Umri ni kigezo kikubwa katika harakati za taasisi ya urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umri ni kigezo kikubwa katika harakati za taasisi ya urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Mar 2, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Je umri unaotajwa wa 35 unafaa kuwa mmojawapo za sifa za presidential candidate ajae,pamoja na matukio yaliyotokea huko Zaire ya zamani kutoa kijana mdogo kama Joseph Kabila na Liberia Samwel Doe.Je nini athari ya wagombea wa nafasi hiyo kubwa nchini mwetu kuwa na umri mdogo?Nawakilisha tulijadili hili kwa mustakabali wa taifa letu
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu umri wa miaka 35 ni sahihi tu wala hauna shida.

  Hapo kwenye wekundu, hawa walifanya nini?
   
 3. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Itatubebesha mzigo kuwatunza baada ya kumaliza mihula miwili wakiwa na miaka 45. Ni gharama kubwa kumgharimia rais mstaafu kwa ziadi ya miaka 30.
   
 4. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Civil war or the military coup to overthrow the Goverment, no matter how the leader of the group
  of persons be, if is seventiny years old or twenty years old, he can be the President.
  Lakini kwa tawala zetu za kiraia za Kiafrika bado hatujafikia kiwango cha kuanzia miaka 35 mtu
  anaweza kuchaguliwa kuwa Rais, tusijidanganye bado wakati. ukomavu ndio muhimi ya muhimili
  huo, kwa kuanzia miaka arobaini na kuendelea hicho ni kiwango kizuri. Ukiangalia marais wote
  walioanza na umri wa chini ya miaka arobaini, walianza vibaya kiutawala na walimalizia vibaya sana.
  Kwa sababu walikuwa wanayumbishwa na washauri kutokana na wao kutoelewa wapi waelekee,
  na mpaka wanaposhtuka muda unakuwa umeshapita bila ya kuwa na mema wala mafanikio.
  Tuchulie mfano Hayati Nyerere, personal secretary wake alikuwa mwanamke mama wa kiingereza,
  na ambaye alikuwa mshauri wake mkuu, sasa angalia iliwezekana vipi amshauri afuate siasa ya
  ujamaa na kujitegemea, yaani Marxist wakati Uingereza hawapo katika mfumo huo, labda inawezekana
  ulikuwa ni mfumo wa waingereza kuiangamiza nchi yetu bila kujijua. na yeye wakati huo hakuwa na
  ukomavu na hakuelewa nini kinchoendelea. Ndio hivyo Mobutu alivyozungushwa akili na wabeligiji,
  na ndio hivyo Gaddafi alivozungushwa akili na Warusi. kwa sababu ya kiungia katika madaraka bado
  wadogo, na bila ukomavu na kushindwa kujiongoza wenyewe. huo ndio muono wangu. tupiganishe
  akili na mawazo kuchambua uzuri na athari zake, kuhusu kigezo cha umri. ingawaje JK. alizungumzia
  kuhusu ndani ya chama chake, lakini inafaa kujadiliwa pia na wanabodi.
   
 5. E

  Emmanuel Piniel Member

  #5
  Mar 2, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwatunza si tatizo endapo ameongoza nchi vizuri ila sheria ingepitishwa ya kuwanyonga wale wabadhilifu kwa mtindo huu watajipunguza wenyewe na gharama zitakuwa chini sana; umenipata hapo
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwalimu hakushauriwa na personal secretary wake kufuata siasa za ujamaa. Kajipange upya.
   
 7. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kwa upande wangu nafikiri umri wa miaka 39 kushuka chini bado ni mdogo,japokuwa tuna tofautiana kimtazamo.Si vizuri kuongozwa na hisia zetu lakini umri wa kuanzia miaka 40 ni umri mzuri ambao licha ya utamaduni tuliouzoea bali pia ukomavu wa fikra ndipo huanzia hapo.Ndo maana Waingereza wana amini ni vizuri kama mtu akifanikiwa kuwa tajiri katika umri wa miaka 45 kwani hawezi kuymbishwa kifikra na wamzungukao.Sisi wote tumeona hata wabunge wetu wakati mwingine wanafanya mambo ambayo hayaendani na hadhi ya kibunge.Wakati mwingine wanaongozwa na ujana zaidi kuliko mtazamo wa kiutendaji.Unapokuwa matured enough hata thinking capacity yako inakuwa zaidi.Unaweza ukawa na mawazo mazuri tu katika kupambanua mambo lakini ukawa una kosa busara na subira katika kufanya maamuzi ama yenye tija au kupotosha kabisa kutokana na ukosefu wa subira.

