Umoja wa wanawake JF

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
Wanawake hapa ndani si wengi sana,
nadhani kuna haja ya kuanzisha umoja wao ambao utasababisha changamoto ndani ya forum.
Wanawake ni ma organizer wazuri sana,
pia wanashiriki kikamilifu shughuli zote za kijamii kama misiba, send off, kitchen party na nyingine.
Je mnaonaje kwa uwepo wenu hapa jamvini mkajiorganize na kupanga ni sehemu gani ya jamii ambayo iko taabuni tuitembelee na kuongea nao kwa kuwasaidia chochote?
Sehemu hizo ni kama nyumba za watoto yatima, shule zenye uhaba wa madawati, waliokumbwa na mafuriko na kadhalika.
Naamini watu kumi wenye moyo wakijichanga kwa moyo na kutoa hata 50,000 wanaweza kufanya kitu cha kuiinua jamii yetu na kuipunguzia ukali wa maisha .
 
hapa nitachangia kesho ngoja nianze kumkaangizia mzee

umenikumbusha mbali wewe ...."why did I get married"

back to the mada....kwanini tusifanye project hiyo kwa yeyote ambaye yupo interested na si wanawake tu??
 
Napinga wazo hili ambalo ni IMPORTED!

wANAWAKE WALIOMO HUMU NDANI WANAAKILI TIMAMU, WASOMI, WAELEWA NA WANAJUA JEMA NA BAYA.

Why the hell ku'implant wazo kama hilo kwao, while you know kama wangeona umuhimu wangeshafanya zamani?

Are you here to give directives to these ladies?

Kama wange'conceive wenyewe wazo hilo basi lingekuwa jema sana na mimi ningesupport, na wao wangelisimamia kuhakikisha lina'take off!

After all, why not wanaume kama wewe kuanzisha umoja?.
I thought it could be the best idea on earth?

Embu ukadigest vizuri, labda kuna point between the lines!
 
Bujibuji,

Niliwahi kutoa wazo la namna hii kwenye thread yangu ya "uwezo tunao, tunahitaji nini zaidi?" sikupata sapoti kubwa. Bado naamini ni wazo zuri kujaribu kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kiasi tutakachoweza. Mimi nafikiri tujipange kama wana JF na sio kwa kuangalia jinsia na vigezo vingine - atakaeguswa aruhusiwe kushiriki bila kuangalia jinsia yake.

Asante sana,

Annina
 
Wanawake hapa ndani si wengi sana,
nadhani kuna haja ya kuanzisha umoja wao ambao utasababisha changamoto ndani ya forum.
Wanawake ni ma organizer wazuri sana,
pia wanashiriki kikamilifu shughuli zote za kijamii kama misiba, send off, kitchen party na nyingine.
Je mnaonaje kwa uwepo wenu hapa jamvini mkajiorganize na kupanga ni sehemu gani ya jamii ambayo iko taabuni tuitembelee na kuongea nao kwa kuwasaidia chochote?
Sehemu hizo ni kama nyumba za watoto yatima, shule zenye uhaba wa madawati, waliokumbwa na mafuriko na kadhalika.
Naamini watu kumi wenye moyo wakijichanga kwa moyo na kutoa hata 50,000 wanaweza kufanya kitu cha kuiinua jamii yetu na kuipunguzia ukali wa maisha .

Huenda unatafuta mwenza hapa JF, endelea kuwa mbunifu maana hata mimi nime-confuse who is dude or dudette.
 
......Wewe Bujibuji nadhani ni mwanamke mmojawapo hapa Jf, hebu anzisha basi hiyo organization ya wanawake hapa na vile vile ingekuwa bora kama ingekuwa ya gender zote.

Mie kama mwanamke pendekezo langu ni kusaidia kwenye vituo vya watoto yatima, na kama mtu una uwezo wa kifedha basi hebu tuwe na utamaduni wa kuadopt watoto jamani.
Hata kama bado hujazaa hebu kuwa na moyo wa kuadopt mtoto, watoto yatima wanataabika wengine huko kwenye vituo vyao vya kulelewa, hebu kuwa na uchungu na hawa watoto.
 
Kama dada zetu wanaliona wazo ni zuri (bila ya kujali limeanzishwa na nani) na kuwa inaweza kuwa ni sehemu yao wao wenyewe kuzungumza na kujadiliana itakuwa powa. Lakini sijaelewa kama ni kutaka kuanzisha kikundi on the ground hapo Bongo na kuweka pa kutania pawe jf. Kama wazo ni la namna hiyo.. tutawaaunga mkono kwa kuhakikisha kuwa mnakuwa na faragha yenu hapa JF na mnasimamia wenyewe ukumbi wenu na mtatuwekea wenyewe masharti ya kushirikiana nanyi. Mwenye wazo naomba unipitishie ili nijue jinsi ya kuwaunga mkono. Haijalishi kama mko CCM au CUF au mnachukia kabisa siasa!
 
Back
Top Bottom