Uchaguzi 2020 Umoja wa wanafunzi TAHLISO wamuunga mkono Magufuli

Nashindwa kufikiria mambo yangekuwaje endapo tamko hilo lingekuwa la kuunga mkono CHADEMA. Leo watu wangetoa mapovu. Wengine wangesema msiingize siasa vyuoni. Akina Sirro nao wangejitokeza wakitoa onyo kali dhidi ya uvunjivu wa amani. Yaani kila mtu angekuwa anatoa povu lake. Lakini kwa kuwa anayeungwa mkono ni Magufuli, hakuna ubaya wowote!
 
Ngoja wamalize chuo waje mtaani ndipo watakumbuka hayo maneno vizuri, hakuna boom mtaani, ajira hazipo, biashara hazitoki kabisa
 
Mbwa kula kuku sio habari ila jogoo kumkamata na kumla Mbwa, hiyo itakuwa breaking news. Ingekuwa ajabu sana eti hawa watu waandae kikao, waite media na kudeclear kumuunga mkono hadharani Membe au Lissu.
 
Kuna member mmoja alidai wanafunzi wote wanamuunga mkono Lissu, lakini ukweli wenyewe ni huu hapa.-
View attachment 1532928

Wanafunzi wametoa msimamo kuelekea uchaguzi Mkuu 2020, Msimamo wao ni kuwa wanaungana na watanzania wote wenye mapenzi mema kumuunga mkono Rais John Pombe Joseph Magufuli
Kadi za kupiga kura Hamna ,hamkujiandikishwa,mnamuugaje Rais mkono?
 
Hawataki kuajiriwa hawa watu? Wenzao wako bench since 2016
Kwa fikra zako unafikiri Lissu atawaajiri wote? Hakuna Rais wa kutatua ajira ila wananchi wenyewe kwa kuanzisha biashara na viwanda kama Mo Dewji. Watanzania lazima waelewe Ulaya watu wamesoma kuanzisha biashara na viwanda kuajiri wengine ndiyo maana wana nafasi zaidi za kazi, hata hivyo ajira bado ni finyu.
 
Back
Top Bottom