Umri, uchumi na umaskini: Vitu vitatu vinavyotutaka vijana tupanuke kiakili je, tutafika?

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,213
56,849
Hivi vitu vitatu ni changamoto haswa katika ujana wetu, kwenda kwa umri ni kana kwamba tunashushuliwa tukue kiuchumi hali ya kuwa umaskini unatuvuta mashati.

Ni ndoto ya kila mmoja wetu kuwa na maisha matamu, maisha ya kula bata n.k

Kuwa imara kiuchumi kwa kijana ni fursa ya kuutumia ujana wake kimatanio.

Naweza nisieleweke nazungumzia nini ila vitu hivyo vitatu ni mind blowing haswa kwa sisi vijana ambao bado hatujatoka kwenye utepe uitwao umaskini.

Umaskini katika familia zetu hufufisha tondo za kujijenga kwetu, kwani kile ukipatacho kinahitajika kuziba pengo nyumbani na wakati huo huo una mapengo yako unayotakiwa uyazibe!!

Kwa hivyo hii inatulazimu kuwa tupate kingi kitoshe kwako na kwenu.

Swali la kujiuliza je, uchumi unakupa nafasi ya kupata kiasi kinono cha kula na kusaza?

Hilo halitoshi wakati unatumikia hilo umri nao unakupiga kikumbo uende nao sambamba kiuchumi!

Haitoshi bado mambo yetu ya kutiana mimba yanatusubiri

Ni dhahiri vijana wa Sasa hali inatutaka tuwaze mbali zaidi ili tutoke kifua mbele, niihase serikali ihakikishe inaweka ubora katika sekta za kiuchumi ili vijana tuwajibike tuitoe fedheha mbele yetu, na hata huko serikalini kunatakiwa kuwe na viumbe vinavyojua shida kiundani wanazopitia watu wao.

Tusilaumiane tu kuwa vijana wa Sasa hatujitumi je, huko kujituma kwenyewe kuna manufaa maana isiwe mbio za sakafuni.

Dimbwi la kujitosa kwenye biashara haramu huhamasishwa na vitu hivi tamaa binafsi, uchumi mbovu wa nchi na chengine ni umaskini!!

Vijana wa Sasa tunahitajika kuwa na maarifa makubwa tutapendeka tu! Huu sio muda wa kujilaumu au kulaumu ila ni muda wa kutumia akili zetu itupasavyo.

Maisha mema ndugu zanguni..
 
Back
Top Bottom