Umoja wa Ulaya watoa wito kwa Marekani kusitisha adhabu ya kifo inayoendelea kutekelezwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Jumuiya ya Ulaya (EU) imetoa wito kwa serikali ya Marekani kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo ya unyongaji iliyoanzishwa tena kufuatia uamuzi uliochukuliwa.

Peter Stano ambaye ni Msemaji wa Kamati ya EU, alitoa maelezo kuhusu suala hilo na kubainisha hofu waliyokuwa nayo dhidi ya serikali ya Marekani kwa kuanza tena kutekeleza hukumu ya kifo ya unyongaji kufuatia uamuzi uliochukuliwa baada ya takriban miaka 20.

Akisisitiza kuwa EU inapinga vikali hukumu ya kifo, Stano alisema kwamba unyongaji ni hukumu ya kikatili inayokiuka haki za kibinadamu, na haiwezi kusawazisha makosa ya mtuhumiwa baada ya utekelezaji.

Stano alisema, "EU inatoa wito kwa serikali ya Marekani kuondoa uamuzi huo na kusitisha hukumu zote za kifo za unyongaji zilizotolewa na ngazi za juu."

Stano pia alifahamisha kuwa hukumu nyingi za kifo zilizotekelezwa na serikali ya Marekani ya ngazi za juu zinatofautiana na hukumu za serikali za majimbo na dunia nzima kwa ujumla.

Baada ya uamuzi kuhusu hukumu ya kifo kuchukuliwa tena mwezi Julai, serikali ya Marekani ilitekeleza hukumu hiyo na watu 8 wakanyongwa.
 
Binafsi naunga mkono hukumu ya kifo kwa watu aliothibitika kufanya unyama juu ya binadamu wenzao.

Mfano juzi alinyongwa bwana Orlando Hall, huyu alimteka binti mdogo wa miaka 14, akambaka kwa zaidi ya siku 2 kisha akampiga na kisha kumzika akiwa hai, huyo mtu ni wa kuonea huruma?

Hua nashangaa wauaji wengi wakiua hua wanaogopa hukumu ya kifo, watakubali makosa iki wasihukumiwe kifo ama watakata rufaa wasiuwawe.

Aliyeua auwawe.
 
Kitu ambacho EU wanashindwa kuelewa ni kwamba hukumu ya kifo hailengi tu kumpa adhabu muuaji, ni zaidi ya hapo....'kuwa protect raia wema"

Na namna nzuri ya ku wa protect ni kumuondoa huyu mbaya, kumuondoa completely kwamba hawezi kupata access tena ya kutekeleza uhalifu kwa watu wengine.

Kumuweka kifungoni for life ni solution pia, ila inakumbana na changamoto mbalimbali kama;
  • Huyu muuaji kutoroka na kwenda kuleta madhara zaidi kwa watu wengine
  • Muuaji kuleta madhara akiwa huko huko gerezani
Mfano mtu kama Charles Merrit aliyeua baba, mama na watoto wadogo wawili under 5 years, motive kubwa ikiwa kufunika madeni makubwa ya mikopo aliyokua amekopa kwa hii family....mtu kama huyo aachwe aishi?

Hata akipewa life sentence then akafanikiwa kutoroka chances ni kwamba atawaua wengine, kuepusha hilo inabidi yeye afe, haitasaidia kumrudisha aliyepoea, ila itawalinda waliobaki.
 
Naona hii si kwasababu wanaonewa huruma.. Kuna kesi ambazo mtuhumiwa anapewa bila makosa..
 
Kitu ambacho EU wanashindwa kuelewa ni kwamba hukumu ya kifo hailengi tu kumpa adhabu muuaji, ni zaidi ya hapo....'kuwa protect raia wema"

Na namna nzuri ya ku wa protect ni kumuondoa huyu mbaya, kumuondoa completely kwamba hawezi kupata access tena ya kutekeleza uhalifu kwa watu wengine.

Kumuweka kifungoni for life ni solution pia, ila inakumbana na changamoto mbalimbali kama;
  • Huyu muuaji kutoroka na kwenda kuleta madhara zaidi kwa watu wengine
  • Muuaji kuleta madhara akiwa huko huko gerezani
Mfano mtu kama Charles Merrit aliyeua baba, mama na watoto wadogo wawili under 5 years, motive kubwa ikiwa kufunika madeni makubwa ya mikopo aliyokua amekopa kwa hii family....mtu kama huyo aachwe aishi?

Hata akipewa life sentence then akafanikiwa kutoroka chances ni kwamba atawaua wengine, kuepusha hilo inabidi yeye afe, haitasaidia kumrudisha aliyepoea, ila itawalinda waliobaki.
Sio tu hilo, rasilimali chache zilizopo zitumike kuhudumia jamii yenye mahitaji. Kumfunga maisha kutaongeza gharama za kumtunza na kumlisha na kumhudumia mtu ambae hakujali maisha ya watu wengine, hizo pesa za kumtunza akiwa gerezani zitumike kufanya kazi nyingine ya maendeleo au zitumike kusaidia wanaohitaji.

Kifungo cha maisha sio suluhisho, suluhisho ni kumuondoa mtu ambae hakujali thamani ya maisha ya binadamu wengine.
 
  • Thanks
Reactions: Pep

Naam, Hakimu
 
Back
Top Bottom