Umri gani ni sahihi kumpa mtoto smart phone?

Smart phone na social media haviepukiki katika dunia ya leo. Moja ya faida ni kuelimisha, kuna binti wa miaka 10 aliweza kuandaa period pack yake kabla hata ya kupevuka kutokana na uwelewa alioupata kutoka kwenye Internet. Hii ni moja ya faida chanya za social media.

Watoto wanapata habari nyingi mno na nyingine ni hatari kwao kufahamu, kutokana na uwezo wao wa kupambanua mambo. Maisha ya sasa hivi yalivyo hata usipomnunulia mtoto simu, kuna ndugu na marafiki wa karibu watakao waza zawadi ya simu kwa birthday au sikukuu ya dini.

Ni umri gani ni sahihi kumruhusu mtoto kuwa na simu hii na ni jinsi gani unaweza kumlinda?
asee hizi smart phone si kwa mtoto wala mtu mzima, zina mambo mengi. Heri umnunulie mtoto computer aizoee mapema, smartphone atumie akisha hitim chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom