Umoja wa wanawake Tanzania kumuenzi Bi. Titi Mohamed

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
BI. TITI MOHAMED (1926 - 2000)HANA MFANOWE

Historia ya Bi. Titi haijaandikwa.

Naamini ni watu wachache sana wanajua kuwa Bi. Titi Mohamed amepanda jukwaani kuhutubia mkutano wa TANU Viwanja Vya Mnazi Mmoja wala haijui sura ya Julius Kambarage Nyerere inafananaje.

Naamini pia si wengi halikadhalika wenye kujua kuwa wazungumzaji wakubwa wa TANU walikuwa watatu - Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU, Bi. Titi Mohamed na Julius Kambarage Nyerere walikuwa wakipanda jukwaani kuhutubia kwa mpangilio huu.

Hawa watatu na wengine katika viongozi ndiyo waliokuwa wakikaa juu ya jukwaa la TANU.

PICHA: Bi. Titi Mohamed akiwa juu ya jukwaa la TANU na Julius Nyerere wakihutubia wananchi bega kwa bega.

Bi. Titi Mohamed na viongozi wengine wa TANU John Rupia, Zuberi Mtemvu, Iddi Faiz Mafungo, Robert Makange, Rashid Sisso wakimsindikiza Nyerere safari ya kwanza UNO 1955.

Screenshot_20211019-080017_Facebook.jpg
 
Ilikuwaje wakavurugana na Nyerere?

Mbona nasikia Oscar Kambona ndio ilikuwa injini ya TANU?
 
Mzee Wangu Mohamed Said, heshima kwako. Naomba nitoke kidogo nje ya mada, hivi umaarufu wa Tabita Siwale kwenye siasa ulisababishwa na nini?

Nakushukuru kwa jibu lolote utalonipa. Asante sana
Buji...
Wakati Harvard na Oxford University Press New York wanatafuta waandishi wa mradi wa Dictionary of African Biography waliniomba nishiriki kama mwandishi niandike historia ya baadhi ya wanasiasa wa Tanzania.

Nilipokea majina kutoka kwao.

Wengi wao hawakuwa na lolote lisilo la kawaida kuwa kigezo cha wao kuwa ndani ya kamusi hilo.
 
Buji...
Wakati Harvard na Oxford University Press New York wanatafuta waandishi wa mradi wa Dictionary of African Biography waliniomba nishiriki kama mwandishi niandike historia ya baadhi ya wanasiasa wa Tanzania.

Nilipokea majina kutoka kwao.
Wengi wao hawakuwa na lolote lisilo la kawaida kuwa kigezo cha wao kuwa ndani ya kamusi hilo.
Asante sana. Sikujua kwamba ulishiriki kwenye mradi mkubwa namna hii, hakika wewe ni Lulu kwenye soli ya kiatu cha mtoto. Natamani Taifa letu lingeutambua na kuuthamini mchango wako na kukutuza.
 
Back
Top Bottom