Umri sahihi wa kumuanzisha mtoto shule ya awali

intelinside

JF-Expert Member
May 21, 2015
304
400
Habari

Ni kama swali jepesi sana kwa nyakati hizi lakini nahitaji sana ushauri na maoni yenu.

Nina mtoto mdogo wa miaka miwili na miezi kama 4, mama yake anataka tumpeleke shule, pamoja na sababu zake anazitoa, mimi naona bado ni mdogo sana yani hata mitatu bado naona ni mapema japo angalau angekua na umri huo kidogo ningeshawishika.

Pia naona huu usasa unatuzuzua na kutafuta sababu za kutokulea watoto wetu kama tulivyolelewa sisi, badala yake tunataka watu watusaidie hata hatua za awali namna hii...

Naombeni ushauri wenu ikiwemo faida na hasara, nisijekuonekana ni mhafidhina wa haya mambo.

Asanteni
 
Bro cku hz wanawake wetu wavivu sana kulea huleta visingizio ving sana kaka baba usikubal yumbishwa na huyo mkeo. Miaka halali n 4yrs kinyume na hapo n mbwebwe na uvivu wa kulea
 
Bado mdogo sana mkuu simama kama mwanaume ndani ya nyumba mwanamke aache uvivu..at least miaka mi3 au mi3 na nusu or labda kama kuna ushauri wa doctor..binafsi mwanangu ana miaka mi2 na miezi 6 hajaweza kuongea vizuri yaani anasema maneno machache sana Muhimbili kitengo cha speech wamenishauri nimpeleke shule kuchanganyika na watoto wenzie.kama kuna sababu za msingi kama hizi sawa sio tofauti na hizi.
 
Ni vema wazazi wakalea mtoto wao kwa hatua za awali, Mlee mtoto wako katika misingi uipendayo huko kwingine wataendeleza,
Ndo maana siku hizo watoto wanakuwa na tabia za ajabu ambazo wazazi hawajui zimetokea wapi, kumbe tatizo hawakuijenga misingi ya awali kwa watoto wao.
 
Mimi naona Walau kuanzia miaka 4 , kumpeleka mtoto mtoto Shule Kwa umri wa chini ya hapo naona ni kumtesa, maana itabidi awe anaanza kuamshwa asubuhi na mapema ili aandaliwe kwenda Shule kila Siku Mimi naona ni kumtesa mtoto! Akifika umri wa miaka 3 Na nusu akishaamka Kwa wakati wake Na kumaliza kunywa uji basi Kama kuna Ka Shule Karibu Na home anaweza kwenda kuanza kujifunza kidogo na kucheza Na wenzie pia ku socialize akifika miaka 4 sasa Ndiyo ataanza Shule rasmi ya kindergarten Kwa kuamshwa asubuhi! Maana ikumbukwe kuwa mtoto anapoanzishwa Shule unakuwa ndo mwanzo wa safari Yake ya kusoma sasa yanini kumchosha mapema ?!
 
Kwa umri huo na kwa kuzingatia mfumo wa utoaji wa elimu ya awali Tanzania bado hauna tija kwa sababu mtoto wa miaka miwili kisaikolojia inabidi afundishwe social skills tu na siyo masomo ya darasani. Usasa unatuharibu! Shule zetu za awali nyingi zinavuka mipaka yaani badala ya kumfundisha mtoto namna ya kuinteract na jamii wao wanarukia kwenye masomo.
 
Ndo globalization ilipo tufikisha hapa na safari yetu ndo kwanzaaa imeanzaa....., wee shemelaaa wew hacha kumchosha mtoto kisa uvivu.
 
Watoto waliotekekezwa siku hizi ni wengiii, wengine wako mitaani,wengine kwenye vituo vya watoto yatima na wengine wapo mashuleni.
 
Pamoja sana wakuu... Msimamo wangu ni kama wenu... Na hivi ndivyo inapaswa kuwa... Asanteni sana...
 
Back
Top Bottom