  Wakati mwingine ni muhimu wazee kuwepo kwenye system ili kuweza kuwarekebisha vijana pale wanapokuwa wamepotea.Sisi sote tumeona madhara yanayosababishwa na vijana wadogo waliopewa dhamana kubwa ndani ya serikali.Sioni ni kwanini tubadili umri huu katika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi kwa kushusha umri uliokuwa unatambulika kisheria na kuweka huu wa sasa unaojaribu kupigiwa chapuo.Sipendi kusema ni uroho wa madaraka kwa vijana,la hasha bali wakati wao unakuja ni vizuri wakawa na subira.Kuna hadithi moja inasema ukinya mavi makubwa si kigezo cha kuonekana umekuwa.Tunathamini sana michango yao vijana katika harakati za kusuma gurudumu la maendeleo yetu lakini haraka ya nini?

  Wakati wa mfumo wa kikomunisti huko Urusi iliaminika ili uwe na kigezo cha kushika nafasi ya juu kabisa ya madaraka katika nchi hiyo kigezo kikubwa kilikuwa umri.Waliamini huwezi kuwa mkomunisti aliyekomaa ukiwa chini ya umri wa miaka 60.Jamhuri ya kisoveti ilipoteza umaarufu wake na umoja wake alipoingia Mh. Gobarchev akiwa na umri chini ya miaka 60,kitendo kilichosababisha kuleta mapinduzi mapya katika utawala uliokuwa chini ya mfumo wa kikomunisti,matokeo yake ni kurubuniwa kwa Gobarchev na kusambaratika kwa taifa lenye nguvu la iliyokuwa Urusi.Kitendo cha kusambaratika kwa taifa hilo leo hii ni kiburi cha Wamarekani kwa mataifa manyonge.

  Lazima umri uwe kigezo japokuwa wanasema hauna athari kibiologia,kwangu mimi naamini miaka 35 ni adolesence stage hivyo bado ni umri mzuri wa kuandaliwa kifikra na kimtazamo katika maisha.Tusiruhusu hali hii ikatokea kwani kuna watu wanaamini wamezaliwa kuwa viongozi kwa mtazamo wao,japokuwa ni haki ya kila raia kugombea nafasi ya uongozi.
   
 8. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Mimi wangu katekeleza moja tu ya kwake aliyojiahidi mwenyewe ya kujipatia posho nono, bahati mbaya nayo kaikosa
   
 9. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Wakuu,kwa muono wangu suala la umri wa urais kupunguzwa mpaka miaka 35 nadhani hapana,hapana yangu itajikita ktk maeneo mengi.mtu wa umri huu kwanza bado mambo ya ujana hayajamtoka,bado kuna mambo kisaikojia anakuwa hajasetle,pamoja na sifa ya umri lakini taasisi ya urais pia inataka hekima ya kipekee sana ambayo walio wengi wanakuwa wanaikosa,sasa hekima hii pamoja na kuwa ni karama pia inahtaji muda wa kuitumikia kabla ya kuingia ktk uwanja mpana wa kutumika na wengne kwny post kama ya urais,uelewa wa mambo in 3d pia ni jambo la msingi sana kwakuwa kila aina za watu utakutana nazo,vijana kwa asili si watu wa subira,tuna haraka na wakati mwingine tunaweza kuamini maamuz yetu ndio sahihi zaid kumbe sivyo.jamani tusipende kujiweka kuwa sample kwny mambo makubwa kama haya,maana kuna maeneo tumekwama sana ktk nchi yetu kwa kuwa hisia zetu ndizo zimechagua viongozi badala ya utashi wetu.nachelea kusema we are not planing to fail,bt we fail to plan.urais si taasisi ya kuchezea coz badae watu watasema pia uraisi ugombewe na miaka 18,vzr tuelewe uzito,ugumu na unyeti wa nafasi ya urais ndipo tuseme pamoja na sifa nyngne pia umri gani unafaa.nawasilisha!
   
Loading...