Umri halisi/ukomo wa mwanamke kuzaa

Sadagada

Member
Dec 9, 2011
76
37
Heshima kwenu Madaktari, naomba kujua ukomo wa umri wa mwanamke kuzaa.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 33. Nimekuwa na uhusiano na mabinti wa umri chini yangu ila wamekuwa wakiniacha kwa sababu ambayo ipo nje ya uwezo wangu kuirekebisha.

Kutokana na mimi kuwa na hamu ya kuitwa baba,nimebahatika kupata mwanamke mwenye umri wa miaka 43 ambaye amesema yupo tayari nizae nae.

Naomba kujua kama jambo hili linawezekana haswa kwa mtoto atakayezaliwa kama atakuwa na afya njema.

Ni matumaini yangu kujibiwa vyema na waheshimiwa Madaktari.

Ahsanteni.
 
ile ni kama photocopy mashine!mwanamke anaweza kuzeeka sura but akaproduce mtoto genious kinoma!-nmejibu kimtaa mtaa.

ngoja waje wanataaluma watwambie!
 
anaweza kuzaa. . . but anahitaji uangalizi mzuri kipindi chote cha ujauzito
 
Sorry kama vile sijaelewa ....eti wewe una 33 yeye ana 43 years.??...Sasa hapo nani ni mume nani ni mke..???
 
miaka 45 mwisho kwa aliyekuwa anazaa tayari.kama hakuwahi kuzaa hata mara moja hiyo 43 ni hatari sana kwake, akapime na kupata ushauri wa daktari kwanza
 
hapo itabidi uwafatilie waliofanya research zao ,japo kiutaratibu mwanamke akifikisha kuanzia 4#+, japo inategemea na mazingira(hapo kuna vitu vingi mno) aliyokuwa nayo.
 
45 mpaka 50. Kama hakuwahi kupata mtoto hapo kabla hapo kupata mtoto na huyo Mama chansi ni ndogo sana. But nendeni hospitalini mkapimwe nyote wawili kisha baada ya vipimo vya uzazi ndio mtapata jibu.
 
Kama wote mna afya njema basi hakuna tatizo Mkuu, kila la heri.

Heshima kwenu Madaktari, naomba kujua ukomo wa umri wa mwanamke kuzaa.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 33. Nimekuwa na uhusiano na mabinti wa umri chini yangu ila wamekuwa wakiniacha kwa sababu ambayo ipo nje ya uwezo wangu kuirekebisha.

Kutokana na mimi kuwa na hamu ya kuitwa baba,nimebahatika kupata mwanamke mwenye umri wa miaka 43 ambaye amesema yupo tayari nizae nae.

Naomba kujua kama jambo hili linawezekana haswa kwa mtoto atakayezaliwa kama atakuwa na afya njema.

Ni matumaini yangu kujibiwa vyema na waheshimiwa Madaktari.

Ahsanteni.
 
Heshima kwenu Madaktari, naomba kujua ukomo wa umri wa mwanamke kuzaa.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 33. Nimekuwa na uhusiano na mabinti wa umri chini yangu ila wamekuwa wakiniacha kwa sababu ambayo ipo nje ya uwezo wangu kuirekebisha.

Kutokana na mimi kuwa na hamu ya kuitwa baba,nimebahatika kupata mwanamke mwenye umri wa miaka 43 ambaye amesema yupo tayari nizae nae.

Naomba kujua kama jambo hili linawezekana haswa kwa mtoto atakayezaliwa kama atakuwa na afya njema.

Ni matumaini yangu kujibiwa vyema na waheshimiwa Madaktari.

Ahsanteni.
Kuna dada mwaka 2015 alipata twins wa kike na wa kiume katika umri wa 49 yaani ali conserve akiwa 48, madaktari walimpa somo watoto wanaweza kuzaliwa na downing syndrome, watoto wametoka fresh, na ilikuwa natural birth.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mie naona kama bi dada ana afya nzuri anakula vizuri basi anapunguza sana hili la down syndrome. Siku hizi katika nchi nyingi duniani wanawake wanachelewa sana kupata watoto kutokana na kutaka kujipatia elimu ya juu na kujiweka sawa kwenye ajira. Hivyo wengi wanaanza kupata watoto mid 35 na kuendelea wengi wanajaaliwa kupata watoto wenye afya njema.

Kuna dada mwaka 2015 alipata twins wa kike na wa kiume katika umri wa 49 yaani ali conserve akiwa 48, madaktari walimpa somo watoto wanaweza kuzaliwa na downing syndrome, watoto wametoka fresh, na ilikuwa natural birth.
 
Monopose inaanza miaka 40 na kuendelea.Uwezo wa mayai kuzalishwa huanza na miaka 40,hivyo uwezekano wa kupata mtoto kwa mwanamke ni mdogo.
Na endapo mwanamke ataweza kuzaa na umri mkubwa kwa maana kuanzia miaka 40 kunauwezekano mtoto akawa na mapungufu ya cell mwilini.
Hivyo ni vema wanawake wakachukua tahadhari mapema katika suala la uzazi,ila kwa mwanaume madhara ya uzazi uzeeni siyo makubwa kwani inachotakiwa tu ni mbegu za mwanaume kuwa na uwezo wa kutunga mimba.
NB: Ukomo wa kuona siku kwa mwanamke(Menstruation Period/cycle) huanzia miaka 40 hivyo ni vigumu urutubishaji kufanyika kwaajili ya utungaji mimba maana hakuna mayai tena na kama yatakuwepo uwezekano ni mkubwa kwa mtoto aliyezaliwa kuwa na mapungufu ktk cell za mwili kwani kuna kiwango cha cell zinahitajika kuzalishwa na mwanamke na mwanaume ili mtoto kupatikana au utingaji wa mimba.
 
Safii sana kwa wachangiaji,, nakuomba uwe makin na matapelii wa mjin wanaotumia kisingzio cha mimba kutapeli mtu,,,,, 43 yrs uwezekano wa kupata mtoto aliyekamilika ni mdogo sana,, mean matatzo mbalimbali kipnd cha mimba hadi kujifungua,,, Ombi tafuta umri chin ya 40 '' ila kama kiuchumi yusmart go on
 
Heshima kwenu Madaktari, naomba kujua ukomo wa umri wa mwanamke kuzaa.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 33. Nimekuwa na uhusiano na mabinti wa umri chini yangu ila wamekuwa wakiniacha kwa sababu ambayo ipo nje ya uwezo wangu kuirekebisha.

Kutokana na mimi kuwa na hamu ya kuitwa baba,nimebahatika kupata mwanamke mwenye umri wa miaka 43 ambaye amesema yupo tayari nizae nae.

Naomba kujua kama jambo hili linawezekana haswa kwa mtoto atakayezaliwa kama atakuwa na afya njema.

Ni matumaini yangu kujibiwa vyema na waheshimiwa Madaktari.

Ahsanteni.
. ANA ZAA TU HUYO
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom