ni kweli? FIKIRIA CHUKUA HATUA SASA
huu mswada wa mifuko ya hifadhi za jamii imesababisha nikumbuke hii mada.
 
Back
Top Bottom