Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Viongozi waandamizi wa vyama mbalimbali vya upinzani leo watazungumza na waandishi wa habari. Watazungumzia maazimio ya #Azimio la Zanzibar.

Muda: Saa tano kamili asubuhi

Eneo: Makao Makuu ya CHAUMMA, Makumbusho, Dar es salaam.

======

UPDATES;

Viongozi Waandamizi wa Vyama mbalimbali vya Upinzani ACT, CUF na CHAUMMA wamefungua kesi Mahakama Kuu ya TZ Kanda ya DSM kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa minajili ya kupitishwa kuwa sheria, kesi hiyo itatajwa kesho kwa mara ya kwanza.

Wanataka muswada wa vyama vya siasa ujadiliwe kabla ya kupitishwa kuwa sheria itakayozuia vyama hivyo visifanye mikutano ya hadhara.

Vyama mbadala tumefanya juhudi kupinga mswada huu, tumetoka matamko, tumeshirikisha nchi wahisahi, mashirika ya kimataifa, AZAKI hapa nchini na viongozi wa dini, hizi ndizo hatua tumechukua kupinga.

Serikali imepeleka bungeni muswada wa sheria ya vyama vya siasa unaohalalisha agizo la Rais Magufuli mkoani Singinga mwaka 2016 kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na kufanya shughuli za kisiasa kuwa suala la jinai. - Zitto Kabwe.

Ni mswada unao kwenda kufifisha nguvu ya vyama vya siasa baada ya vyama vya siasa kuimalika na kuwa na uwezo wa kushindana kwa hoja.

Muswada huo unalenga kumfanya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa na Mamlaka ya Usimamizi (Regulatory Authority), na kuwa na mamlaka ya kuingilia shughuli za kiutawala na maamuzi ya ndani ya vyama vya siasa ikiwemo kusimamisha / kumfukuza mtu uanachama.


"Hatujajadili suala hili bungeni kama mnavyofahamu bunge limejaa wabunge wa CCM, na wabunge wa CCM wengi ni makasuku"- Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

"Walalamikaji (Applicants) kwa niaba ya vyama ni Waheshimiwa Joran Lwehabura Bashange, Salim Abdalla Rashid Bimani na Zitto Zuberi Kabwe. Mlalamikiwa (Respondent) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali."


Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa kujadiliwa na Bunge kwa ajili ya kuupitishwa kuwa sheria.

Kesi hiyo imefunguliwa Desemba 20,2018 ikitarajiwa kuanza kusikilizwa kesho Ijumaa Januari 4,2019 huku mlalamikiwa akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Akisoma tamko la umoja huo leo Alhamisi Januari 03, 2019, Kiongozi wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema muswada huo unakinzana na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 hivyo ni muhimu kwao kuupinga.

Amesema muswada huo unalenga kuvikandamiza vyama vya siasa na kufanya shughuli zote za kisiasa kuwa jinai.

“Tunawaomba wanachama wetu wote kesho tufike kwa wingi mahakamani kusikiliza kesi hii, wanademokrasia waone kwamba hatujakaa tunachukua hatua,” amesema Zitto.
=========​
Imefunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania, case no. 31/2018 ipo mbele ya jopo la majaji 3, Sehel, J., Maghimbi, J., na Masoud, J.
 
Nafikir sasa ni muda kwa vyama vya upinzani kuwa na makao makuu ya pamoja ili kuimarisha umoja huo, kuliko kukaa ofisi za uchochoroni mnatia aibu, mkiwa katika ofsi halali inayojulikana Tanzania nzima hata vikao vyenu vitakuwa na uhalali wa kiwango kisicho cha kubughudhiwa, sababu kitaaminiwa.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom