momara
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 463
- 490
Ndugu nawapa salam
Mimi ni kijana ambaye niliamua bila kushinikizwa na mtu kuoa ningali kijana. Huku shauku kubwa ikiwa ni kupata na kulea kizazi changu ningali kijana na mwenye nguvu. Kifupi nilikuwa na shauku kubwa ya kupata mtoto.
Nilioa nikiwa na umri wa miaka 26 ila mpaka sasa ni miaka 5 ndani ya ndoa sijabahatika kupata mtoto. Kinachoniuma zaid umri unazidi kusonga na wadogo zangu wana watoto.
Kifupi kuna shida ambayo inamsumbua mke wangu na nimejaribu ktk hospitali bila mafanikio, tiba asili na mitishamba pamoja na maombi bila mafanikio.
Hospitali tumepima mpaka ultra sound tatizo hamna dawa mbalimbali zimetumika mpaka za kutumbukiza ktk mfumo wa uzazi bila majibu.
Tiba asili na mitishamba nako hali kadhalika hakuna matokeo. Kila aliyesema anajua tulimtafuta na matokeo ni sifuri.
Na ktk maombi pia ni hivyo hivyo. Mimi ni mwislam kwa hiyo nimepita ktk visomo vya Rukya ila bado hakuna matokeo.
Wengi wanashauri ktk uvumilivu na kuwa na subira.
Subira ni jambo kubwa sana na sina shaka na hilo, ila kwa kipindi chote hicho najihisi mpweke na mnyonge sana nikiwa mtaani washkaji na marafiki wakihangaika na watoto wao mara uniform mara madaftari mara hiki mara kile ilimradi tu kila mtu anahangaika na damu yake. ROHO INANIUMA SANA.
Unajua wanaume tunatafuta hela kwa ajili ya wanawake na watoto hasa hata nguvu ya kuzisaka nakosa. Natamani na mimi iwe asubuhi halafu mtoto aliyetokana na mimi (my blood) aje kitandani na kuniita BABA NATAKA HELA NIKANUNUE SAMBUSA NJE. Hii huleta furaha sana asikwambie mtu na nguvu pia ya kuzitafuta inakuja maradufu.
Imefika hatua natamani sana kutafuta hata mtoto angalau mmoja tu nje ya ndoa na hapo ndipo tatizo lingine linapoanzia.
Kila msichani ninayejaribu kumtongoza ananielewa vizuri tu ila kabla ya kufanya lolote naye swali la kwanza hujaoa? Hapo napataga wakati mgumu sana kujibu, binafsi dhambi inayonitafuna sana ni kuongea ukweli na kuogopa kumdanganya msichana ktk mapenz.
Nikimwambia sina itakuaje pale atakapopiga simu usiku na kutuma meseji mimi muda huo nipo na wife? Mbaya zaidi mke nilie nae ana wivu mpaka balaa na ukimkosea kidogo basi yeye hupeleka fikra zake ni kwa vile sina mtoto. Kifupi nachunga sana ili asikwazike na awe na furaha japo wote tupo na stress.
Kifupi sipendi kudanganya kuepusha hayo yote. Dini yangu inanipa fursa ya kuoa mke zaidi ya mmoja ila nalo ni changamoto sana, binti kumwambia nikuoe mke wa pili nayo ni shida kubwa ni lazima uwe na uwezo nami nikijiangalia sina uwezo wa kuhimili ndoa ya pili na uwezo wa kifedha pia ni changamoto.
Niliamua kutafuta angalau nimpate single mother ambaye tayari ana uwezo wa kujisimamia japo kidogo ili nianzie alipoishia tusonge mbele nami anizalie wangu tukishibana tujenge familia ila nalo ni changamoto sana.
Nimefungua na uzi kabisa hapa JF nikitaka single mother ila sijaona mwitikio bado.
Kifupi tu inafikirisha sana na kila ninaemfikiria na kumkabili kumweleze kuwa nahitaji mtoto ROHO inanambia utapotea na utatafutiwa au upewe mimba isiyo yako.
Natamani kufanya ngono hovyo na huyu na yule then nikae nisubiri kuletewa mimba ila nawaza na kufikiri magonjwa nabaki nanywea. Nyumbani wananiangalia tu nami naangalia chini mwingine ananiuliza huna hata mtoto nje nabaki natabasam kumfumba naye anabaki haelewi...!
Jamani wanaJF niko hapa kupokea maoni nifanye nini nipate japo mmoja wa kuanzia. Umri unaenda kasi sana nami sipendi mwaka huu uishe bila mtoto au hata mimba tu.
Kwa upande wa mke wangu yeye bado mdogo 23yrs so hata ikitokea miaka mingne 4 au 5 ya kuhangaika ikatokea kupata mtoto bado si mbaya sana nikijilinganisha na mm sasa hivi nina 30+.
Karibun.
Sent using Jamii Forums mobile app