Umoja wa wabunge wa Mtwara

Namahochi

Senior Member
Jan 1, 2016
138
98
Nimefarijika kuckia wabuge wote wa majimbo yote ya mtwara hasa wale wanaounganishwa na barabara ya mtwara mjini, Nanyamba, Tatahimba, na Newala, wametengeneza combination bila kujali itikadi ya vyama vyao ili kuakikisha barabara hii inajengwa kwa kiwango cha lami.

Ikumbukwe kuwa barabara hii ni chanzo kikubwa cha mapato ya miji hiyo na uchumi wa taifa pia, Ikumbukwe pia barabara hiyo ambayo haijawai kuwa na lami tangu dunia ilivyoumbwa licha ya kuhaidiwa na serikali zote zilipita.

Barabara hii inatumiwa na magari makubwa yenye uzito hasa kipindi cha msimu wa korosho lkn haipati matengezo ya kutosha hasa baada ya msimu kishwa.

Chanzo: Pride Radio
 
Aisee hiyo Barabara kama unaugua tumbo ukiwa unapita yaani hali yake haielezeki iko na mashimo telee au kama vile umepanda horse. kama wameungana kuhakikisha barabara Mtwara Newala inawekwa lami ni kheri
 
Back
Top Bottom