Salvatory Mkami
Senior Member
- Apr 17, 2013
- 146
- 244
Umri wa kustaafu unawahusu watumishi wa umma pekee au pamoja na viongozi wote wa serikali, Mahakama, Bunge na Wabunge?!
Sheria zetu zinasemaje?!
Kwasababu kituko kitakuwa ni pale ambapo anayetoa taarifa kuhusiana na wale ambao wameghushi vyeti vya kuzaliwa na umri wao ili waendelee kudumu kwenye ajira na yeye mwenyewe akiwa mmoja kati ya wanaotakiwa kustaafu kwa lazima kutokana na umri wake wa kustaafu kuwa umepita kwa miaka kadhaa!
Ifike wakati kama serikali inamaanisha na imeamua katika kweli kulivalia njuga suala la ukomo wa ajira husiana na suala la ukomo wa ajira serikalini kwa maana ya mtumishi, kiongozi kustaafu kwa hiyari au kwa lazima iwe hivyo kwa nafasi zote na sio kwa baadhi ya sekta pekee ilihali sekta nyingine zikifumbiwa macho!
Pia ili kutoa nafasi kwa vijana na fikra mpya katika kuliendeleza taifa kuna haja kubwa ya kuweka ukomo kwa wagombea na wanaoteuliwa kwa nafasi za Ubunge, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu, Wakurugenzi nk. Kwa utaratibu huo tutakuwa tunatekeleza kwa vitendo kile tunachokimaanisha lakini kinyume na hapo ni kama tutakuwa tunaenda mbele hatua tano na kurudi nyuma hatua kumi na kujipongeza!